Huwa tunapenda sana kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Hata hivyo majibu ya namna hiyo hayatibu ugonjwa.
Mtaji wa kwanza wa chama cha siasa ni wanachama waaminifu ambao wapo tayari kukitetea, kukilinda na kukipigania chama chao.
Tafakari, kama chama viongozi wake, wanaweza nunuliwa kwa bei ya TSh. 2,000,000/- tunazoambiwa ili wakiharibu chama chao, sasa kuna chama hapo?
Tuwe wa kweli, kuna mahali vyama vya upinzani havifanyi vizuri. Na mahali hapo ni malezi ya makada wake. Hii ndio sababu kila siku tunasikia malalamiko ya wanachama wao kununuliwa.
Waswahili husema baniani mbaya kiatu chake dawa. Kama CHADEMA wanalijua hili ni vyema wakaenda kujifunza CCM namna ya kuwalea makada wao kuwa viongozi waaminifu.