Kama Hayati Magufuli alikuwa anaipeleka nchi shimoni tujuzwe. Watendaji wengi aliowafurumusha wamerejeshwa huku wake wakifurumushwa

Kama Hayati Magufuli alikuwa anaipeleka nchi shimoni tujuzwe. Watendaji wengi aliowafurumusha wamerejeshwa huku wake wakifurumushwa

Bana all in all mimi tu nina furaha sana, watu tuliishi kwa hofu, kutishana kila siku kama tupo vitani,, wakati maisha ni haya haya tu, maisha yetu mafupi tu kwann tutishane na tuache kufurahia? Hata kama naishi kwa kunywa uji tu na familia yangu ndani nalala kwa amani, poa sana

Me nachoelewa hii nchi watu asilimia kubwa wana furaha!! Wanaolalamika wengi ni wale chawa wa mwendazake waliokuwa wanafurahia watu kuteswa, kuumizwa na kupotezwa!!

Ila Karma is a bitch!! Wengi wao Mungu kashawalila sawa sawa na matendo yao!! Bado mmoja aliyekuwa anajiita mungu dar es salaam[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mie Nina furaha sana. Tuko huru. Yale mambo ya mara umemtukana rais sijui wewe msaliti ooh unahujumu au unashirikiana na mabeberu yamekwisha kafa na mavi yake tumboni hakupata hata muda wa kuomba maji.

Bado huyo Makonda anayakujibu.

Kumbukeni waliokuwa wanateswa wote yeye alikuwa anakuja mbele ya vyombo vya habari na kusema Fulani atapatikana siku Fulani.

1. Mo dewj
2. Roma
3. Nondo

Inawezekana huyu Makonda anajua Ben Sanane Yuko wapi na Azory anajua wako wapi.

Ni suala la Muda tu
 
Watendaji wengi ambao hayati Magufuli alikuwa akiamka ama usiku wa manane akiwafurumusha hatimaye wengi wanarejeshwa kwa kasi tena wakipanda vyeo maradufu. Kwa uchache

1. Lawrence Mafuru alifurumushwa kutoka msajili hazina kwa kupinga kuwa hakuna mkurugenzi anayelipwa milioni 15. Leo amepandishwa cheo hadi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambayo hazina ipo chini yake.

2. Felschemi Mramba alifurumushwa kutoka ukurugenzi mkuu wa Tanesco leo ni katibu mkuu nishati ambayo Tanesco ipo chini yake.

3. Nape Mosses Nnauye alifurumushwa kutoka waziri wa habari na michezo. Leo kateuliwa kwenye nafasi ile ile.

Pia wapo watu wa karibu sana na hayati ambao walikuwa wakiaminika naye sana na walipewa kipaumbele huku tukiaminishwa kuwa upigaji umetokomezwa serikalini na kila fedha sasa inaenda sehemu sahihi. Cha ajabu mwaka mmoja baada ya Magufuli kufariki watu hao wamefurumushwa kwa kasi ya ajabu.

1. Uongozi wote wa wizara ya nishati na Tanesco uliokuwa umesimikwa na hayati umeondolewa na sasa wamerejeshwa wale waliokuwa wakiongoza hapo kabla. Nini tatizo?

2. Ndugu wa karibu wa hayati bwana Dotto James aliyekuwa hazina hapo kabla alihamishwa kwenda viwanda na biashara na sasa amefurumushwa kabisa. Nini tatizo?

3. Mawaziri pendwa wa hayati kina Kabudi, Kitila, Lukuvi wamefurumushwa. Hata waliobaki ni kama hawana amani.

4. Chawa wote wa hayati kwa sasa wameufyata kweli kweli kuanzia mitaani, kwenye media mpaka maofisini. Kwa ufupi ni kuwa wazee wa kutetea legacy wamepigwa ganzi vibaya mno.

Mradi pendwa wa hayati wa bwawa la umeme alilolipa jina la Nyerere unaenda kwa kusua sua mno na ni kama January Makamba hana mzuka nao. Hauongelei na wala haupi kipaumbele.

Vitambulisho vya machinga hatimaye vimezikwa na hakuna anayejishughulisha navyo tena.

Cha ajabu wakati anatumbua na kufanya haya yote msaidizi wake mkuu alikuwepo na huyo msaidizi alipochukua tu hatamu ameyabadilisha kwa kasi ya ajabu! Lipo tatizo tena kubwa. Sasa kuliko kuficha ficha moto kwa blanketi ni bora tukaambiwa mapema ikiwa hayati alibugi pakubwa.
Kipindi kile mlisema kila zama na kitabu chake. Sasa nawakumbusha hiki ni kitabu kingine.
 
Nimeami heri Mungu alimuumbia binadamu kifo,tungekuwa tunaishi milele,tungeoneana sana tena sana.
 
Nimeami heri Mungu alimuumbia binadamu kifo,tungekuwa tunaishi milele,tungeoneana sana tena sana.
Na kifo cha huyu mwamba kwa hakika kimetoa funzo.
 
Back
Top Bottom