Kama hutojali, tupe siri yako ya kupata usingizi haraka usaidie wenye tatizo hili

Kama hutojali, tupe siri yako ya kupata usingizi haraka usaidie wenye tatizo hili

Takribani wiki sasa changamoto hii inanitesa, naingia kitandani saa tatu usiku Mpaka saa Tisa an sehemu nahangaika kutafuta usingizi.....Leo nikaona niende site, tangu asubuhi napiga kazi, metoka huko nimechoka balaa Kama ng'ombe wa plau. Nimeingia ndani saa 2 usiku, Nikajua Leo nalala sana, saa 3 nikaingia zangu kulala, cha kushangaza Mpaka Muda huu naandika hapa hakuna hata dalili ya lepe la usingizi. Hata sijui nifanye nini.
 
1. Zingatia nyakati regular za kula, kulala, kupumzika, mazoezi na shughuli zingine ili kuboresha ur mental, physical & digestive health.

It may be you have some serious disruption of your circadian rhythm (biological clock). Huu mfumo wa asili ndio unaamua muda gani na kiwango gani mwili urelease sleep hormones na kulegeza mwili ili usinzie.

2. Manage kama unayo stress or depression, too much blood sugar ama diabetes, obesity, disorders zingine zinazohusiana na moyo ama mfumo wa mishipa ya damu, BP, use of alcohol, caffeine, smoking, high fat food stuff. Pumzika, fanya mazoezi, use a lot of water badala ya vinywaji baridi, try fresh fruits and take some quality time for relaxation and innocent socialization.
 
Anayesimulia mvua ujue imemnyeshea, yawezekana kwa wengine ikawa ni mshangao wanaposikia kuna watu hawapati usingizi kirahisi, lakini hili tatizo linawasumbua watu kiukweli. Mtu anaweza kuingia kitandania saa nne usiku ila usingizi ukampata saa sita usiku.

Binafsi njia nayotumiaga ni kusikiliza kinanda laini kwa kutumia ear phones, kile kinanda laini hakika kwangi hakijawai kuniangusha
Wakati wa mlo wa usiku unywe na maziwa fresh yaani usingizi wa ghafla utakuja na utalala fofofo usiku mzima.
 
Hivi mnakosaje usingizi? Wenzenu tunajikuta tumeamkia sebuleni asubuhi sababu ya usingizi usio na adabu
 
Hahahaaa naamini hili fumbo linahitaji mtu alifumbue, wachache sana watakuwa wamekuelewa.

Akishika tu biblia shetani atampa usingizi haraka sana.
Nishawahi jaribu hiyo njia ila ikagonga mwamba,shetani sio boya kama tunavyofikiri

nilishika bible nikiwa bed nikaanza kusoma Ufunuo wa Yohana,nikaanza Mlango wa 1

nikaja mlango wa 2,mara kushtuka nipo mlango wa 11 sina hata tone la usingizi,ngoma inasonga tu

nikaona hapana usintanie,nikafunga bible nikatafuta njia ingine ya kusaka usingizi,kesho yake nikiwa kazini

nikashka bible hata sijaifungua vizuri tayari nishaanza kusinzia,hapo ndio nikajua kaka shetani sio wa kisport sport.
 
Kuna msemo kwamba "Mafundi seremala ndio wanaoongoza kwa kupata usingizi mzuri." Jiulize kwa nini? Usingizi ni sehemu ya burudani kwa mwanadamu. Burudani yoyote ile inahitaji maandalizi ili mwili uifurahie.

1. Hakikisha mwili umelishwa vizuri na kuchoshwa kwa kazi halali ya kipato
2. Hakikisha akili imelishwa chakula chake bora na cha kiafya
3. Hakikisha moyo wako umesafishwa na hauna mzigo wa husda, chuki, wivu, na negatives kama hizo

Hapo dakika 5 tu ushasinzia sana tu, wanaweza kukuhamisha hadi Kongo bila kujua
Oanisha hizo dondoo zako tatu na ufundi seremala.
 
Anayesimulia mvua ujue imemnyeshea, yawezekana kwa wengine ikawa ni mshangao wanaposikia kuna watu hawapati usingizi kirahisi, lakini hili tatizo linawasumbua watu kiukweli. Mtu anaweza kuingia kitandania saa nne usiku ila usingizi ukampata saa sita usiku.

Binafsi njia nayotumiaga ni kusikiliza kinanda laini kwa kutumia ear phones, kile kinanda laini hakika kwangi hakijawai kuniangusha
Nakatakata kachumbari ya vitunguu maji pekee. Natafuna. Nasuuza mdomo. Nakwenda kulala. Nalala Fofofo kabisa.
 
Oanisha hizo dondoo zako tatu na ufundi seremala.
Pointi ya ufundiseremala ni poetic kwa maana kwamba kazi yoyote halali, ya kipato huleta contentment na enjoyment --- unakuwa na uhakika wa kipato, mwili umefanya mazoezi, akili imeshughulishwa, hakuna muda wa kubumunda umbeya na kulea mafundo & vinyongo kumtima. Pointi ya ufundiseremala vilevile inavuta hisia za Fundiseremala Mnazareti.
 
Kipindi nasoma Kunguni Mbu na joto, vilinifanya niende kitandani kwa lengo moja tu, kusinzia.

Naenda nikiwa nimechoka, Nikifika tuu Nazima.

Tofauti na hilo Mimi ni mmoja wapo wa wanaoutafuta usingizi kwa tochi,

Nina jamaa yangu ni kiboko,
Yaani akiona tu kitanda anaanza kukoroma.
Akina mm nikilala kuamka aaa nne
 
Back
Top Bottom