MWALLA
JF-Expert Member
- Dec 12, 2006
- 16,952
- 10,500
kwa kukusaidia tu,....Zanzibar kwa maana ya unguja na pemba ipo sawa na jimbo la ilala!!!
Ama kweli utajua kama hujui
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya iliyofanyika Agost 2012, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina jumla ya wakazi wapatao 1,220,611, ambapo idadi ya Wanaume ni 595,928 na na wanawake ni 624,683
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imegawanyika katika Tarafa tatu (3) ambazo ni Ukonga , Ilala , na Kariakoo . ambapo ina jumla ya Kata Thelathini na tano (35) zikiwa na jumla ya Mitaa mia moja na hamsini na tatu (153)
Aidha Halmashauri ya Manispaa ina Majimbo matatu (3) ya Uchaguzi ambayo ni Ilala, Ukonga na Segerea.
Zanzibar ina Wapiga kura laki tano na 66, katika majimbo 50 ya visiwa vya Zanzibar, wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu. Watu wa Zanzibar ni wa asili mbalimbali, hasa watu wa asili ya Afrika Bantu, yakiwemo makabila ya Wahamidu na Watumbatu; halafu Waasia, awali kutoka India na nchi za Kiarabu.
Idadi ya wakazi wa Zanzibar ilikuwa 1,303,569 mwaka 2012, tarehe ya sensa ya mwisho, iliyoonyesha ongezeko la 3.1% kwa mwaka.
Karibu theluthi mbili ya watu wanaishi katika kisiwa cha Zanzibar (Unguja).