Kama hujajipanga vizuri usichokoze ujenzi

Hiyo akiba kama haitakiwi kuguswa maana yake haitakiwi kutumika, na kama haitumiki basi hata isipokuwepo yote sawa tu.
Akiba inaguswa pale zinapotokea dharura kama ugonjwa,ajali,misiba,safari na mambo mengine ambayo huwa hayapo katika mipango hapo ndipo sehem sahihi ya kupeleka akiba yako ila kwa ww unaeishi kwa shemeji unalala sebuleni kama Tv akiba siyo ya muhimu kwako na Wala huwezi kujua ina umuhimu gan
 
Mkuu mimi na wewe ni ndugu nn maaana natembelea humo humo,nikiona kitu hakiwezekani nakuwa nakipa muda wa kujipanga upya ili tu nisiguse akiba.
Maisha ni sanaa mkuu huwa yanakufunza baada ya kukupa maumivu, mimi binafsi najali sana kuhusu akiba nikiona kitu nachotaka kufanya kitaharibu akiba naaacha kwanza, ukitumia hiyo mbinu wala ujenzi haiwezi kuwa mateso na hata Kama utateseka haitakua kwa kiwango kikubwa kama ukiwa unamaliza hadi akiba
 
Sawa
 
Ukitaka kujenga nyumba nzuri ila unauwezo wa kujenga nyumba ya kawaida fanya hivi.
1. Jenga hiyo nyumba ya Milion 30

2. Tangaza kuuza hiyo nyumba kwa Milion 50

3. Ikienda jenga ya Milion 40 na tangaza kuuza kwa Milion 70


Mpaka ufikie lengo la nyumba unayotaka, japo itakuchukua muda, tatizo wanawake zetu ndiyo waoga, ya kwangu ningesha uza kitambo kama siyo uoga wa mwanamke
 
yeah , kama walivyoshauri wadau huipaswi wakati unajenga kutumia mbaka pesa ya akiba inabidi uende taratibu.
- mwaka jana nilianza kumwaga mawe , nikaja msingini na kujenga kiti .nikatulia

- Mwaka huu , mwezi watu nikaanza simamisha kuta nusu nikatulia ilipofika mwezi wa sita nimemalizia kozi zilizobaki, kwasasa nimetulia napiga hesabu namna ya kupiga linta sina presh maana still plan zangu zipo ndani ya muda

- incase mungu akinijalia uzima kufikia mwezi wa kumi na moja ntakuwa nishamaliza na linta na kumalizia kozi za juu zilizobaki . Ila mbaka mwakani mwezi wa saba najua ntakuwa nishapaua kabisaa.

- hii picha chini inaonesha nilipokwamia kwa sasa najua ntatoboa tuu lazima nimiliki mjengo wangu lazimaaa
 
Hapo kwenye tofali 5000mbona nyingi sana mkuu bungalow hilo!??
 
Mungu mkubwa utamaliza,omba uwe na afya njema.
 
Napata Somo hapo mkuu!Hongera sana.
 
Kwa kipato cha wengi wetu si rahisi
Labda kama wewe Mungu kakubariki vikubwa zaidi
 
Inategemea kule mbali Bei rahisi ila karibu huku Bei ndefu kingine ukinunua kwa muhusika sio pesa ndefu unaweza kupata kwa 35k per square meter uko mbali hata 20k kwa square
Ila ni Vyema kujenga karibu. Ukijenga Mbali na City Center garama za usafiri zako, Pengine wife kama anafanya kazi na watoto wanaoenda Shule zinaweza fika laki 2 kwa mwezi😁na haya mafuta yanavyopanda kila kukicha ata kavitz unaweza kukipark
 
Naona bora kujenga karibu
Ila ni Vyema kujenga karibu. Ukijenga Mbali na City Center garama za usafiri zako, Pengine wife kama anafanya kazi na watoto wanaoenda Shule zinaweza fika laki 2 kwa mwezi😁na haya mafuta yanavyopanda kila kukicha ata kavitz unaweza kukipark
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…