Kama hujawahi kukutana na usumbufu, dharau na jeuri za watumishi wa serikali, utaendelea kutoona anachofanya Makonda

Kama hujawahi kukutana na usumbufu, dharau na jeuri za watumishi wa serikali, utaendelea kutoona anachofanya Makonda

Ukweli ni kwamba yawezekana makonda ana mapungufu yake kama mwanadamu mwingine yeyote. Lakini kwa kero za
Hapa👇👇👇 ndipo penye KERO KUBWA:
Quote" ......Lakini kwa kero za nyingi ya ofisini za uma hasa unapokuwa unahitaji huduma yenye viashiria vya maslahi, utazungushwa na kusumbuliwa kwa vitu vidogo sana, unapoteza muda, gharama ya fedha na gharama zingine nyingi."

Yeah! Utaulizwa maswali mengi yanayojirudia-rudia e.g. yalikuwa ni madai ya lini? Sh.ngapi.
Faili halionekani au iliwekwa kwenye faili gani (ilhali wanajua ww sio mtumishi wa ofisi hiyo.). Mara anapokea simu kutoka kwa rafiki na wanaanza kucheeeka.

Then unaambiwa "Tunaomba utupe muda ili tulifuatilie...........ukirudi baadaye unamkuta mhudumu mwingine sio yule uliyeongea naye kwanza. Naye huyo anaanza tena maswali yale yale..... Mwisho wa siku unachoka unaondoka na hasira zako na endapo akitokea mtu akakuuliza hatma ya ulichofuata ikoje? Unakuwa Huna jibu lililonyooka.

Wacha Konda awakikimishe tuu.:Cheergi:
 
Hapa👇👇👇 ndipo penye KERO KUBWA:
Quote" ......Lakini kwa kero za nyingi ya ofisini za uma hasa unapokuwa unahitaji huduma yenye viashiria vya maslahi, za hatma ya ulichofuata ikoje? Unakuwa Huna jibu lililonyooka.
Wacha Konda awakikimishe tuu.:Cheergi:

Mtanzania ukimwambia afuate utaratibu anadai unamsumbua, na hatimaye anaomba atoe kitu kidogo ili akwepe mchakato halali kisheria.

Hapa usiku huu, saa 11:44PM, ninapoandika nipo kazini.

Watanzania wanapenda short-cuts. Ukisisitiza utaratibu anakasirika kwamba unamuonea.

Kuna mmoja kadai hata kama rais ndiye kaweka utaratibu, basi kuna kuoneana huruma.

Mkiambiwa muwe mnaelewa.
 
Kinachofanyika hapa ni usanii... watu waje na suluhisho za matatizo za ukweli.

Ngoja nikupe mfano... kuna idea ilikuwa floated ya serikali kuanzisha "Inconvinience fee", kila huduma ya serikali iwe na ukomo wa muda; baada ya huo kuisha, na huduma haijapatikana, taasisi itakatwa pesa na mlipaji kurudishiwa.

Mtu umelipia huduma ya maji 100,000/- kila wiki inayochelewa, unarudishiwa 10,000/-. Taasisi za serikali zote zitapata adabu. Baada ya hapo, taasisi inayopoteza pesa nyingi, inaingia kwenye matatizo automatically. Lazima utengeneze accountability kwenye mfumo, sio viongozi kuzurula tu.
Wazo zuri lakini thubutu watanzania ni wezi kuanzia viongozi hadi wananchi.

Kibaya zaidi ni dunia ya utapeli
 
Kwahiyo unaamini kuzodolewa hadharani ndio suluhisho la usumbufu na dharau za watumishi? Alikuwepo Dar na alizodoa sana watumishi, nini kimebadilika? Leo hii ukiulizwa, Makonda kaacha alama gani hapa Dar, utataja ipi?
Unataka aache alama gan wkt mnakumbuka mabaya yake na kuyapuuza mazuri yake au unahisi alama inabakia yenyewe bila watu kukubali kufuata alichokiacha ?
 
