Kama ilipo Israel siyo Israel, Wayahudi wanaotajwa kwenye Quran na Biblia walikuwa wanaishi wapi?

Swali langu linakuja hawa watu japo waliondoka hawakuondoka wote walikuwepo jews asilia hawakutoka mzee usije kuchanganya Madesa. Waliishi na waarabu pamoja na wote waliitwa raia wa mamlaka ya palestina. So hao wakuja wakaanza kununua ardhi mdogo mdogo na waliuziwa na waarabu so waarabu kuja kustuka ni kama wanalingana idadi. Kila jamii ikawa na wanamgambo wake na mwisho wa siku jews walitaka wawe na taifa lao na pamoja na waarabu. Waarabu wakakataa ndio tupo hapo mpaka leo
 
Israel ni israel tu iwe ya sasa ama ya zamani.
Unaposema ya sasa inamana kulikuwa na yazamani
Pale walishakuwepo miaka na miaka
Na wao wanatambuana mno.
Na pale ndipo eneo lao
Io kaanani ilikuwepo miaka na miaka,mlima sayuni ulikuwepo tangu musa,hekalu lao lilikuwepo tangu zamani.
Na kwaimani yao wao wanaamini Mungu hawasikii maombi yao mpaka wawe kwenye ardhi waliyoahidiwa baraka.

Myahudi amechukuliwa utumwani mara 4 na amerudi kwao,na mara zote akirudi anakuta watu wameshapachukua.izo vita ni zamiaka na miaka
 
Nataka kujua Kwa wajuzi wa historia za ulimwengu na maandiko ya kidini watupe mwanga.
usisumbuke sana mkuu, anzia hapa!

1. misri ya kale (ya farao) walikua ni weusi, this is a fact, wanahistoria wengi (karibia wote) wanakubaliana na hii fact!

2. Ibrahimu mara nyingi alishuka misri pindi kanani kulipokuwa na changamoto (hasa ukame)- a biblical fact

3. Yusufu (mtoto wa Yakobo/Israel) aliuzwa utumwani Misri,- a biblical fact (hapa pana swali, je Yusufu alikua wa rangi gani?)

4. Nduguze Yusufu waliposhuka misri kununua chakula nyakati zile za Ukame, hawakumtambua NDUGU YAO YUSUFU- this is a biblical fact, wao walimwona kama wafanyakazi wengine wa Farao (kwahiyo, hapa inatupa picha kwamba yumkini Yusufu alikua na rangi sawa na wamisri wengine waliokuwa watumishi wa Farao, kinyume chake nduguze wangeshangaa kumkuta mtumishi wa Farao mwenye cheo kikubwa then hafanani na wa Misri wengine)

5. Yakobo/Israel alihamia Misri nyakati za Ukame (yeye na uzao wake) -a biblical fact

6. Musa alilelewa nyumbani mwa Farao baada ya 'kuokotwa' na binti Farao - a biblical fact,

7. Yusufu, baba yake Yesu, alikimbilia Misri kujificha dhidi ya Herode- a biblical fact ....(inawezekana mtu asie mweusi akaenda kujificha kwa weusi na asitambulikane na majasusi wa herode?)

zipo facts nyingi ila naishia hapa kwa muktadha wa uzi wako!


******************

sasa, swali ni hili,

kwa fact hizo nilizoandika hapo juu, Yakobo alikua mtu wa rangi gani? alifanana na watu gani?

Je, hawa wanaoitwa wa-Israeli wa leo ni watu wa rangi gani,? wanafanana na watu gani?

NB/.
ukiondoa fact ya utumwa (chini ya warumi), hakukua na engagement ya aina yoyote iliyorekodiwa na Biblia kati ya wa-Israel na watu wa Ulaya, ISIPOKUWA kulikua na mwingiliano wa kihistoria kati ya wa-Israeli (toka Ibrahimu hadi mitume) na wa Misri na wa 'Ethiopia'

*neno 'Ethiopians' wagiriki walilitumia kuwakilisha watu waliokuwa kusini mwa Misri (sudan mpk east africa- by then hakukua na rekodi zozote kuhusu watu wa kusini za east africa!)

mengine jiongeze mwenyewe na ujitoe kwenye gereza la kifikra!
 
Quran haikatai kuwa Wayahudi kwao ni nchini Israel

Ila kinachopingwa na wapenda haki na sio waislam tu hata Nyerere pia alikuwa anapinga kwanini Wapalestine wabaguliwe wakati na wao pia ni kwao?

Kwa sababu Yahudi ni jina la kabila Moja katika makabila 12 ya watoto wa Yakobo hivyo basi hayo makabila yote pale ni kwao

Lakini pia Yakobo sio mtoto pekee wa Isaka pia yupo Esau na Esau pia Ile aridhi ni yake na Esau ndio ameza wapalestine

Mwisho kabisa hawa akina Netanyau sio waisrael original wale ni wamarekani na waingereza wamewekwa pale Ili kulinda wizi na ujanbazi wa Marekani na Uingereza katika rasilimali za mashariki ya kati
 
Kama niko sawa nimeielewa hoja yako hivi.

Kina Benjamini pale siyo kwao maana ni wazungu. Umetumia kigezo gani kujua kama Benjamin Netanyahu siyo Waisraeli?

Kumbe wapalestina wanatokana na uzao wa Essau, hilo nilikuwa sijui.

Rasirimali gani zilizopo hapo Mashariki ya kati zinazoibiwa na Uingereza na Marekani?
 
Mbinguni.
 
Mkuu ni kama historia umeianzia kati kati kuisimulia.

