Kama hauna njaa acha kazi msinisumbue!

Kama hauna njaa acha kazi msinisumbue!

Jamani katika harakati za kutafuta kazi, vibarua na ajira rasmi. Wengi tumeangukia sekta binafsi.

Aloo huku watu wanasota mbaya, kuna viwanda hapo vingunguti malipo ni bukutano per day. Unaingia asubuhi mpaka saa 12 jioni. Wengine wanaingia usiku.

Ili upate hizo kazi lazima uhonge mlinzi wa gardaworld ama section foremen na hiyo bukutano yenu mtapewa mwisho wa wiki.

Kuna taasisi pia nilifanya nayo kazi, ilifikia hatua unasaidiwa hela ya msosi na client wako na mkilia kwa Manager kuwa mshahara hautoshi, Manager anasema kama hauna njaa acha kazi!

Hivi najiuliza maofisa kazi, wizara ya kazi na ajira, Osha, WCF na watu wa haki za binadamu mnaijua hali wanayopitia Watanzania wenzenu humo viwandani na sekta binafsi?

Ukilalamika wewe pekee yako lazima ufukuzwe inatakiwa mlalamike wafanyakazi wote kwa sauti moja
Lakini pia ni ngumu sana watu kulalamika wote sababu ya njaa za watu kwahiyo ni ukandamizaji tu mwanzo mwisho
 
bora saidia fundi, nalamba 15,000 kwa kutwa. Sema na yenyewe haina uhakika wa kila siku. Maisha ni changamoto sana hasa kwa vijana.

Aisee mkuu hii saidia fundi nisaidie connection 😐
 
Hivi najiuliza maofisa kazi, wizara ya kazi na ajira, Osha, WCF na watu wa haki za binadamu mnaijua hali wanayopitia Watanzania wenzenu humo viwandani na sekta binafsi?
Sorry huenda ukaona ni mateso...lakini changamoto tuliyonayo wengi ni kudhani kisa unafanya kazi basi mshahara bora na maokoto makubwa ni haki yako, kila sector binafsi unayoona nyingi katika hizo zinapambana katika level yake kuwa hapo zilipo....kama unahisi ni rahisi upewe wewe uone kama haifi mikononi mwako....tunawaza kuvuna bila kupanda...amini kuwa kama kila kitu kingekuwa kinawezekana kufanyika na mashine bila uwepo wa binadam basi wengi wangetumia mashine lakini uwezo hauruhusu...
 
Naijua dhiki naijua njaa Ina ladha gani..

Kitabu Cha zaburi kina chapter 150 nilisoma na kutafakari Sana nilitumia miezi 3 usiku na mchana mpaka kumaliza chapter hizo 150..

Ilifika kipindi nikawaza labda MUNGU hajaweka better day kwangu..mama yangu mzazi alinambia mwanangu @Dr am 4 real siku yako IPO na uta sahau haya yoteee

Sijisifii Mimi nilikua na akili shuleni na nimefaulu vyema kila ngazi ya kielimu Ila kwenye Maisha na kupata kazi nilisugua Sana Gaga

Asante mwenyezi Mungu Sasa nimesahau Asante kwa neema na milango ya RIDHIKI uliyo ifungulia is IMMEASURABLE 🙏🙏 🙏

Neno langu kwa vijana tusikate tamaa tufanye kile tunacho kiamini kwa bidii Kama Ni mpira wa miguu cheza, Kama Ni music fanya, Kama Ni biashara fanya kwa bidii, Kama Ni kilimo fanya kwa bidii one day YES😊😊
 
changamoto tuliyonayo wengi ni kudhani kisa unafanya kazi basi mshahara bora na maokoto makubwa ni haki yako
Hivi kima cha chini cha mshahara (ambacho nadhani ni 300k) hakiwahusu hao wenye viwanda?
 
Kuna muwekezaji mmoja hapo mwanza wa kuitwa la kairo ana kiwanda kinatengeneza makorokoro kibao yanayofanyika pale ni huzuni, kiukwel masikini hana haki hapa duniani
 
Jamani katika harakati za kutafuta kazi, vibarua na ajira rasmi. Wengi tumeangukia sekta binafsi.

Aloo huku watu wanasota mbaya, kuna viwanda hapo vingunguti malipo ni bukutano per day. Unaingia asubuhi mpaka saa 12 jioni. Wengine wanaingia usiku.

Ili upate hizo kazi lazima uhonge mlinzi wa gardaworld ama section foremen na hiyo bukutano yenu mtapewa mwisho wa wiki.

Kuna taasisi pia nilifanya nayo kazi, ilifikia hatua unasaidiwa hela ya msosi na client wako na mkilia kwa Manager kuwa mshahara hautoshi, Manager anasema kama hauna njaa acha kazi!

Hivi najiuliza maofisa kazi, wizara ya kazi na ajira, Osha, WCF na watu wa haki za binadamu mnaijua hali wanayopitia Watanzania wenzenu humo viwandani na sekta binafsi?
Wanaijua sana na ndio wako nyuma ya camera.
Mkataba wako unasoma 11500/- ila inayokufikia wewe ni hiyo uliyosema na yenyewe pia mkataba unaoneshwa na ndio uiosaini upo.
 
Hivi kima cha chini cha mshahara (ambacho nadhani ni 300k) hakiwahusu hao wenye viwanda?
Hizi ni siasa ndugu....tuchukukulie baada ya yote ya kiserikali tra, osha, halmashauri na mengineyo kulingana na kazi yenyewe tuje kwenye uzalishaji na tulipe hiki kima cha chini kisa ni kiwanda unadhani tunatoboa....mara nyingi unapoona hizo kazi zinatangazwa au zinakuwepo mtoa kazi anasema na uwezo wake wa malipo kwa kazi husika kama unaona malipo hayo kulingana na njaa zako unaweza basi fanya na usilalamike kuwa unaonewa....la acha katafute kule ambako unalingana napo....huwezi jua akilipa zaidi ya hapo anafilisika na hatutamuona tena sokoni .
 
Back
Top Bottom