Kuna wakati unawaza kama bunduki zingekuwa zinauzwa kiholela basi wengi wa watumishi wa umma wangesha kula chuma.
Pole pole tutafika tu huko. Maana kwa kweli usumbufu uliopo kwenye maofisi ya umma unatia kichefuchefu.
Nimeona clip ya mkandarasi mmoja analamikia kutolipwa pesa zake kwa shughuli za ujenzi alizofanya, mpaka jamaa amefirisika. Halmashauri wanapokea pesa toka serikalini, badala ya kumlipa yeye ili amalizie kazi, wao wanawapa watu wengine wanalizie kazi bila kujali wala kumlipa haki zake.
Hiyo clip iliniumiza sana. Utafika wakati watu watavitafuta vya moto huko drc, unakuja unawawasha wote waliokufirisi, then hata ukienda kunyongwa ni sawa tu.
 
Na wale waliopotezwa na kuuwawa na wengine kupigwa risasi na wanamtaja Makonda?!

Na yule aliemtolea Bastola Waziri fulani na kutaka kumuua?!
Kama mna ushahidi si bora mpeleke mahakamani sio kutuimbia mitandaoni
 
Kwahiyo unaamini kuzodolewa hadharani ndio suluhisho la usumbufu na dharau za watumishi? Alikuwepo Dar na alizodoa sana watumishi, nini kimebadilika? Leo hii ukiulizwa, Makonda kaacha alama gani hapa Dar, utataja ipi?
Kwa hiyo suluhisho la hili tatizo la watumishi kuwa usumbufu na dharau ni nini? Tupe majibu wewe si hutaki wasizodolewe tupe suluhisho mbadala
 
Ukweli ni kwamba yawezekana Makonda ana mapungufu yake kama mwanadamu mwingine yeyote. Lakini kwa kero za nyingi ya ofisini za uma hasa unapokuwa unahitaji huduma yenye viashiria vya maslahi, utazungushwa na kusumbuliwa kwa vitu vidogo sana, unapoteza muda, gharama ya fedha na gharama zingine nyingi.

Kusema kweli kuna wakati mjane mmoja alikuwa anafuatilia mirathi ya mme wake yaani amekamilisha kila kielelezo kinachotakiwa lakini ilimchukua miaka 3 kupata hiyo hela huku akienda maofisini kila wiki.

Kuna wakati unawaza kama bunduki zingekuwa zinauzwa kiholela basi wengi wa watumishi wa umma wangesha kula chuma.

Yawezekana approach ya Makonda sio nzuri kama ndivyo lakini naomba tunapomkosoa tuje na majawabu ya kuondoa hizi dharau za watumishi wa umma kwa watu ambao kimsingi ndio mabosi wao.
Yaani
 
Kusema kweli kuna wakati mjane mmoja alikuwa anafuatilia mirathi ya mme wake yaani amekamilisha kila kielelezo kinachotakiwa ladato cha nnkini ilimchukua miaka 3 kupata hiyo hela huku akienda maofisini kila wiki.

Kuna wakati unawaza kama bunduki zingekuwa zinauzwa kiholela basi wengi wa watumishi wa umma wangesha kula chuma.

Yawezekana approach ya Makonda sio nzuri kama ndivyo lakini naomba tunapomkosoa tuje na majawabu ya kuondoa hizi dharau za watumishi wa umma kwa watu ambao kimsingi ndio mabosi wao.
Kuna clip huyo jamaa yenu alikua Arumeru akiwabagaza watumishi juzi ndo utajua kua jamaa ni hamnazo na kweli alipata zero form four.Somola uraia kidato cha pili khs mamlaka za miji midogo ni sheria iliyotungwa na serikali chini ya wizara ya OR TAMISEMI,lkn yeye anawadhalilisha watumishi wkt sheria ipo inayotambua mamlaka hayo,sema nini,yeye ni public attention seeker km alivyokua JPM.Anayo nafasi ya kuishauri serikali ikaifuta sheria ile ila ukiiangalia clip ile yule mwanasheria wa halmashauri alikua very smart kumjibu yeye alikua anatafuta kiki mbele ya wananchi.Makonda kimsingi hafai kwenye uongozi wa umma alifaa zaidi kule kwenye propaganda kwasababu ana uelewa mdogo sana wa mambo
 
Ndo maana tunasemaga wazi hamna akili nyie wafuasi wa Mbowe, ndo nyie kila thread mnaleta story za Ben Saanane, Yani watu wawili au watatu wanaohisiwa kuhusishwa kupotea kwao na Makonda ndo kufanye mtu asione changamoto za mkoa mzima anazozitatua Makonda!?!?,umewahi kuzungushwa ofisi za serikalini??,umeelewa hata kilichoelezewa!?,siku ukizungushwa maofisini au ukadhurumiwa haki yako na mahakama ndo siku utaondoa kichwani hizo story za Ben Saa8.
Angekuwa mwanao usingesema watu wawili au watatu, ni lazima tujifunze kuheshimu utu wa mtu.
 
