Wanabodi,
Hili ni bandiko la kuwafariji, watu wote waliokumbwa na bomoa bomoa popote pale bila fidia, japo hiyo bomoa bomoa katika baadhi ya maeneo, imefanyika kwa dhulma kubwa, ikiwemo kupuuzwa kwa zuio la mahakama, then waathirika na wahanga wa bomoa bomoa hii, wasiwe na wasiwasi kabisa, machungu yao, mateso yao, maumivu yao, vilio vyao na machozi yao hayatapotea bure, kwa sababu kuna baadhi yao, hizo nyumba zao, wamezijenga kwa machozi, jasho na damu, na hapo walipofika ndio mwisho wa uwezo wao, hivyo kubomolewa bila fidia ni sawa na na Kuwazika wazima na kufa huku unajiona, then watu hawa nawapa pole, na kuwapa neno moja tuu la faraja kuwa mwisho wa siku, ni lazima watafidiwa tuu, ila fidia hiyo sio lazima ifidiwe sasa, italipwa tuu hata mbele ya safari lakini na watesi wao nao pia wana malipo yao.
Kwa vile sisi binadamu wote tunaoishi humu duniani, tunasemekana, ni tuko safarini tuu, mambo yote tunayokutana nayo ni mapito tuu ya dunia hii, na yote huishia mwisho wa safari yetu katika makao yetu ya milele, hivyo usiumize sana moyo wako na roho yako kwa vitu vya kupita, hata kama umepoteza mali, mali, majumba, fedha na vyote vionekanavyo ni vitu vya kupita tuu, kitu muhimu sana kwako ni roho yako na nafsi yako pekee, na ni hiyo roho/nafsi ndio itafidiwa.
Baada ya kusikia hadi jengo la Tanesco litabomolewa bila fidia, na ile miundombinu ya DRT pale Ubungo stend ya mkoa, iliyogharimu mabilioni ya shilingi kwa fedha za mkopo, utakaolipwa na Watanzania wote, nayo pia itabomolewa na kujengwa upya, then nimejikuta nikilazimika kupitia historia ya hii bomoa bomoa,
Nimejiridhisha ni kweli kabisa hii bomoa bomoa, haitendi haki katika baadhi ya maeneo, hivyo faraja pekee kwa waliobomolewa Ubungo na Kimara na kwinginepo bila fidia, ni kuwa, hatimaye wote watafidiwa tuu, hata kama fidia hiyo sio sasa, lakini lazima watafidiwa mbele ya safari, na hata kama fidia hiyo itawakuta wameisha tangulia mbele ya haki, fidia hiyo italipwa kwa watoto wao na watoto wa watoto wao.
Na wakati huo huo, hao waliowatenda nao pia watalipwa haki yao na stahiki zao kwa mujibu wa matendo yao, na malipo hayo ni hapa hapa duniani au mbele ya safari.
Fidia hiyo itapatikana kupitia hukumu pekee ya haki hapa duniani inayoitwa hukumu ya karma.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili ...
Poleni sana!.
Paskali