Kama huna fikra za kikandamizaji, hauwezi kuishadadia Urusi

Kama huna fikra za kikandamizaji, hauwezi kuishadadia Urusi

Wapi umeona serikali ya Marekani inaeneza ushoga. Yaani Marekani inatoa mashoga New York na kuwaleta mbagala na Gongo la Mboto au inakuwaje??
Media zinapromote ushoga, we angalia muvi za kutoka marekani nyingi zina maudhui hayo
 
Kama huamini kwamba Kiongozi anatakiwa kuabudiwa, hauwezi kuishadadia Urusi. Kama wewe unaamini kila mtu ana haki ya kuelezea hisia zake bila ya kutishwa na dola, huwezi kuishabikia Urusi.

Kama unataka Kiongozi akiwa madarakani asitumie madaraka hayo kujitajirisha, wewe na Urusi hamfanani. Kama unapenda demokrasia duniani, kaa mbali na Urusi. Kama unachukia viongozi Katili, jitenge na Urusi.

Kama siyo tabia yako kupenda wanasiasa wanaopenda rushwa na wanaozuia kukamatwa, iache Urusi ikae mbali na wewe.
Unamaanisha Urusi ni pariah / rogue state..?
 
Kama huamini kwamba Kiongozi anatakiwa kuabudiwa, hauwezi kuishadadia Urusi. Kama wewe unaamini kila mtu ana haki ya kuelezea hisia zake bila ya kutishwa na dola, huwezi kuishabikia Urusi.

Kama unataka Kiongozi akiwa madarakani asitumie madaraka hayo kujitajirisha, wewe na Urusi hamfanani. Kama unapenda demokrasia duniani, kaa mbali na Urusi. Kama unachukia viongozi Katili, jitenge na Urusi.

Kama siyo tabia yako kupenda wanasiasa wanapenda rushwa na wanaozuia kukamatwa, iache Urusi ikae mbali na wewe.
unataka tuishadadie marekani hii iliyovamia Iraq na kuuwa maelfu ya watu,, iliyovamia Libya na kuua maelfu ya watu Afghanistan, Vietnam etc. Punguza mahaba ndugu,,, kila uchao kufungulia nyuzi za kuiponda urusi utadhani unalipwa vile!!!
 
Wewe ukisia wamarekani wameuawa utafurahi?? Hakuna mtu anayeshabikia nchi kwa kuwa inaua watu. Lakini mfumo wa kuendesha nchi kwa Urusi ni mbovu na wa kikatili sana.

Na wewe kila nyuzi ninayoandika kuhusu Urusi lazima uisome, Unalipwa??
 
Kuna mahali nimeuliza kwamba Sodoma na Gomora ushoga ulienezwa na Marekani?? Hoja hapa ni kwamba ili uikubali urusi ni lazima uwe na chembe chembe za kupenda kukandamiza wengine.
Labda nikukimbushe mwaka 2003 kama ulikuwa hujazaliwa, Marekani iliishutumu Iraq kuwa ina silaha za kikemikali, ikabidi watumwe wachunguzi wa kimataifa kwenda Iraq kukagua, na Iraq haikupinga.

Wakakagua hawakukuta hizo silaha wala residuals, wakatoa ripoti kuwa hakuna silaha hatarishi,

Marekani bila sababu yoyote akaivamia iraq, wakaua maelfu

Kuna wakari wanajeshi wa marekani waliua watoto kama wanacheza video games,

ICC ikataka kuwashitaki wakaijia juu kuwa wataiwekea vikwazo.

Urusi kaivamia ukraine kwa sababu ilikuwa ina mu host marekani na ni hatari kiusalama kwa urusi, NI KIPI KINA JUSTIFY UUAJI WA MAREKANI? AU KWA SABABU ALIUA WAARABU?

jitahidi ufuatilie maswala kiundani usipelekwe na mkumbo wa Western media
 
Iko hv wengi wanaomshabikia mrusi sio kwamba wanapenda anayoyafanya kwasasa,hata wao wanajua sio kitu poa,ila wanashabikia kwasababu tu mrusi kafanya kile ambacho marekani hatak watu wengine duniani wakifanye wakati mmarekani akitaka kufanya anafanya na hakuna wa kumzuia
 
jitahidi ufuatilie maswala kiundani usipelekwe na mkumbo wa Western media
Kwa umri wangu mambo mengine nikumbushe tu wala huna haja ya kutoa mhadhara. Vita ya Iraq haikustahili na kwa kweli wakati mwingine Marekani imekuwa na marais wapenda vita kama BUSH mdogo alivyokuwa. Lakini pia hiyo haihalalishi Urusi kuivamia Ukraine eti kwa kuwa tu Ukraine inataka kuwa mwanachama wa NATO.
 
Kumbe watu wengi Bado wako usingizi wa kifikra namna hii? Sasa naamini propaganda ina nguvu Sana, Sana Sanaa.
 
Mtz yeyeto anae ishabikia russia hajui kitu mbaya aliyotufanyia mrussi wakati iddi aminwa alipo tuvamia na kuzuka vita ya Kagera!
[emoji116][emoji116]
mrusi alimsaidia idi amini kwa kumuuzia ndege vita na kutupa masharti magumu tulipo muomba atuuzie heat seeking missiles ambazo zilituishia!
Kukosa Hekima ya nyerere Kuomba msaada wa Anti aircraft Missiles Msumbiji na Algeria na wao kutusaidia amini angeendelea kutamba mwanza!; na vita ingekuwa endelevu na mrusi ange-balance vita ili Iwe fursa ya kuuza silaha zake![emoji56][emoji15]
Au Tatizo inawezekana bado hujui uchungu na athari za kuvamiwa hata na vibaka[emoji12]
Au Afya ya Akili ni mgogoro...
 
We mleta mada uelewa wako uko chini sana. Unahitaji elimu ya ana kwa ana sio jf.
Tafuta mtu mtaan akusaidie kidogo geopolitics. Akusaidie tafsiri ya uhuru wa nchi kimipaka na kijeshi. Akusaidie kuhusu super power countries na 3rd world countries.
Muhim jua Tanzania na marekan zote ni nchi lakin si sawa
 
Watu hawajui kuwa jinsi wanavyoizungumzia neno ushoga ndipo inability kushamiri? Kitu kinapingwa kwa matendo siyo maneno...make mnavyozidi kuliongelea ndiyo graph inaonesha kuwa inapanda.

Andamaneni mshinikize serikali na bunge watunge sheria kali sana kuanzia sasa kama njia ya kupinga siyo propaganda.
 
Labda nikukimbushe mwaka 2003 kama ulikuwa hujazaliwa, Marekani iliishutumu Iraq kuwa ina silaha za kikemikali, ikabidi watumwe wachunguzi wa kimataifa kwenda Iraq kukagua, na Iraq haikupinga.

Wakakagua hawakukuta hizo silaha wala residuals, wakatoa ripoti kuwa hakuna silaha hatarishi,

Marekani bila sababu yoyote akaivamia iraq, wakaua maelfu

Kuna wakari wanajeshi wa marekani waliua watoto kama wanacheza video games,

ICC ikataka kuwashitaki wakaijia juu kuwa wataiwekea vikwazo.

Urusi kaivamia ukraine kwa sababu ilikuwa ina mu host marekani na ni hatari kiusalama kwa urusi, NI KIPI KINA JUSTIFY UUAJI WA MAREKANI? AU KWA SABABU ALIUA WAARABU?

jitahidi ufuatilie maswala kiundani usipelekwe na mkumbo wa Western media
Huwezi kupinga uvamizi wa US Iraq ila ukaunga mkono uvamizi wa Urusi kwa Ukraine. Matukio yote ni ya uonevu. Hivyo ukimwona mtu aliyebeba kinyongo cha Iraq na huku akifurahia kinachoendelea Ukraine, either ni udini unamsumbua au hana anachosimamia.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Huwa nawashangaa sana watu wanaojidai kupigania demokrasia na katiba mpya kwenye nchi hii huku wanamshadadia Putin!
Sijawahi kuelewa wanai reconcile vipi hiyo contradiction.
 
Back
Top Bottom