Kama hujajiandaa kuingia kwenye ndoa usiingiee kabisa

Kama hujajiandaa kuingia kwenye ndoa usiingiee kabisa

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Ndugu zangu za ASBH, najua wiki imeanza na kuna watu Ijumaa na Jumamosi wanatarajia kuoa. Vyema, nkasema niwashauri bado wana nafasi ya maamuzi hizi siku 4-5 zilizobaki.

Kama unahisi hauko tayari kuingia kwenye ndoa, usiingie. Huu ni ushauri wa bure... kwenye ndoa hakuna red carpet tu, kuna na mchanga na mavumbi.

Ukifanya maamuzi ya ndoa, jua umefanya uamuzi wa kupambana na Shetani. Ujiandae kweli kupambana na Shetani. Shetani kazi yake ni kuua na kuharibu, kwa hiyo kama ujajiandaa kupambana naye, usiingie kwenye ndoa.

Ndoa nyingi zimevunjika ama ziko kwa ICU siyo mapenzi ya wanandoa. Kuna Shetani ameingia ndani ya wanandoa anataka wasambaratike.

Kama ujawaza kujiandaa na machungu ya ndoa, basi hata usiwe na hisia za ndoa kabisa. Utakufa. Ndoa ni mapenzi ya Mungu, ndani ya hayo mapenzi Shetani huzunika sana. Ujue kuna wengi walikuwa malaya baada ya ndoa wakabadilika, Shetani anaumia sana.

Ndugu, bado una muda wa maamuzi, usikimbilie ndoa ukafurahisha watu, utalia.

Jitatu njema.
 
Safi Mkuu kwa andiko zuri sana! Haya ni baadhi ya kuongezea tu!
Usiingie kwenye ndoa kwa kigezo cha kuwafurahisha rafiki au ndugu! Utafeli vibaya sana! Watu hubadilika mapema sana, haswa jinsi ya kike maana hawa hutazama harusi na ndoa kama vitu ambavyo ni dhahania.
Hongera Mkuu
 
Pole Sana Pafu dady kwa yaliyokukuta..

Naimani hujaandika bure , yamekutokea.

Ila serious ndoa zinavunjika sana now, jumamosi iliyopita mwanandoa mtarajiwa kapigwa na bwana wake kwa kumfuma anachati na Xwake..

Ndoa ikahahirishwa hapo hapo..

Familia ya mwanamke inalia tu..
 
wamiliki wa ndoa wangejulikana tungebanana <siondizi> naoo....
 
Back
Top Bottom