Kama Hii Ndio Situation ya Bomoa Bomoa ya Ubungo na Kimara Bila Fidia, Then Faraja Pekee ni Kuwa, Watafidiwa Tuu!.

Whatever wrong you do towards others, my friend think twice. In the face of others you will defend your self... ooh it is the law, or whatever excuse you can put across for justification. In the face of yourself you know you did not do the right thing. This will never change until you die, and after your death your spirit will remember this karma and will be in trouble. At that time it can no longer ask for amnesty, or forgiveness. YOU WILL REINCARNATE in a different body just to suffer similar sufferings like those you inflict on to others before you died. You can also suffer it before you die, when you have no power any more. WATCH OUT!
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la kuwafariji, watu wote waliokumbwa na bomoa bomoa popote pale bila fidia, japo hiyo bomoa bomoa katika baadhi ya maeneo, imefanyika kwa dhulma kubwa, ikiwemo kupuuzwa kwa zuio la mahakama, then waathirika na wahanga wa bomoa bomoa hii, wasiwe na wasiwasi, kwa sababu mwisho wa siku, wote watafidiwa, ila fidia hiyo sio lazima ifidiwe sasa italipwa tuu hata mbele ya safari.

Kwa vile sisi binadamu wote tunaoishi humu duniani, tunasemekana, tuko safarini tuu, mambo yote tunayokutana nayo ni mapito tuu ya dunia hii, na yote huishia mwisho wa safari yetu katika makao yetu ya milele.

Baada ya kusikia hadi jengo la Tanesco litabomolewa bila fidia, na ile miundombinu ya DRT pele Ungo iliyogharimu mabilioni ya shilingi kwa fedha za mkopo, nayo pia itabomolewa ma kujengwa upya, then nimepitia historia ya hii bomoa bomoa,

Nimejiridhisha ni kweli kabisa hii bomoa bomoa, haitendi haki katika baadhi ya maeneo, hivyo faraja pekee kwa waliobomolewa Ubungo na Kimara na kwinginepo bila fidia, ni kuwa, hatimaye wote watafidiwa tuu, hata kama fidia hiyo sio sasa, then watafidiwa mbele ya safari, na wakati huo huo, hao waliowatenda nao pia watalipwa haki yao stahiki zao kwa mujibu wa matendo yao, malipo ni hapa hapa duniani au mbele ya safari.

Fidia hiyo itapatikana kupitia hukumu pekee ya haki hapa duniani inayoitwa hukumu ya karma.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili ...
Poleni sana!.
Paskali
Ni kweli mzee umenena vyema kwani kwasasa hawayaoni wamevaa makofia makubwa imewaziba kutokuona mbele. Ila kama mungu atatuweka hai baadhi yetu wataiona hiyo siku. Hakuna aliejua kuwa kuna siku yule Jongwe wa Zimbabwe atatikiswa. Ila kwasasa anatikiswa ni heshima tu bado kapewa. Ndio maana nasema baadhi viongozi wa kiafrika wakishaingia madarakani wanajiona wao ndio mungu. Hawajali ila hukumu itatoka hiyo siku. Asante Pascal
 
Hatutaweza kuibadilisha kama sheria zitaendelea kupindishwa; ni lazima waliojenga pasipo sahihi waondoshwe, kutowalipa fidia ni funzo tosha kwa wengine kutokurubia kosa hilo
 
..ni vema kuwajibu kwa picha watawala dhalimu hawa....maana dhambi imewapa uziwi wa kutosikia vilio vya watu....picha hizi angalau ziwafungue akili zao ili waone wanavyowatendea dhambi maskini wa nchi hii kwa jeuri na fedhuli kuu....utawala unaowaletea umaskini watu wake ni utawala wa shetani.....ni muda tu utasema...

View attachment 631583 View attachment 631584 ingawa umetumia tafsida kueleza ulicho maanisha mi ntakuongezea msemo

akili fupi uamua kwa ufupi wake; mfano angalia hizo picha hapo chini;-
View attachment 631584 View attachment 631583 View attachment 631584 o
 
Tz Tz ni nchi ya ajabu hasa kipindi hiki cha awamu ya 5 kwani mambo mengi hayana mipango wala dira ya kuongoza nchi: 1. Hali za maisha ni walio wengi ni ngumu sana, 2. Bomoa bomoa ya baadhi mikoa inaupendeleo mfano walioambiwa wawe na human face lakini Kimara hakuna cha human face bali bomoa tu, 3. Watu wanapotea na wengine wanapigwa risasi,
 
Utabiri wako unaanza kutimia.......

World Bank wamesema hawawezi jenga Hiyo barabara iwapo watu hawajalipwa fidia ya ubomoaji huo!

Ndiyo tatizo la kupata kiongozi wa ngazi za juu akiwa masikini, anataka na nyinyi nanyi wote muishi kimasikini!
 
