Hili ni kutoka moyoni kabisa!
Na kama iko namna bora na ambapo viongozi wetu wanapaswa kutumia hekima ili kuondoa mpasuko unaoendelea mitandaoni na ambapo viongozi wetu huwenda wanaona ni kawaida, basi wanapaswa kuliangalia hili na kuwa nalo makini sana, kwani linazidi kuipasua nchi na kuleta tofauti mkubwa kwa wananchi na mpaka kwa viongozi wenyewe!
Kuilinda Amani kwa majeshi na vitisho, ni njia nzuri ila sio namna bora yenye kuleta utengamano kwa jamii iyoumizwa; watanyanaza kwa midomo yao lakini mioyo yao ingali inawaka moto!
Tukubali ama tusikubali, nyuma ya hayati JPM kuna mamilioni ya watanzania ambao mpaka sasa wamekuwa wafuasi wa mlengo wake na wameendelea kuumizwa na matusi na kejeli nyingi kumhusu JPM, Ikumbukwe, JPM alikuwa Raisi wa nchi hii, hivyo, ameacha watu wengi nyuma waliathiriwa na namna ya uongozi wake na wakampenda kama kiongozi wa aina yake kwenye mioyo yao
Si kwenye majeshi yetu, si kwa viongozi wa ndani na nje ya nchi tu, bali hata viongozi wengi waliko ndani ya ccm na ndani ya vyama vingi vya upinzani
Kuendelea kuacha jina lake kutukanwa kama mdori! Hii sio heshima wala mila zetu watanzania
Ifike pahala, jambo hili likomeshwe ili kuwaleta watanzania kwa pamoja na umoja wao!
Kama kuna mtu anajidanganya kusema eti hao sukuma gang, kwanza ni wachache na itafika mahali watasahau, huku ni kujidanganya na kuendelea kuchochea ghadhabu ndani ya mioyo ya wengi! Mtu aliyewatoa tongotongo watanzania na kuona kwamba kumbe hata Tanzania na watanzania kuinuka kiuchumi inaezeakana, iwe rahisi tu kusahaulika?
Hii ni nchi yetu sote, tumekuwa na utaratibu usiopendelea mtu wala dini na ama kabila ili kumfanya
Mtu awe kiongozi wetu!
JPM alishinda kwa haki na nyinyi ccm ndio mliotuletea, na ushindi wake mliusimamia nyinyi wenyewe, kwa nini hata chama chake kimeacha kumtunzia heshima yake kama mtu aliyeitumikia hii nchi tena kwa mafanikio makubwa?
Mnamaanisha kwamba nyinyi ccm ndio mnaoratibu haya unayoendelea kumhusu JPM?
Nahitimisha kusema, ccm majijengea uhasama na wananchi nyinyi kwa nyinyi!