Kama hewa itatoka katika eneo lililo na uwazi, je ni kitu gani huzuia hewa isitoke nje ya uso wa dunia?

🤣 hii si tulifundishwa darasa la tano huko! hebu Google ozone layer
 
Hewa kama oksijeni haitoki kwenye uso wa dunia na kupotelea angani kutokana na sababu kadhaa kuu:

1. Mvuto wa Dunia (Gravity): Mvuto wa dunia huvuta kila kitu, ikiwemo molekuli za gesi, kuelekea katikati ya dunia. Hii ina maana kuwa gesi katika angahewa zinavutiwa kuelekea uso wa dunia, hivyo kuzuia gesi kama oksijeni kutoroka kwenda angani.

2. Tabaka za Angahewa: Dunia ina tabaka mbalimbali za angahewa (troposphere, stratosphere, mesosphere, na thermosphere) ambazo husaidia kuhifadhi gesi. Tabaka hizi hufanya kama kizuizi kinachozuia gesi kutoka kwenye tabaka za chini kupotea kwenda anga za mbali.

3. Mzunguko wa Dunia: Mzunguko wa dunia unaathiri jinsi gesi zinavyosambaa. Usiku na mchana, pamoja na misimu tofauti, husaidia kusawazisha joto na usambazaji wa gesi katika angahewa, hivyo kuzuia gesi kutoroka kwa urahisi.

4. Shinikizo la Anga: Katika uso wa dunia, shinikizo la anga ni kubwa zaidi ikilinganishwa na juu zaidi kwenye angahewa. Shinikizo hili linasaidia kushikilia gesi katika tabaka za chini za angahewa.

5. Mfumo wa Sumaku wa Dunia (Magnetic Field): Ingawa sio sababu kuu kwa gesi kama oksijeni, mfumo wa sumaku wa dunia husaidia kulinda angahewa dhidi ya upepo wa jua (solar wind), ambao unaweza kuondoa baadhi ya molekuli za gesi kutoka katika angahewa.

Kwa sababu hizi, gesi muhimu kama oksijeni huendelea kuwepo katika tabaka za chini za angahewa, zikihifadhiwa na mvuto wa dunia na tabaka za angahewa ambazo zinazuia kupotelea angani.
 
Habari za jioni wadau....

Kama mnakumbuka nilileta mada kuhusu chanzo au asili ya Oxygen, Nashukuru wadau walinipa elimu nzuri kuhusu Oxygen na nikaelewa vyema.

Leo pia nina swali kuhusu Oxygen au hewa.

Kwa mujibu wa sayansi, asili ya hewa au mazingira yake ni lazima iwe katika eneo ambalo limefungwa, ndani yake kuwe na pressure na kizuizi ili hewa hiyo isitoke.

Kwa mujibu wa NASA, dunia haipo closed, viumbe na vitu vyote vipo nje ya uso wa dunia,dunia inaelea katika space ambayo ipo wazi pande zote na haina mwisho.

Je, inakuwaje mpaka duniani panakuwa na mgandamizo wa hewa ingali pande zote zipo wazi?

View attachment 3057848

Naomba wadau wa sayansi ya mazingira mnijuze kuhusu hili....
MIND YOU.........Oxygen is denser than air and the universe is covered by air, therefore oxygen produced by plants cannot escape from the surface of the earth.
Mfano rahisi ni kama ukichanganya mafuta na maji , lazima mafuta yakae juu na maji chini, ndo mfano wa hewa na oxygen .
 
Baharini kunajulikana kijiografia kuwa ni bondeni. Sasa inawezekanaje kitu chenye ujazonene mkubwa, kama udaivyo, kisiwe huko bondeni?

You're clearly missing something important.
Mkuu, kuhusu bahari pia kuna jambo la msingi sana kujadili...
 
Mgandamizo wa hewa una kikomo kadiri unavyozidi kwenda juu, huu Mgandamizo huvuta hewa kurudi kwenye surface ya dunia juu zaidi inapotezea control yake.
Bado unajichanganya.

Iwapo huko juu mgandamizo wa hewa ni mdogo kuliko chini kwenye uso wa dunia (jambo ambalo ni kweli kabisa), tungetegemea hewa izidi kupanda huko juu kwa mujibu wa kanuni ya uwaalifu wa hewa (diffusion), na hatimaye kutoka kwenye ukanda au kingo za juu za dunia -- kama anavyodai mleta-mada.
 
Maji ambayo yanageuka kuwa mvua hayapo mbali kwa upande wa juu, yanaelea kama mawingu.
Yanapotoka kwenye uso wa dunia, si yanatoka katika hali ya hewa, sasa kama yanatoka katika hali hiyo kwa nini yasifike mbali?

Pili je concentration ya oxygen ni sawa jinsi unaenda angani?
Yani kwenye usawa wa bahari, na juu ya mlima kilimanjaro concentration ya oxygen ni sawa?
 
Hewa kama oksijeni haitoki kwenye uso wa dunia na kupotelea angani kutokana na sababu kadhaa kuu:

1. Mvuto wa Dunia (Gravity): Mvuto wa dunia huvuta kila kitu, ikiwemo molekuli za gesi, kuelekea katikati ya dunia. Hii ina maana kuwa gesi katika angahewa zinavutiwa kuelekea uso wa dunia, hivyo kuzuia gesi kama oksijeni kutoroka kwenda angani.

