Nilitaka kucheka hayo ya "Zanzibar...", hadi nilipokumbuka hayo ya mwanzo, kuhusu "kung'ang'ania kwake CCM."
Hivi haiwezekani kabisa kupambana humo ndani kwa ndani ya CCM yenyewe na kupata ushindi wa kuleta mabadiilko ndani ya chama hicho?
Tafadhari, naomba radhi kwa kuuliza swali kama hili linaloonekana kuwa la kipumbavu kabisa, lakini ukweli ni kuwa sijui jibu lake sahihi.
Ina maana huko ndani ya CCM, wote walioko huko sasa wanaamini kitu kimoja tu, maslahi yao, hakuna wengine wanaoona umuhimu wa maslahi ya nchi yao, na wao wakaamua kupambana humo humo ndani kwa ndani?
Binafsi, namshauri akazie hapo hapo. Katika mika yake iliyobaki kuwa bungeni, atumie fursa hiyo kujipambanua, na kuwaeleza waTanzania waelewe CCM ilikofikia.