Ukweli ni kwamba yawezekana Makonda ana mapungufu yake kama mwanadamu mwingine yeyote. Lakini kwa kero za nyingi ya ofisini za uma hasa unapokuwa unahitaji huduma yenye viashiria vya maslahi, utazungushwa na kusumbuliwa kwa vitu vidogo sana, unapoteza muda, gharama ya fedha na gharama zingine nyingi.

Kusema kweli kuna wakati mjane mmoja alikuwa anafuatilia mirathi ya mme wake yaani amekamilisha kila kielelezo kinachotakiwa lakini ilimchukua miaka 3 kupata hiyo hela huku akienda maofisini kila wiki.

Kuna wakati unawaza kama bunduki zingekuwa zinauzwa kiholela basi wengi wa watumishi wa umma wangesha kula chuma.

Yawezekana approach ya Makonda sio nzuri kama ndivyo lakini naomba tunapomkosoa tuje na majawabu ya kuondoa hizi dharau za watumishi wa umma kwa watu ambao kimsingi ndio mabosi wao.
Mkuu naunga mkono hoja yako, ndio maana tunamuasa Makonda ajitahidi kuweka mfumo mzuri wa usimamizi wa kitaasisi ndani ya mkoa wake kwa kushirikisha taasisi na viongozi mwenzake kama timu moja kudhibiti changamoto zilizopo kuliko anavyojiendea mwenyewe kuzodoa na kudhalilisha kila mtumishi wa serikali.

Shida ya Makonda ana uwezo mdogo wa kufikiri, amekariri mbinu moja hiyo hiyo bila kupima uwezo wa watu, aina ya watu, upepo wa kisiasa, nyakati na mazingira yaliyopo.

Taratibu anaanza kuwa so irrelevant!
 
Ndo maana tunasemaga wazi hamna akili nyie wafuasi wa Mbowe, ndo nyie kila thread mnaleta story za Ben Saanane, Yani watu wawili au watatu wanaohisiwa kuhusishwa kupotea kwao na Makonda ndo kufanye mtu asione changamoto za mkoa mzima anazozitatua Makonda!?!?,umewahi kuzungushwa ofisi za serikalini??,umeelewa hata kilichoelezewa!?,siku ukizungushwa maofisini au ukadhurumiwa haki yako na mahakama ndo siku utaondoa kichwani hizo story za Ben Saa8.
Mkuu tuweke mambo ya siasa kando uhai wa mtu mmoja ni muhimu mno.

Udhalilishaji wa utu wa mtu sio jambo la kuchekea hata kama huyo mtu anawapa watu hela bure.

Afuate utaratibu wa sheria kushughulikia watendaji waovu.
 
Tuongelee current situation kama hizo allegations zina ushahidi apelekwe mahakamani ili haki itendeke japo hilo haliondoi kwamba watumishi wengi wa umma ni kero isiyovumilika
Mkuu naye Makonda, Kama anaona watumishi wenzake ni kero awapeleke mahakamani kuliko kupayuka na kudhalilisha watu hadharani. Sheria ni msumeno.
 
Mkuu achana na huyo chizi amejaza story za vijiweni za wanasiasa. Nilichogundua asilimia kubwa ya watanzania hawatumii ubongo wao kufikiri na kutatua jambo, wanafuata mkumbo tu.
✍️📝👌👍👏🤝🙏🛡️
 
Unataka aache alama gan wkt mnakumbuka mabaya yake na kuyapuuza mazuri yake au unahisi alama inabakia yenyewe bila watu kukubali kufuata alichokiacha ?
Wewe uliyeona mazuri tusaidie sisi tusiyaona. Tupe hizo alama ambazo ameacha
 
Inavyoonekana wewe ni mnufaika wa upuuzi wa watumishi wa umma unatumumia kipimo gani kwamba hakuna tatizo lilitatuliwa? Maana nina uhakika hata hapa jf hatuwezi kukosa mashuhuda wa mambo yaliyokuwa sugu lakini yalimalizwa na makonda.
🤣 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom