Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,153
- 3,800
Polio, ndui, kifaduro, pepopunda, TB, nk ni chanjo ambazo wengi wetu tumechanjwa utotoni. Na huenda kupitia chanjo hizo ndiyo sababu ya kuwa hai hadi leo tunapotunisha misuli majukwaani.
Halikadhalika ukienda kwa upande wa Mifugo,kuna chanjo nyingi mifugo yetu huchanjwa kukinga magonjwa mbalimbali. Hivyo chanjo ni kitu muhimu kwa binadamu na wanyama hasa kwa magojwa yale yasiyotibika kwa tiba za kawaida.
Kwa uelewa wangu,zaidi ya 99% ya chanjo hizo za binadamu zimetengenezwa nje ya nchi( hasa ulaya) kupitia uangalizi wa Unicef na WHO. Ni nani aliwahi kuhoji kuhusu usalama wake? Na kama alihoji,ni hatua ,zipi za Serikali zilichukuliwa kupata mbadala wake? Na je, viongozi wa awamu zilizopita wangeamua kusitisha kuziingiza nchini, nini kingetokea?
Tumesikia kwenye vyombo vya habari kuhusu ligi inayoendelea kuhusu chanjo ya Covid- 19 hasa kwa nchi zetu changa kupanga kuikataa. Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa, kwa nchi changa, hofu siyo aina ya chanjo bali ni gharama kubwa za chanjo hiyo. Na yawezekana, ingetolewa kama msaada kama zile za Unicef kwa chanjo za watoto tusingesikia haya yote.
Kama ndiyo hivyo yaani kuogopa gharama,viongozi wetu wanapaswa kufahamu kuwa kipaumbele cha serikali yeyote ile kwa watu wake ni kulinda maisha yao! Kenya na baadhi ya nchi zinazotuzunguka wameshashaagiza au kuweka mipango ya kupata chanjo hiyo. Ni rai yangu kuwa,,nasi tuwe kwenye mstari wa pamoja na jirani zetu.
Na kama ipo agenda inayolenga kufafanua madhara yake,tucampaign kwa pamoja kuikataa. Mwl. Nyerere alipogundua IMF inayumbisha nchi maskini, alihamasisha na kuungana na nchi nyingi kuyakataa masharti ya IMF wakiwemo Nigeria ya kina Sani Abacha w, Zambia ya Mzee Kaunda
nk.
Hiyo approach ilifanya Wenye IMF kutikisika na kuanza kufuta baadhi ya misaada. Naamini hata viongozi wetu wa nchi hizi changa wanapaswa kutumia technique hiyo ya umoja pale wanapogundua kuna genuine reason ya kukataa jambo,na hapohapo wawe na mbadala. Covid-19 au 21 ni janga zito na siyo la kuisha leo wala kesho.
Siyo jambo la afya sana viongozi wa nchi zetu changa kuanza matamko ya kukinzana na juhudi yeyote ya awali ya kukabili tatizo la covid kama chanjo kwa staili ya majukwaa mepesimepesi.