GE2025 Kama hujafa maandamano ya 29/10 basi wewe ni key board warrior tu, msituchoshe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mkuu 'Stuxnet', staha ingekuwa kwamba usubiri kidogo watu wawazike vijana hawa, na Samia apumue na kutafakari haya yote yaliyojili.

Lakini najuwa moyo wa kujipongeza unao msukumo mkubwa sana kuweza kuushinda; kwa hiyo imelazimu uje hapa mara moja hii kutupasha/kutukumbusha upumbavu wetu mkubwa tulio nao.

Basi mkuu, acha nikupe wewe na Samia Suluhu Hassan hongera zenu nyingi za ushindi wa damu za vijana hawa. Ninachojuwa mimi, hii damu kamwe haitaondoka akilini mwenu tena maisha yenu yote.

Kuhusu nafasi zetu wengine tuliokuwa tunaililia Tanzania yetu; usiwe na shaka hata kidogo kwamba kamwe hatukati tamaa.
In fact, kumwagika kwa damu ya hawa vijana ndiko kutakuwa kichocheo kikubwa kwetu kuzidi kuipigania nchi yetu kwa njia zozote zitakazo wezekana.

Kwa hiyo, usiwe na shaka, bado tupo pamoja sana na nyinyi.
 
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Sijaelewa ulichokiandika,

anyway, Hili n swali langu au n swali kwa huyo aliyenijumuisha?
 
..Ikulu pachafu namna ile?

..Maraisi wote wa muungano, na Zanzibar, wamekuwa wakiapishwa katika viwanja vya wazi, ambapo wananchi huhudhuria, sio mafichoni.
Samia ni Rais ama sio Rais? Mmemuondoa? Hata wewe intel zinaonesha haupo TZ na mmechocha watu wameuawa πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Sijaelewa ulichokiandika,

anyway, Hili n swali langu au n swali kwa huyo aliyenijumuisha?
Ni swali kwako. Na kama bado huelewi maana yake utakuwa hujitambui ni sehemu ipi unakosimamia wewe ndani ya taifa hili..
Huwezi kuwa mguu mmoja upande wa waovu; halafu wakati huo huo ujifanye huhusiki na lolote. Waovu hao hao watakuweka watakakoona kunakufaa.
 
Kaka tuponye nchi na kugangana mioyo. Naomba mambo ya siasa tuweke pembeni mkuu wangu kwa sasa sio mda wa kunangana huu. Watu wamepoteza ndugu ma marafiki. Moyo wangu umeinama sana kwa kilichotokea.
 
Kumbe hukuandamana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…