Kama huko inbox mambo ndio haya, wanaume turudi shule

Kama huko inbox mambo ndio haya, wanaume turudi shule

Wanaboa sana hawa watu, yaani cjui wakoje, sasa hv nimemblock mtu, jifunzeni kujieleza bhana, ukisema usimjibu unyamaze atakusalimia hata miaka 2 hachoki halafu kila siku
Mii ata salam sijui Agynasa tufanye mkutano leo mahala fulani pm kama hutojali.
 
Nilichoka ujuee,saa ingine unadhani sms ya MPESA kumbee unauliza uko poa,upo shwari,za weekend vipi ,upo wapi,unafnya nini khaaaaa
Basi mii sina bahati mana kijibiwa tu nauliza tigopesa
 
Nachukia sana neno "NIAMBIE " Au "nipe story, habari "
Mtu unitext mwenyew, sijaku bip bado unataka nikupe story Mimi nazitoa wapi, hizo habari wanazolazimishwa kupewa ni zipi?
Wenye hizi tabia mnaboa.
Sirudii tena [emoji5]
 
HII NI CHATING INBOX
Mkaka: hi!
Mdada: helow!
Mkaka: Mambo!?
Mdada: Poa.
Mkaka: Inakuwaje
Mdada: Fresh tu
Mkaka: Shwari kabisa?
Mdada: Shwari tu..
Mkaka: Mishe zinakwenda poa!
Mdada: Poa tu
Mkaka: Mambo mengine?
Mdada: Poa tu
Mkaka:ehe Nambie sasa...
Mdada: Poaz
Mkaka: hata mi nko poa vp michongo?
Mdada: Poa tu
Mkaka: Pande zipi mrembo....
Mdada: Nipo home
Mkaka: Pande zipi hizo mi nipo Mwanza
Mdada: Dar
Mkaka: kwema pande hizo
Mdada: kwema tu
Mkaka: Maisha yanasemaje?
Mdada: Poa tu
Mkaka: Familia iko poa Mdada: Poa tu
Mkaka: SAMAHANI HIVI UNAISHI NA
WAZAZI AMA UMEOLEWA? Na kama umeolewa je
unaionaje ndoa?
Mdada: kimya..
Baada ya dakika mbili mdada akamblock yule
mkaka......
**Wakati mwingine tunawalaumu bure akina dada
eti wanadharau huko Inbox. Sasa jamani kweli huyu
mtu huyu!! Unamsaidiaje hata kama ni wewe...Yaani
salamu imerudiwa weee mpaka kero halafu
mwishowe anauliza swali la ghafla tu ka mpu.mbavu
vile!!!
Tuheshimiane tafadhal....acha kutudhalilisha wanaume wenzio..[emoji23][emoji23]
 
Aniaquote ke yeyote tuoneshe mfano wa mtongozano hapa
Niko mwanza mimi[emoji39] [emoji39] [emoji39]
 
Bora huyo kakujibu ki staarabu kuliko wale wa kukujibu

P
K
 
Back
Top Bottom