Kama hii ndiyo idadi ya CHADEMA kutoka mikoa kuja kwenye kesi ya Mbowe, basi chama kimepoteza mvuto kabisa

Tutajie maendeleo yaliyoletwa na ccm,yaani kama baada ya miaka 60,Bado mnatuambia mnataka kutuletea maendeleo nyie ni vilaza,kitu gani hicho Cha kutumia miaka 60 kuleta?
Maendeleo waliyokuletea Chadema ni yapi?
 
Ndugu zangu fanyeni kazi kwa bidii ukikamatwa pale kisutu ,mnyika au pambalu hakujui wewe utaishia kuitesa familia yako na wazazi wako tu na kuuza mashamba au nyumba ili kukutoa wewe
 
Akina maria sarungi, lemma, lisuu na fatuma karume wanawadanganya watu wakati wao wamejificha kwenye keyboard ya computer wajitokeze wao sasa hivi hakuna.mmachinga mjinga aaache biashara zake anazofanya kwa uhuru akaandamane never
Hao akina Maria Sarungi, Fatuma Karume na Lema leo hawakutokea mahakamani. Wajinga ndio waliwao.
 
Tutajie maendeleo yaliyoletwa na ccm,yaani kama baada ya miaka 60,Bado mnatuambia mnataka kutuletea maendeleo nyie ni vilaza,kitu gani hicho Cha kutumia miaka 60 kuleta?
ndugu katikanchi za kiafrica unaweza kuiongelea vibaya nchi hiikweli? uhru ulionao maendeleo yaliyopo unakunywa maji unapata umeme hakuna matukio mabaya kkama somalia hebu niambie tu wewe ni baya gani ulionalo hapa nchini? nchi za kiafrica zote maskini ingawaje tunajikongoja unategemea chadema wakiingia madarakani ndiyo wataleta maajabugani tuache ushabiki wa kihuni ho
 
Unaangalia Wingi au Ubora bwashee?
aina ya watu kama mleta uzi ndio wale wale waliokuwa waksema 'Mungu kaondoa corona tz", wao wanawaza kuwa maisha ni kujikomba na teuzi tu hata kama zinagharimu damu za wenzao.
kwa hiyo hata cdm wasipotokea kabisa ndio itaondoa ukweli kwamba hii ni kesi ya kutengeneza? Asubiri tu siku yakimkuta
 
Kipigp baba.... Watanzania awapendi tabu za kijingajinga. watangulize watoto wao kwanza ndipo na sisi tuwafute..... wacha mchezo na mirungi cha POLICE
 
CCM haiwezi kujivunia kujitokeza kwa watu wachache kwenye kesi ya CADEMA kuwa ni nguvu kwao. Wajue kinacho Fanya hivyo ni jeshi wanalo tumia. Ikizoekeja hiyo, watatafuta njia ya kupambana na jeshi, huo ndo utakuwa mwisho wa amani
 
Kipind CDM wananguvu kubwa Katibu mkuu alikuwa Dr. Wilbroad Slaaa na Naibu wake alikuwa Zitto Zuber Kabwe.

Leo Katibu mkuu wa CDM na Naibu wake wote wawili uwezo wao kisiasa hauufikii wala kuukaribia uwezo wa Zitto Zuber Kabwe .

Usije ukakufuru kumfananisha Mnyika na Dr. Slaa.

Maelezo hayo juu ndio kiini cha hali ya uungwaji mkono wa watanzania Kwa CDM wakat ule na sasa.
 
Usijidanganye, ondoa majeshi utajua nani anaushawishi kati ya CCM na CHADEMA
 
CCM haina ushawishi kwa watu Bali jeshi linazuia kujulikana kuwa CCM hsikubaliki katika jamii yetu
 
Utakuwa CCM inayo simama nyuma ya jeshi kuonyesha nguvu zake fake.
 
Wanaelimisha nini kwa hizo purukushani zao na serikali? mimi sijataka wapoe au wawe wamoto bali watumie akili ili wajue wakati gani ufanye kitu gani na kwa vp ili upate unachokipigania na sio wakati wote kuingia kwenye purukushani na serikali ili usionekane umepoa et haki yako hujavunja.
 
Lengo lako la kutaka wanasiasa wanaoangalia masilahi ya wananchi kwanza kupitia upinzani kwa kweli bado halijatimia... i mean kwa sasa hakuna mpinzani wa aina hiyo hapa Tanzania. Shibodo aliwahi kuifadhili chadema kwa kuipa mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kujenga au kuboresha ofisi za chama hicho nchi nzima na zingine wachimbishe vizima kwa ajili ya wananchi mbali mbali katika majimbo wanayoyasimamia. Ila kilichofanyika ni tofauti na alivyotarajia mfadhili wao.

