Kama ilipo Israel siyo Israel, Wayahudi wanaotajwa kwenye Quran na Biblia walikuwa wanaishi wapi?

Kama ilipo Israel siyo Israel, Wayahudi wanaotajwa kwenye Quran na Biblia walikuwa wanaishi wapi?

Achana na vitabu vya dini, na izo blabla nyingine zisokua na maana.mi swali langu lipo hapa.sie Leo tunasema tupo kwenye nchi yetu ya Tanzania au sio, lakini ukijaribu kusoma historian ya watu wanaojiita wao ni raia wa Tanzania Ivi sasa,hakuna jamii au mtu anayeweza kusubutu kusema yeye kizazi chake kiliishi hapa Tanzania tangu zaidi ya miaka elfu2 iliyopita. Inamana kwa kwa mnavyomaanisha,ni kwamba sisi hapa Tanzania sio kwetu. Sasa hao walioshi hapa miaka elfu2 iliyopita ambao ndio kwao,siku wakijitokeza na kudai ardhi Yao ili waunde taifa lao lipya na sisi tufanye ndio tupo chin Yao kwa Kila kitu,tuwe tunwasikiliza wao kwa Kila jambo wewe kama wewe utawaelewa? Achlia mbali jamii nzima ya Tanzania ya leo.ebu nijibu ,au munachukulia wepesi wepesi tu kwa vile Aya mambo yapo kwa wenzenu?
Swali langu linakuja hawa watu japo waliondoka hawakuondoka wote walikuwepo jews asilia hawakutoka mzee usije kuchanganya Madesa. Waliishi na waarabu pamoja na wote waliitwa raia wa mamlaka ya palestina. So hao wakuja wakaanza kununua ardhi mdogo mdogo na waliuziwa na waarabu so waarabu kuja kustuka ni kama wanalingana idadi. Kila jamii ikawa na wanamgambo wake na mwisho wa siku jews walitaka wawe na taifa lao na pamoja na waarabu. Waarabu wakakataa ndio tupo hapo mpaka leo
 
Hujajibu swali ndugu yangu.

Tukubaliane kwamba Taifa la Israel ya Sasa, Lilianzishwa mwaka 1948. Kabla ya hapo hakukuwa na Taifa la Israel ya Sasa.

Sasa kabla ya mwaka 1948, Waisraeli wanaotajwa kwenye Biblia na Quran walikuwa wanaishi wapi?

Isije kuwa Waisraeli wa zama hizo za Biblia na Quran ni wamakonde wa Leo!?
Israel ni israel tu iwe ya sasa ama ya zamani.
Unaposema ya sasa inamana kulikuwa na yazamani
Pale walishakuwepo miaka na miaka
Na wao wanatambuana mno.
Na pale ndipo eneo lao
Io kaanani ilikuwepo miaka na miaka,mlima sayuni ulikuwepo tangu musa,hekalu lao lilikuwepo tangu zamani.
Na kwaimani yao wao wanaamini Mungu hawasikii maombi yao mpaka wawe kwenye ardhi waliyoahidiwa baraka.

Myahudi amechukuliwa utumwani mara 4 na amerudi kwao,na mara zote akirudi anakuta watu wameshapachukua.izo vita ni zamiaka na miaka
 
Nataka kujua Kwa wajuzi wa historia za ulimwengu na maandiko ya kidini watupe mwanga.
usisumbuke sana mkuu, anzia hapa!

1. misri ya kale (ya farao) walikua ni weusi, this is a fact, wanahistoria wengi (karibia wote) wanakubaliana na hii fact!

2. Ibrahimu mara nyingi alishuka misri pindi kanani kulipokuwa na changamoto (hasa ukame)- a biblical fact

3. Yusufu (mtoto wa Yakobo/Israel) aliuzwa utumwani Misri,- a biblical fact (hapa pana swali, je Yusufu alikua wa rangi gani?)

4. Nduguze Yusufu waliposhuka misri kununua chakula nyakati zile za Ukame, hawakumtambua NDUGU YAO YUSUFU- this is a biblical fact, wao walimwona kama wafanyakazi wengine wa Farao (kwahiyo, hapa inatupa picha kwamba yumkini Yusufu alikua na rangi sawa na wamisri wengine waliokuwa watumishi wa Farao, kinyume chake nduguze wangeshangaa kumkuta mtumishi wa Farao mwenye cheo kikubwa then hafanani na wa Misri wengine)

5. Yakobo/Israel alihamia Misri nyakati za Ukame (yeye na uzao wake) -a biblical fact

6. Musa alilelewa nyumbani mwa Farao baada ya 'kuokotwa' na binti Farao - a biblical fact,

7. Yusufu, baba yake Yesu, alikimbilia Misri kujificha dhidi ya Herode- a biblical fact ....(inawezekana mtu asie mweusi akaenda kujificha kwa weusi na asitambulikane na majasusi wa herode?)

zipo facts nyingi ila naishia hapa kwa muktadha wa uzi wako!