Utabiri wako unaanza kutimia.......

World Bank wamesema hawawezi jenga Hiyo barabara iwapo watu hawajalipwa fidia ya ubomoaji huo!
Barabara itajengwa na hakuna fidia hapo..... world bank wametishia tuuu lakini hela watatoa...
 
Japo JJMnyika ameomba wafidiwe, boss amegoma kuwafidia kuwa hawatafidiwa, naomba kuendelea kuwafariji waliobomolewa bila fidia kwa kuwahakikishia kuwa mwisho wa siku, lazima watafidiwa tuu, na waliowabomolea bila fidia nao pia watafidiwa.

P
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la kuwafariji, watu wote waliokumbwa na bomoa bomoa popote pale bila fidia, japo hiyo bomoa bomoa katika baadhi ya maeneo, imefanyika kwa dhulma kubwa, ikiwemo kupuuzwa kwa zuio la mahakama, then waathirika na wahanga wa bomoa bomoa hii, wasiwe na wasiwasi, kwa sababu mwisho wa siku, wote watafidiwa, ila fidia hiyo sio lazima ifidiwe sasa italipwa tuu hata mbele ya safari.

Kwa vile sisi binadamu wote tunaoishi humu duniani, tunasemekana, tuko safarini tuu, mambo yote tunayokutana nayo ni mapito tuu ya dunia hii, na yote huishia mwisho wa safari yetu katika makao yetu ya milele.

Baada ya kusikia hadi jengo la Tanesco litabomolewa bila fidia, na ile miundombinu ya DRT pele Ungo iliyogharimu mabilioni ya shilingi kwa fedha za mkopo, nayo pia itabomolewa ma kujengwa upya, then nimepitia historia ya hii bomoa bomoa,

Nimejiridhisha ni kweli kabisa hii bomoa bomoa, haitendi haki katika baadhi ya maeneo, hivyo faraja pekee kwa waliobomolewa Ubungo na Kimara na kwinginepo bila fidia, ni kuwa, hatimaye wote watafidiwa tuu, hata kama fidia hiyo sio sasa, then watafidiwa mbele ya safari, na wakati huo huo, hao waliowatenda nao pia watalipwa haki yao stahiki zao kwa mujibu wa matendo yao, malipo ni hapa hapa duniani au mbele ya safari.

Fidia hiyo itapatikana kupitia hukumu pekee ya haki hapa duniani inayoitwa hukumu ya karma.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili ...
Poleni sana!.
Paskali
Kubenea Jana alifuatwa akambiwa acha husingumze....mambo magumu sana
 
Pascal pamoja na kumsikia jiwe bado unaendelea kuwafariji wahanga?! Labda kama unaongelea faraja ya kuona maeneo yao zimejengwa njia nane za barabara ambazo hawakuwahi kuziona hapo mwanzo.
Japo JJMnyika ameomba wafidiwe, boss amegoma kuwafidia kuwa hawatafidiwa, naomba kuendelea kuwafariji waliobomolewa bila fidia kwa kuwahakikishia kuwa mwisho wa siku, lazima watafidiwa tuu, na waliowabomolea bila fidia nao pia watafidiwa.

P
 
Whatever wrong you do towards others, my friend think twice. In the face of others you will defend your self... ooh it is the law, or whatever excuse you can put across for justification. In the face of yourself you know you did not do the right thing. This will never change until you die, and after your death your spirit will remember this karma and will be in trouble. At that time it can no longer ask for amnesty, or forgiveness. YOU WILL REINCARNATE in a different body just to suffer similar sufferings like those you inflict on to others before you died. You can also suffer it before you die, when you have no power any more. WATCH OUT!
Mkuu Mfamaji, maneno makali haya...ila huu ndio ukweli wenyewe, mwenye masikio na asikie.
P
 
Pascal pamoja na kumsikia jiwe bado unaendelea kuwafariji wahanga?! Labda kama unaongelea faraja ya kuona maeneo yao zimejengwa njia nane za barabara ambazo hawakuwahi kuziona hapo mwanzo.
Nimejiridhisha ni kweli kabisa hii bomoa bomoa, haitendi haki katika baadhi ya maeneo, hivyo faraja pekee kwa waliobomolewa Ubungo na Kimara na kwinginepo bila fidia, ni kuwa, hatimaye wote watafidiwa tuu, hata kama fidia hiyo sio sasa, then watafidiwa mbele ya safari, na wakati huo huo, hao waliowatenda nao pia watalipwa haki yao stahiki zao kwa mujibu wa matendo yao, malipo ni hapa hapa duniani au mbele ya safari.

Fidia hiyo itapatikana kupitia hukumu pekee ya haki hapa duniani inayoitwa hukumu ya karma.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili ...
Poleni sana kwa sasa ila mtafidiwa tuu
P
 
Back
Top Bottom