Kama hujajipanga vizuri usichokoze ujenzi

Kama hujajipanga vizuri usichokoze ujenzi

Hapana,
Sio kweli. Ujenzi kama unataka kujenga we anza na chochote ulicho nacho. Mshahara wangu haujaongezeka sana Kwa hivi karibuni lakini nimemudu kujenga ndani ya miezi 6 nyumba kubwa tu na ikaisha kabisa.

Sasa nimejiuliza miaka ya nyuma Kwa mshahara almost huo huo nilikua nafanyia nini hata sijui.

Ukiwa na mentality hizo kwamba mpaka upate kikubwa ndio uanze ujenzi utaishia kua mpangaji milele
How much are u paid monthly ?
 
HII POINT KUBWA SANA, KAMA HUNA FAMILIA JENGA HATA CHUMBA KIMOJA, YANI JENGA KUTOKANA NA FAMILIA YAKO USIJENGE KAMA FASHION, HIYO PESA NYINGNE UNAWEKEZA SEHEMU ITAKAYOINGIZA PESA.
Yes correct jenga nyumba ya kawaida. Hela Inayobakia nunua hata Maeneo/viwanja uyatunze.baada ya.miaka.10 au.15 unauza unatapa.mkwaja.mzuri sana.
 
Mimi pia nilikua natishwa hivyo hivyo ila kujenga ni rahisi sana mzee

Mbinu unayotakiwa kutumia kwanza usijenge kama adhabu alaafu pili punguza matumizi yasiyo ya lazima na uanze ku save, ukisha save tenga kiasi Cha akiba alafu Anza ujenzi hakikisha ujenzi wako usiguse kabisa pesa ya akiba uliyo nayo.

Kama uliamua akiba yako iwe laki 3 fanya ufanyavyo tafuta hela tupia kwenye ujenzi ila huo ujenzi usiguse hiyo akiba yako, tafuta fundi akupigie hesabu ya vifaa na gharama za ufundi mtoe chake afanye kazi ila akiba yako ibaki palepale.

Epuka kujenga kwa kutumia hela zote Hadi kumaliza akiba yako yote utateseka zaidi na ujenzi hautakiwi uwe ni mateso.

Mbinu hizi za ujenzi tunatumia sisi wagangaa njaa na ukiweza kutumia hiyo mbinu utajenga Kama tajiri kumbe huna utajiri wowote na jengo litaisha bila maumivu
Hii mbinu sasa hivi mimi najenga nyumba ya pili ndani ya fensi yangu na hata sina presha maana nyumba ya kwanza ndimo ninamoishi na familia yangu,yaani nataka nije nijikite namiliki Apartments kiana iwapo MUNGU atanifadhili
 
Hivi viwanja huko kigamboni au pembeni ya mji bei zipoje jamani?
Watafute hawa kwenye mitandao bei za Kigamboni kwa Ndugulile ni kama hapo! Wa-follow hao jamaa watakupeleka mpaka kwenye viwanja.
Screenshot_20241204-052438_Instagram.jpg
 
Tunauza mbao kwa bei ya jumla na rejareja :-
2*2 fut12=2500
2*3 fut 12=3500
2*2 fut12(treated) ya dawa=2800
2*2 fut18(treated) ya dawa=5000
2*4 fut12 treated(ya dawa)=5000
2*4 fut12 isiyo ya dawa=4500
1*6 fut12=4500
1*8 fut12=8500
1*8fut12 ya fisher board(treated)=9500
1*10 fut12=14000
1*10fut 12 fisher board( treated)=15000
2*4 fut18(treated)=10000
2*6 fut12=8000
1*4 fut12=2800
2*6 fut 18=19000
Tunapatikana muda wote kwa namba za simu zifuatazo:-
----0759630751
----0687371138
----0654830416

vile vile kuna huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu pia Tunafanya delivery kwa wakazi wa Dar es salaam
Ofisi zetu zipo Tegeta kibaoni-Bagamoyo road
Nakucheki aisee
 
Wazee hebu nipeni ushauri
Nipo nataka kupunguza gharama kwenye kupaua

Nataka kutumia mirunda badala ya kutumia mbao 2*4 wanasema nayo inaubora mzuri tu.

Nipeni mawazo yenu.
 
Wazee hebu nipeni ushauri
Nipo nataka kupunguza gharama kwenye kupaua

Nataka kutumia mirunda badala ya kutumia mbao 2*4 wanasema nayo inaubora mzuri tu.

Nipeni mawazo yenu.
1. Kama unatumia msouth tumia mabati meupe
kuokoa gharama.
2. Kama unatumia mabati.meupe tafuta hela ununue mbao
 
Unaweza kufa na nyumba ukaacha hapo, otherwise jenga bila haraka, kwa awamu na taratibu uta enjoy

Ukifikia level vitu vya kingereza uwiiiiii ni stress juu ya stress hasa kama unafosi nyumba kuisha na budget yako ni ndogo

Hongereni watu mnaomiliki mabangalooooo

Hongereni mnaomiliki ghorofa
🤣🤣🤣😂😂
 
Nimeshtuka kuona huu uzi, hapa nna ujenzi nimeuanza km unanisema mimi 😹😹

Nasubiri nipaue niwafate Nmb wanipe pesa za kumalizia..!!
 
Mi sina stress coz sijachoka kupanga halafu sina familia yaani msela tupu ningeanza hata mwaka huu sema nabagua viwanja nataka cha kigamboni karibu na niwe na access ya kufika post mpaka kariakoo ... Vya mbali sana sitaki
Hakuna kwako mbali mkuu!
 
👍😃😄
Vitu vya kiingereza... Blandering, skimming, plaster etc😄
Ujenzi si lelemama.

Sometimes i wish watu wa Nhc, wangekuwa wanajenga kwenye makazi ya kawaida ya watu kulingana na ramani ya mtu husika, then tunawalipa robo tatu au nusu. Robo ya gharama au nusu nyingine unalipa polepole.

Kuna watu kweli wanapata kiharusi (stroke) kwasababu ya ujenzi wanadhani ni kurogwa kumbe stress za ujenzi.

Na ukimpata fundi mwenye mawenge ndio balaa hatari. Anakutajia vifaa vingi ambavyo havitumiki vyote au anachanganya cement ratio isiyo sahihi., na ile inayomwagika chini haangaiki kuizoa.

Misumari ikidondoka kama hakuna wa kuokota imekula kwako. Bati au mbao zinakatwa vipande vipande bila mpangilio anajua una hela.
Yaani kuset msingi fundi anahitaji mbao za 2x2 pieces kadhaa. Wakati fundi mwingine mzoefu naahitaji kama na misumari tu
 
Back
Top Bottom