Mbowe alichukua yale mabilioni akaenda kuyaficha nje ya nchi na zilizobaki alienda kula bata na familia yake Dubai bila kuzuga japo kwa kupaka rangi ili kumhadaa mfadhili. Lkn kama hiyo haitoshi kila mwezi alikuwa anajilipa mamilioni ya shilingi kupitia ruzuku ya chama kwa kisingizio cha kujilipa madeni huku akiwaacha viongozi wa kwenye mashina ya chama wakifanya kazi ya kukitangaza chama bila mshahara, hapo hatujazungumzia mamilioni ya michango ya wabunge waliyochanga kwa miaka mi5, na ile waliyokuwa wanachangisha katika mikutano yao kipindi cha uchaguzi mkuu.

Kifupi kama kweli jamaa wana uchungu na wananchi kama walivyotumia udhaifu wako kukudanganya basi Mbowe na genge lake wangejiuzulu kwa kukubali kupokea hao unaoita wanasiasa njaa na mafisadi waingie ndani ya chama na kuwapitisha kugombea nafasi kubwa za uraisi nk adi kupelekea chama kushindwa kushinda, na kupoteza matumaini ya wanachama wengi kwa chama na uongozi kwa ujumla. Ukiona mtu ametoa boko na bado hataki kuachia nafasi yake basi jua ana masilahi nayo.
 
Masikini ndo mikoa yote lol,
Watoto wa Mbowe walikuwepo?
 
Hiyo ilikuwa ni kesi na sio sensa ya wanacdm. Tumia kichwa kufikiri na sio kama fuvu la kubebea meno.
Fuvu la kubebea meno!! [emoji23][emoji23][emoji23] watu wa humu mna maneno sana asee...
 
Elewa hata hao kesi zao ziliitwa za kubambikiziwa #KESI ZAO ZILIHAKIKIWA KWANZA UPYA NA KUTHIBITISHWA NA NDIPO MTU ALIPOACHIWA HURU
 
Sasa kama hako kakikundi kadooogooooo ka wanachadema kamelazimisha mahakama ihamie video conference, kama yangekuja mafuriko, basi kesi ingefutwa kabisaaaa!

Hebu nikurudishe 2020. Tundu Lissu alipokelewa na wanachadema kadhaa. Alipokwenda Dodoma kuchukua fomu, kulikuwa na watu wachache sana. Sasa Fast Forward alipofika Dodoma tena wakati wa kampeni. Uliona mtiti ule?
Kwanini? Ni kweli upinzani wana kazi kubwa saaaanaaa ya kuwaunganisha watanzania. Sisi sio kama Kenya. Wala sio kama Zambia. Watanzania wengi ni watii wa mamlaka. Lakini wanataka mabadiliko. Walishayakosa ndani ya ccm, wanayatafuta nje ya ccm. Hili ccm wanalijua, ndio maana hakuna uchaguzi halali Tanzania. Ila watanzania wanapoona hapa kuna uwezekano wa kuiweka kando ccm, wanajitokeza kwa wingi. Ndio maana Tundu Lissu alipata mafuriko ya watu siku za mwishoni wa kampeni. Na ndio maana ccm walianza kumwekea vikwazo kibao.
Kwa kufanikiwa huku, believe me, si wanachadema tu, bali watanzania wengi zaidi watampigania Mbowe. Na kama rais Samia anajitetea alikuwa kweli ana nia ya kukutana na wapinzani, "ratiba zikaingiliana", basi maana yake atalazimika kutafuta namna yakukutana nao
 
Nadhani muda wao mwingi hawa CHADEMA wanautumia kupiga ganja. Sehemu kubwa ya mipango yao haifanani kabisa na mipango ya watu wanaotumia akili au busara ya kawaida!

Kwani umewa biushungi au Sirro wao wanasema je?
 
Elewa hata hao kesi zao ziliitwa za kubambikiziwa #KESI ZAO ZILIHAKIKIWA KWANZA UPYA NA KUTHIBITISHWA NA NDIPO MTU ALIPOACHIWA HURU

Kumbuka hata hao tulipiga kelele sana tu kuwa serikali dhalimu na taasisi zake zilikuwa zikibambikiza kesi.

Hata hii ni moja wapo.

Kumbuka Mbowe kesha shitakiwa kesi ngapi hadi leo. Haijawahi kutiwa hatiani hata katika moja ya hizo.

Bado haikifikirishi tu?

Subiri uone hata hii itakavyo kwisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…