Kama hauna njaa acha kazi msinisumbue!

Kama hauna njaa acha kazi msinisumbue!

mkuu wabongo wengi wanaishia kuwa vilema humo ndani, pengine hapo SBC-Pepsi
Hili nakubaliana na wewe 100% .
Kuna mzee mwaka wa 4 sasa hajalipwa na amevunjika kila siku ni kuzungushana.

Bora niuze matunda au kuchoma kuku buguruni sio kwenda kwa dewji kufa.

Kazi za viwandani bora uwe na skills sio kibarua utaumia na hakuna mtu ana muda na wewe.
 
wakati nasoma bandiko hili niko kiwanda cha uchanaji mbao daaah jamaa hawana kitendea kazi chochote sio barakoa, miwani wala mabuti magumu

kifupi mazingira,ni hovyo na posho ni iyo buku tano kwa siku
Huwa ninamshangaa kijana anayeumia kubeba bando kwa mo dewji au viroba kwa bakhresa.

Vijana wengi hatutaki kazi kwa kusema watanionaje.

Ukiuza matunda ukapata sehemu nzuri utafurahia maisha yako, na kipato chako kitakuwa kizuri ambacho hakichoshi mwili na akili to the extent.

Kama huna skills viwandani ni reserve utaumia sana, nishakuwepo humo naelewa na sasshiv mafanya biashara vyangu maisha ni tofauti.
 
Jamani katika harakati za kutafuta kazi, vibarua na ajira rasmi. Wengi tumeangukia sekta binafsi.

Aloo huku watu wanasota mbaya, kuna viwanda hapo vingunguti malipo ni bukutano per day. Unaingia asubuhi mpaka saa 12 jioni. Wengine wanaingia usiku.

Ili upate hizo kazi lazima uhonge mlinzi wa gardaworld ama section foremen na hiyo bukutano yenu mtapewa mwisho wa wiki.

Kuna taasisi pia nilifanya nayo kazi, ilifikia hatua unasaidiwa hela ya msosi na client wako na mkilia kwa Manager kuwa mshahara hautoshi, Manager anasema kama hauna njaa acha kazi!

Hivi najiuliza maofisa kazi, wizara ya kazi na ajira, Osha, WCF na watu wa haki za binadamu mnaijua hali wanayopitia Watanzania wenzenu humo viwandani na sekta binafsi?
Hao uliowataja wapo kwa ajili ya maslahi yao tu sio kutetea wapiga kura wa ccm.
 
Jamani katika harakati za kutafuta kazi, vibarua na ajira rasmi. Wengi tumeangukia sekta binafsi.

Aloo huku watu wanasota mbaya, kuna viwanda hapo vingunguti malipo ni bukutano per day. Unaingia asubuhi mpaka saa 12 jioni. Wengine wanaingia usiku.

Ili upate hizo kazi lazima uhonge mlinzi wa gardaworld ama section foremen na hiyo bukutano yenu mtapewa mwisho wa wiki.

Kuna taasisi pia nilifanya nayo kazi, ilifikia hatua unasaidiwa hela ya msosi na client wako na mkilia kwa Manager kuwa mshahara hautoshi, Manager anasema kama hauna njaa acha kazi!

Hivi najiuliza maofisa kazi, wizara ya kazi na ajira, Osha, WCF na watu wa haki za binadamu mnaijua hali wanayopitia Watanzania wenzenu humo viwandani na sekta binafsi?
Nchi imeuzwa na vijana hawajielewi.

Usipojielewa na kushirikiana uratumika sana, mnooo
 
Hivi najiuliza maofisa kazi, wizara ya kazi na ajira, Osha, WCF na watu wa haki za binadamu mnaijua hali wanayopitia Watanzania wenzenu humo viwandani na sekta binafsi?
Hawa Maofisa ni Wanyama sana halafu ni Makatili kupindukia na hawa ndio wanaowapa Waajiri viburi, maana hawafuati maadili ya kazi yao. Wananuka rushwa hawa. Mkuu la msingi pambana kwa kila namna ili uwe na cha kwako ukiendeleze na Wewe uwaajiri wengine.
 
Back
Top Bottom