Hili ni kutoka moyoni kabisa!
Nchi ya watu wa jamhuri ya JPM, haifumbii macho upandaji wa mazao kiholela na kuishi kwa tozo zisizo na kichwa wala mkia, Haina uhusiano kabisa na rushwa, wazembe kule hawatakiwi, mafisadi hawaweki pua zao kule, kule ni HAPA KAZI TU Na kuishi kwa kumtegemea MUNGU
Kule miradi haihujumiwi kijinga! Kule ni Taifa la watu wenye nguvu na wanaojiamini! Hakuna kuoneana, masikini ataishi kwa haki yake na tajiri kwa haki yake, kila mtu atakula kwa jasho lake na si kwa urefu wa kamba zake!
Na kama iko namna bora na ambapo viongozi wetu wanapaswa kutumia hekima ili kuondoa mpasuko unaoendelea mitandaoni na ambapo viongozi wetu huwenda wanaona ni kawaida, basi wanapaswa kuliangalia hili na kuwa nalo makini sana, kwani linazidi kuipasua nchi na kuleta tofauti mkubwa kwa wananchi na mpaka kwa viongozi wenyewe!
Kuilinda Amani kwa majeshi na vitisho, ni njia nzuri ila sio namna bora yenye kuleta utengamano kwa jamii iyoumizwa; watanyanaza kwa midomo yao lakini mioyo yao ingali inawaka moto!
Tukubali ama tusikubali, nyuma ya hayati JPM kuna mamilioni ya watanzania ambao mpaka sasa wamekuwa wafuasi wa mlengo wake na wameendelea kuumizwa na matusi na kejeli nyingi kumhusu JPM, Ikumbukwe, JPM alikuwa Raisi wa nchi hii, hivyo, ameacha watu wengi nyuma waliathiriwa na namna ya uongozi wake na wakampenda kama kiongozi wa aina yake kwenye mioyo yao
Si kwenye majeshi yetu, si kwa viongozi wa ndani na nje ya nchi tu, bali hata viongozi wengi waliko ndani ya ccm na ndani ya vyama vingi vya upinzani
Kuendelea kuacha jina lake kutukanwa kama mdori! Hii sio heshima wala mila zetu watanzania
Ifike pahala, jambo hili likomeshwe ili kuwaleta watanzania kwa pamoja na umoja wao!
Kama kuna mtu anajidanganya kusema eti hao sukuma gang, kwanza ni wachache na itafika mahali watasahau, huku ni kujidanganya na kuendelea kuchochea ghadhabu ndani ya mioyo ya wengi! Mtu aliyewatoa tongotongo watanzania na kuona kwamba kumbe hata Tanzania na watanzania kuinuka kiuchumi inaezeakana, iwe rahisi tu kusahaulika?
Hii ni nchi yetu sote, tumekuwa na utaratibu usiopendelea mtu wala dini na ama kabila ili kumfanya
Mtu awe kiongozi wetu!
JPM alishinda kwa haki na nyinyi ccm ndio mliotuletea, na ushindi wake mliusimamia nyinyi wenyewe, kwa nini hata chama chake kimeacha kumtunzia heshima yake kama mtu aliyeitumikia hii nchi tena kwa mafanikio makubwa?
Mnamaanisha kwamba nyinyi ccm ndio mnaoratibu haya unayoendelea kumhusu JPM?
Nahitimisha kusema, ccm majijengea uhasama na wananchi nyinyi kwa nyinyi!
Amani yetu, Maendeleo yetu!
Najisikia raha kuzaliwa Tanzania, nitakuenzi Tanzania na nitakupigania kwa nguvu zangu zote, nitakulinda, Mafisadi watasalenda tu!