******************

sasa, swali ni hili,

kwa fact hizo nilizoandika hapo juu, Yakobo alikua mtu wa rangi gani? alifanana na watu gani?

Je, hawa wanaoitwa wa-Israeli wa leo ni watu wa rangi gani,? wanafanana na watu gani?

NB/.
ukiondoa fact ya utumwa (chini ya warumi), hakukua na engagement ya aina yoyote iliyorekodiwa na Biblia kati ya wa-Israel na watu wa Ulaya, ISIPOKUWA kulikua na mwingiliano wa kihistoria kati ya wa-Israeli (toka Ibrahimu hadi mitume) na wa Misri na wa 'Ethiopia'

*neno 'Ethiopians' wagiriki walilitumia kuwakilisha watu waliokuwa kusini mwa Misri (sudan mpk east africa- by then hakukua na rekodi zozote kuhusu watu wa kusini za east africa!)

mengine jiongeze mwenyewe na ujitoe kwenye gereza la kifikra!
 
Kuna hoja ipo kuwa pale ilipo Israel kwa Sasa si Ardhi ya waisrael bali wapalestina.

Binafsi nakubaliana na hoja hiyo. Lakini swali la kujiuliza ni kwamba, kama ilipo Israel kwa Sasa siyo nchi ya waisrael, jee pale Mashariki ya kati, waisrael wanastahili kuwepo kwenye nchi Gani?

Quran na Biblia zina hadithi kuhusu wayahudi. Hao wayahudi wanaotajwa kwenye Quran na Biblia, zama hizo walikuwa wanaishi kwenye nchi gani ambayo kwa sasa haipo?
Quran haikatai kuwa Wayahudi kwao ni nchini Israel

Ila kinachopingwa na wapenda haki na sio waislam tu hata Nyerere pia alikuwa anapinga kwanini Wapalestine wabaguliwe wakati na wao pia ni kwao?

Kwa sababu Yahudi ni jina la kabila Moja katika makabila 12 ya watoto wa Yakobo hivyo basi hayo makabila yote pale ni kwao

Lakini pia Yakobo sio mtoto pekee wa Isaka pia yupo Esau na Esau pia Ile aridhi ni yake na Esau ndio ameza wapalestine

Mwisho kabisa hawa akina Netanyau sio waisrael original wale ni wamarekani na waingereza wamewekwa pale Ili kulinda wizi na ujanbazi wa Marekani na Uingereza katika rasilimali za mashariki ya kati
 
Quran haikatai kuwa Wayahudi kwao ni nchini Israel

Ila kinachopingwa na wapenda haki na sio waislam tu hata Nyerere pia alikuwa anapinga kwanini Wapalestine wabaguliwe wakati na wao pia ni kwao?

Kwa sababu Yahudi ni jina la kabila Moja katika makabila 12 ya watoto wa Yakobo hivyo basi hayo makabila yote pale ni kwao

Lakini pia Yakobo sio mtoto pekee wa Isaka pia yupo Esau na Esau pia Ile aridhi ni yake na Esau ndio ameza wapalestine

Mwisho kabisa hawa akina Netanyau sio waisrael original wale ni wamarekani na waingereza wamewekwa pale Ili kulinda wizi na ujanbazi wa Marekani na Uingereza katika rasilimali za mashariki ya kati
Kama niko sawa nimeielewa hoja yako hivi.

Kina Benjamini pale siyo kwao maana ni wazungu. Umetumia kigezo gani kujua kama Benjamin Netanyahu siyo Waisraeli?

Kumbe wapalestina wanatokana na uzao wa Essau, hilo nilikuwa sijui.

Rasirimali gani zilizopo hapo Mashariki ya kati zinazoibiwa na Uingereza na Marekani?
 
Kuna hoja ipo kuwa pale ilipo Israel kwa Sasa si Ardhi ya waisrael bali wapalestina.

Binafsi nakubaliana na hoja hiyo. Lakini swali la kujiuliza ni kwamba, kama ilipo Israel kwa Sasa siyo nchi ya waisrael, jee pale Mashariki ya kati, waisrael wanastahili kuwepo kwenye nchi Gani?

Quran na Biblia zina hadithi kuhusu wayahudi. Hao wayahudi wanaotajwa kwenye Quran na Biblia, zama hizo walikuwa wanaishi kwenye nchi gani ambayo kwa sasa haipo?
Mbinguni.
 