2. Tabaka za Angahewa: Dunia ina tabaka mbalimbali za angahewa (troposphere, stratosphere, mesosphere, na thermosphere) ambazo husaidia kuhifadhi gesi. Tabaka hizi hufanya kama kizuizi kinachozuia gesi kutoka kwenye tabaka za chini kupotea kwenda anga za mbali.

3. Mzunguko wa Dunia: Mzunguko wa dunia unaathiri jinsi gesi zinavyosambaa. Usiku na mchana, pamoja na misimu tofauti, husaidia kusawazisha joto na usambazaji wa gesi katika angahewa, hivyo kuzuia gesi kutoroka kwa urahisi.

4. Shinikizo la Anga: Katika uso wa dunia, shinikizo la anga ni kubwa zaidi ikilinganishwa na juu zaidi kwenye angahewa. Shinikizo hili linasaidia kushikilia gesi katika tabaka za chini za angahewa.

5. Mfumo wa Sumaku wa Dunia (Magnetic Field): Ingawa sio sababu kuu kwa gesi kama oksijeni, mfumo wa sumaku wa dunia husaidia kulinda angahewa dhidi ya upepo wa jua (solar wind), ambao unaweza kuondoa baadhi ya molekuli za gesi kutoka katika angahewa.

Kwa sababu hizi, gesi muhimu kama oksijeni huendelea kuwepo katika tabaka za chini za angahewa, zikihifadhiwa na mvuto wa dunia na tabaka za angahewa ambazo zinazuia kupotelea angani.
Mizunguko wa dunia unahusika kivipi na kutunza au kuzuia hewa isitoroke?
 
Yanapotoka kwenye uso wa dunia, si yanatoka katika hali ya hewa, sasa kama yanatoka katika hali hiyo kwa nini yasifike mbali?

Pili je concentration ya oxygen ni sawa jinsi unaenda angani?
Yani kwenye usawa wa bahari, na juu ya mlima kilimanjaro concentration ya oxygen ni sawa?
Kadri unavyopanda kwenda juu oxygen inapungua.
 
MIND YOU.........Oxygen is denser than air and the universe is covered by air, therefore oxygen produced by plants cannot escape from the surface of the earth.
Mfano rahisi ni kama ukichanganya mafuta na maji , lazima mafuta yakae juu na maji chini, ndo mfano wa hewa na oxygen .
Sawa kuna matabaka ya hewa, lakini sayansi inasema ni lazima eneo liwe limefungwa na pasiwe na nafasi ya kutoka
 
Ndyo nilikimbia physics, Google bado sijaona jibu la uhakika
Jibu ni rahisi sana.

Ni sawa na kuuliza kwa nini vitu havitoki nje ya ukanda wa dunia? Kwa nini vinaendelea kubaki duniani na havitoki kwenda kwenye shuba ama bwango (space)?

Kwa sababu vinavutwa na kani ya dunia. Dunia ni kama sumaku. Kila kitu juu yake, hadi hewa, ni sawa na chuma -- huvutwa na kubaki duniani muda wote.
 
Mkuu maana yangu ni kwamba,mada yako imekaa kisayansi na kitafiti,humu ndani hakuna wanasayansi na watafiti wa kisayansi!

Humu wengi ni wapiga Zomari tu,ndo maana nikapendekeza ya kwamba,kama ulikuwa unahitaji majibu yatakayokufanya upate uelewa Moana utakaokusaidia katika maisha yako kutokana na swali lako,ni vema ungeenda Google ambako Kuna majibu yaliyokwisha kufanyiwa tafiti za Kisayansi na wanasayansi nguli wa Ulimwengu!

Tofauti na hapo uenda unahitaji hapa watu wajichangamshe tu lakini sidhani kama utapata majibu ya kueleweka tofauti na Google!
Sio kila mtu ni afsa usafirishaji, nisome hapo juu
 
Jibu ni rahisi sana.

Ni sawa na kuuliza kwa nini vitu havitoki nje ya ukanda wa dunia? Kwa nini vinaendelea kubaki duniani na havitoki kwenda kwenye shuba ama bwango (space)?

Kwa sababu vinavutwa na kani ya dunia. Dunia ni kama sumaku. Kila kitu juu yake, hadi hewa, ni sawa na chuma -- huvutwa na kubaki duniani muda wote.
Ukichukua mawe ukayaweka juu ya meza, yataweza kutoka au kuelea juu ya anga?

Dunia ni kama meza, kitu kikiwa juu yake tayari kinaweka uzito, hivyo hakiwezi kuelea au kupaa juu. Labda hicho kitu kiwe na uwezo wa kupaa au kusogea kwa kutumia uwezo wake binafsi
 
Yanapotoka kwenye uso wa dunia, si yanatoka katika hali ya hewa, sasa kama yanatoka katika hali hiyo kwa nini yasifike mbali?

Pili je concentration ya oxygen ni sawa jinsi unaenda angani?
Yani kwenye usawa wa bahari, na juu ya mlima kilimanjaro concentration ya oxygen ni sawa?
Mimi pia nahitaji kujua kwanini yasifike mbali, kwanini yasifike kwenye space? Ni kitu gani huzuia?
 
Ndege ni physical object, hewa haionekani....

Ni kipi husababisha hewa ibaki ndani ya uso wa dunia na isifike juu?
Bro ,umeshajibiwa kuwa ni Gravity...
Gravity ina effects kulingana na uzito wa matter....Heavier the matter,the more it is affected.....
 
Back
Top Bottom