Kama hawa wote wanaomtuhumu Heche wamenunuliwa, CHADEMA hamna makada!

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Huwa tunapenda sana kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Hata hivyo majibu ya namna hiyo hayatibu ugonjwa.

Mtaji wa kwanza wa chama cha siasa ni wanachama waaminifu ambao wapo tayari kukitetea, kukilinda na kukipigania chama chao.

Tafakari, kama chama viongozi wake, wanaweza nunuliwa kwa bei ya TSh. 2,000,000/- tunazoambiwa ili wakiharibu chama chao, sasa kuna chama hapo?

Tuwe wa kweli, kuna mahali vyama vya upinzani havifanyi vizuri. Na mahali hapo ni malezi ya makada wake. Hii ndio sababu kila siku tunasikia malalamiko ya wanachama wao kununuliwa.

Waswahili husema baniani mbaya kiatu chake dawa. Kama CHADEMA wanalijua hili ni vyema wakaenda kujifunza CCM namna ya kuwalea makada wao kuwa viongozi waaminifu.
 
Mtoa mada huogopi kutukanwa?!!!! Huko hauhitajiki ukweli, Bali kumpigia magoti lissu na heche tu. Ukienda tofauti basi utapatiwa majina yoooote mabaya na kashfa, kubwa ikiwa "umenunuliwa na ccm".

Kwa chama hicho, tuhuma za kununuliwa makada zimekuwa zikisikika miaka mingi tangu enzi za kina zitto, lijualikali, mashinji n.k Hadi kufika Leo wimbo ukiwa huohuo; ni dhahiri mtoa mada uko sahihi. Lakini asili ya wachadema wengi waliopo humu NI upumbavu basi watakutulana tu.
 
Vyama vya upinzani hakuna hela ,so wanajipambania kivyao . Pesa zinazopatikani ni kurataibu shughuli za kichama ambazo ni wakubwa tu , unafikiria uwe kada huko Muheza pesa itakufikia , kitu ambacho ni tofauti na CCM ; wana miradi mingi .
 
Ni kweli comrade. Ifike mahali hizi story za "wamenunuliwa" zifike mwisho. Ni wakati sasa nao waanze kununua makada wa CCM kama wataweza.
 
Vyama vya upinzani hakuna hela ,so wanajipambania kivyao . Pesa zinazopatikani ni kurataibu shughuli za kichama ambazo ni wakubwa tu , unafikiria uwe kada huko Muheza pesa itakufikia , kitu ambacho ni tofauti na CCM ; wana miradi mingi .
Sawa vyama vya upinzani hawana hela, lakini kwanini wanunulike? Umasikini sio tiketi ya kujiuza
 
Huwa tunapenda sana kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Hata hivyo majibu ya namna hiyo hayatibu ugonjwa.

Mtaji wa kwanza wa chama cha siasa ni wanachama waaminifu ambao wapo tayari kukitetea, kukilonda na kukipigania chama chao.

Tafakari, kama chama viongozi wake, wanaweza nunuliwa kwa bei ya TSh. 2,000,000/- tunazoambiwa ili wakiharibu chama chao, sasa kuna chama hapo?

Tuwe wa kweli, kuna mahali vyama vya upinzani havifanyi vizuri. Na mahali hapo ni malezi ya makada wake. Hii ndio sababu kila siku tunasikia malalamiko ya wanachama wao kununuliwa.

Waswahili husema baniani mbaya kiatu chake dawa. Kama CHADEMA wanalijua hili ni vyema wakaenda kujifunza CCM namna ya kuwalea makada wao kuwa viongozi waaminifu.
Ccm ni chama dola, kina pesa za kutosha ndiyo maana huwezi sikia wakilalamika wanachama wake kununuliwa. Wapinzani watapa wapi pesa za kununua wanachama wa CCM? Lakini CCM hakuna mwanachama yeyote mwaminifu, kama yupo mtaje hata mmoja
 
Wana CCM wote ni waaminifu kwa chama chao ndio maana hujawahi sikia wamenunuliwa kutekeleza project za wapinzani wao
 
mleta uzi ni mchumia tumbo flani hivi mpuuzeni wameshinda asilimia mia nane na wanakubalika na wana kila kitu na bado wanaona wivu kwa mtu kuchangiwa bukubuku, yaani ukitaka kujua maffiisiiemu yamefilisika ndio hapo sasa, mnaacha kuhangaika na maisha ya watu magumu mnahangaika na masiasa uchwara.
 
Sawa vyama vya upinzani hawana hela, lakini kwanini wanunulike? Umasikini sio tiketi ya kujiuza
Unajua Swalika na kujijibu mwenyewe propaganda lumumba inaongozwa na mazuzu Yani I'd mbili zote unaziongoza mwenyewe Sasa hapa Id mbili buku 7 au 14 hebu nisanue comredi.
 
Back
Top Bottom