Kama haufanyi mambo haya hauna haki ya kumiliki pesa au mali; utaishia kutamani tu na umasikini hautakuacha

Kama haufanyi mambo haya hauna haki ya kumiliki pesa au mali; utaishia kutamani tu na umasikini hautakuacha

Bado naona kama umeegemea kwenye nadharia zaidi. Hebu fafanua vizuri kwa mifano halisi (practical examples) huku ukizingatia mazingira yetu haya yenye utitiri wa kodi za TRA na tozo za kila aina. Maana wengi wanapambana sana lakini wanaishia tu kupata hela ya kula na kuendesha familia zao lakini siyo kutajirika. Hawa wanakosea wapi?

Inaonekana una fomyula ya utajiri ila hujaiweka wazi kama ilivyo kawaida yenu matajiri na watia hamasa (motivational speakers). Huwa mnaishia kugusia gusia tu nadharia za juu juu na kamwe huwa hamtoi codes zote.

Hebu funguka mkuu jinsi ulivyoweza kutajirika kihalali kabisa katika mazingira haya ya Tanzania bila connections zilizokuwezesha kukwepa kodi, kuingiza bidhaa feki n.k.

Utatusaidia wengi; na Mungu Akubariki sana kwa moyo wako huu mwema 🙏🏿
Utajiri ni siri
 
Hakuna formula maalumu ila kuna mambo ukiyafanya Kwa kujua au kutojua unakuwa tajiri ndiyo maana baadhi ya wataalamu wa uchumi wanaamini kuwa kuna sayansi ya utajiri. Ikumbukwe kuwa raslimali ni chache "scarce" hivyo matumizi mazuri ya raslimali yoyote ile ni code mojawapo.

Kodi kweli ni changamoto hususani maeneo ya mijini katika Taifa letu ikiambatana na aina ya biashara na namna tunavyoziendesha, mifumo ya Serikali yetu kupata Kodi ni changamoto nyingine. Jambo zuri kwa nchi yetu ni kwamba tunasoko kubwa na matatizo ni mengi kuliko biashara zilizopo.
 
Ukweli mchungu lakini ndivyo ulivyo, Ili dawa iingie wakati mwingine sindano kwanza. Moja kwa moja kwenye hoja ni kwamba kwamba kama hakuna huduma au bidhaa unayoizalisha na kuitoa kwa jamii kama mbadilishano kutafuta utajiri bila njia hiyo ni kujighilibu akili.

Mahitaji ya jamii yako ndiyo utajiri wako, utajiri mwingi upo kwenye changamoto na matatizo ya jamii. Huduma au bidhaa unazozizalisha na kuzisambaza Ili kutatua kero mbalimbali katika jamii yako ndiyo suri ya mafanikio yako.

Kuna matatizo kila mahali hivyo kuna utajiri kila mahali amka Anza kufumbua macho ya akili yako uone. Pesa ni njia tu ya kubadilishana huduma au bidhaa weka kipaumbele katika kuiona huduma au bidhaa yako Kwa jamii.

Mtu anaweza kukupa pesa na zisikusaidie chochote Kwa sababu pesa ni njia tu ya kubadilishana, tafuta cha kubadilisha kwanza Kwa kuangalia jamii yako inahitaji nini.
Easy said than doing..
 
Semin ukweli mnapiga madeal haramu ndio mnafungua biashara zenu za halali
emoji23.png

Easy said than doing..
Naam! Likisemwa lipo na linatakiwa kufanywa, kuonekana gumu kwa mtu binafsi haimaanishi kila mtu hawezi kulifanya Mkuu..
 
Hizo siri ni zipi mkuu.
Ila za kishirikina na kijambaka sizitaki
mimi sio tajiri ila kuna moja niliigundua baada ya kufatilia sana siasa za marekani,

kuhonga wanasiasa(lobbying) wakurahisishie mambo mfano tozo za bandarini

pia kuna kukwepa kodi ila inakua rahisi ikifanywa kwa kuambatana na hiyo ya kwanza
 
Ni kweli.
Huduma au bidhaa.
Ila bidhaa ndio inayoleta utajiri usiochosha kuliko huduma.

Dunia ya sasa inahama kwenye utajiri wa kukomaa wanaenda kwenye passive income.

Mfano unaebook, na umeitafutia marketing agency wa maana. Baada ya hapo unakua unaokota pesa huku bidhaa yako inatoka sokoni kimyakimya duniani kote.

Huduma kama unategemewa wewe lazima ife siku usipokuwepo. Pia kwenye list ya mabilionea laki wa dunia hakuna aliyetajirika kwa kutoa huduma.

Nitakubali kukosolewa.
Weeee! Ivi searching engine like chrome, na apps like Facebook,X , tuachane navyo twende like Microsoft ni huduma au bidhaa tuaze hapo kwanza
 
Back
Top Bottom