Wayahudi kuongozwa na Mussa kutoka utumwani kurudi Kanani, siyo kwamba walikuwa wanaenda nchi ya ahadi ambayo ni ngeni kwao, hapana.

Kabla ya kwenda Misri ambako mzee Yakobo alihamishia makazi yake kumfuata mwanaye Yusufu aliyeuzwa utumwani na ndugu zake huko ,kisha akawa boss kwa cheo mwenye mamlaka ya mema ya nchi.

Baadaye kwa chuki walifanywa watumwa na baadaye Mussa akaoteshwa ndoto za kuwarejesha kwenye nchi yao ya zamani.

Ukitaka kuunga historia sawa sawa kuwasimulia Wayahudi, lazima uanze na Abrahamu na mkewe Sara, wapi walitokea na walifikaje hapo.
 
Kwa ivo ni Biblia tu ndiyo fasihi Andishi?

Dini nyingine vitabu vyake navyo vikoje? Pia ni fasihi Andishi?
Kila dini mkuu ni kazi za ubuni.

Ni watu tu walikua wakirekodi matukio ya watu maarufu na kuongezea chumvi.

Kama hadithi za alfu lela ulela.

Ungekua mfatiliaji wa falsafa tofauti na dini ungegundua binadamu anauwezo wa kufikiri vitu vyenye hekima sana.

Hebu pitia falsafa tofauti tofauti, baadhi zina mafundisho bora kuliko dini na ni matokeo ya akili za watu tu, dini je?
 
Napenda fasihi.

Kwa ivo kulikuwa na matukio halisi halafu yakatiwa chumvi🙄

Kwa muktadha wa hoja hii kipi kilichotiwa chumvi. Waisraeli kuwa na asili ya Mashariki ya kati au nini?
 
Napenda fasihi.

Kwa ivo kulikuwa na matukio halisi halafu yakatiwa chumvi🙄

Kwa muktadha wa hoja hii kipi kilichotuwa chumvi. Waisraeli kuwa na asili ya Mashariki ya kati au nini?
Yaah mkuu!

Mfano boti ya nuhu inasemekana ni kubwa haijawahi tokea na haiji tokea ila kiuhalisia ni Chai "Uongo" sababu ziko meli kubwa duniani kuizidi safina ya Nuhu na bado haziwezi kuchukua kila sampuli ya kiumbe kimoja duniani.


Pia kuchukua viumbe vyote sio jambo la kufikuri juu juu, ilitakiwa kila kiumbe Nuhu akitengenezee mazingira ya kusurvive;

Unaona hii mkuu, ni logic sio BLAH! BLAH! 👇

Huo ni mfano mdogo ku proove kwamba hizo ni fictious, Kwanza safina Ya nuhu ilikua ndogo kuliko hii Sea giant ya sasa ila iliweza kuchukua viumbe vyote, kama sio chumvi ni nini?

Huu ni mfano mmoja wa mia kuprove kwamba hizo ni kazi za Fasihi andishi tu.
 
Yaah mkuu!
Huu ni mfano mmoja wa mia kuprove kwamba hizo ni kazi za Fasihi andishi.
Nakubaliana na hoja yako. Lakini ni kwa nini watu wengi wakitaka kusema vitabu vya dini vina hadithi za kutungwa, mfano hutolewa kwa Biblia?

Ni Kwa nini Biblia ndiyo inayoongoza kwa kufanyiwa rejea ya hoja hii ya vitabu vya dini vya uongo?
 
Nakubaliana na hoja yako. Lakini ni kwa nini watu wengi wakitaka kusema vitabu vya dini vina hadithi za kutungwa, mfano hutolewa kwa Biblia.

Ni Kwa nini Biblia ndiyo inayoongoza kwa kufanyiwa rejea ya hoja hii ya vitabu vya dini vya uongo?
Kwasababu Christian ndiyo dini maarufu, Hata hivyo hukuniambia nitumie reference ipi, Hivyo nakua huru kutumia mifano ninayoitaka.
 
Kwasababu Christian ndiyo dini maarufu, Hata hivyo hukuniambia nitumie reference ipi, Hivyo nakua huru kutumia mifano ninayoitaka.
Yes.

Kimantiki kinachochaguliwa kwanza ndicho kinachofaa kuliko vingine vilivyopo.

Ukristo ni maarufu kuliko ubudha na Uislamu? Maana sioni watu wakinukuu Sana maandiko ya waislamu na kusema kuwa Quran ni hadithi za kutungwa.
 
Yes.

Kimantiki kinachochaguliwa kwanza ndicho kinachofaa kuliko vingine vilivyopo.

Ukristo ni maarufu kuliko ubudha na Uislamu? Maana sioni watu wakinukuu Sana maandiko ya waislamu na kusema kuwa Quran ni hadithi za kutungwa.
Yaah!

Na Kuchaguliwa hakumaanishi ubora, kwani wakati mwingine kinachochaguliwa kinaweza kuwa dhaifu zaidi kuliko vyote vilivyopo.
 
Yaah!

Na Kuchaguliwa hakumaanishi ubora, kwani wakati mwingine kinachochaguliwa kinaweza kuwa dhaifu zaidi kuliko vyote vilivyopo.
Nimesema kimantiki Kwa muktadha wa hoja yako. Kama umesema ukristo ndiyo dini maarufu duniani. Bila shaka kitabu chake hunukuliwa zaidi kutokana na ubora na udhaifu wake.

Ndiyo maana nauliza vitabu vingine kama Quran siyo hadithi za kutungwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…