Swali unalojiuliza linahusu moja ya masuala yenye historia ndefu na yanayozungumziwa sana katika dini, historia, na siasa. Linagusa juu ya hadithi za kihistoria, kidini, na madai ya kisiasa kuhusu ardhi ya Israeli ya kisasa na uhalali wa Waisrael kuishi huko.

1. Hadithi za Waisrael Katika Biblia na Quran

  • Biblia: Katika Biblia, inasimuliwa kwamba Waisrael (ambao walikuwa wazawa wa Yakobo, mwana wa Isaka na mjukuu wa Ibrahimu) walipewa ardhi ya Kanaani na Mungu kama urithi wao wa milele. Hii ndio eneo ambalo linahusishwa na Israeli ya kisasa na Palestina ya sasa. Waisrael waliishi hapo kabla ya kufukuzwa na watawala wa kigeni kama Wababeli na Warumi. Hadithi ya kupewa ardhi hiyo inapatikana zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Kutoka, ambapo Mungu anawaongoza Waisrael kutoka Misri kwenda kwenye "Nchi ya Ahadi" (Kanaani).
  • Quran: Quran inataja Wana wa Israeli (Bani Israel) kama taifa lililochaguliwa na Mwenyezi Mungu. Wanatajwa kupewa ardhi takatifu baada ya kukombolewa kutoka utumwa wa Firauni huko Misri. Quran inasema katika Surat Al-Ma'ida (5:21) kwamba Mungu aliwaagiza Wana wa Israeli waingie kwenye ardhi takatifu (Al-Ard al-Muqaddasah), ambayo ni sawa na Kanaani. Hata hivyo, kuna mazungumzo zaidi kuhusu dhambi na kupoteza neema ya Mungu, ambayo yanawafanya kuhama na kuwa katika hali ya kutawanyika (diaspora).

2. Nchi ya Waisrael Katika Historia

Kihistoria, Waisrael waliishi kwenye eneo linalojulikana kama Kanaani, ambalo liko kati ya Bahari ya Mediteranea na Mto Yordani. Eneo hili linajumuisha sehemu za Israeli ya kisasa, Palestina (Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi), Lebanoni, na sehemu za Jordan na Syria.

  • Israeli ya Kale: Kulikuwa na milki za kale za Israeli ambazo zilitawaliwa na Wafalme kama Daudi na Sulemani. Baada ya muda, milki hizo zilipoteza nguvu na Waisrael walitekwa na tawala za Wababeli na baadaye Warumi, ambao walisababisha kufukuzwa kwao kwenye ardhi yao. Kuanzia hapo, Waisrael walienea kote ulimwenguni, hali inayojulikana kama "diaspora."
  • Sasa hivi: Eneo la Mashariki ya Kati limekuwa na historia ngumu ya mizozo ya ardhi, na Waisrael waliporudi kwenye ardhi hiyo katika karne ya 19 na 20, ilikuwa ni matokeo ya harakati za kisiasa za Zionism zilizoanzishwa kwa lengo la kuunda taifa la Kiyahudi. Hii ilisababisha migongano ya madai ya ardhi kati ya Wayahudi na Wapalestina, ambao walikuwa wakiishi kwenye eneo hilo kwa muda mrefu.

3. Madai ya Waisrael na Wapalestina kwa Ardhi

  • Wapalestina: Wapalestina wanadai kwamba walikuwa wameishi katika eneo hilo kwa karne nyingi kabla ya kuja kwa Wazayuni. Wanahoji kuwa Israeli ilitwaliwa kutoka kwao na mkoloni wa kigeni kwa msaada wa Uingereza baada ya Vita ya Pili ya Dunia, na wanataka haki yao ya kurejea kwenye ardhi hiyo.
  • Waisrael: Kwa upande mwingine, Waisrael wanadai kwamba hiyo ni ardhi yao ya kihistoria na ya kidini, wakisema kwamba walinyang'anywa ardhi yao na watawala wa kigeni lakini wamekuwa na uhusiano wa kihistoria na kidini nayo kwa maelfu ya miaka.

4. Wapi Waisrael Wanastahili Kuishi?

Swali lako linahusisha mchanganyiko wa historia, dini, na siasa. Kulingana na Biblia na Quran, Waisrael walitoka kwenye eneo la Mashariki ya Kati, hususan kwenye ardhi ya Kanaani, ambayo kwa sasa ni Israeli na Palestina. Hivyo, hadithi za kidini zinaashiria kwamba hiyo ni ardhi yao ya kihistoria.

Hata hivyo, kwa mtazamo wa kisasa wa kisiasa, suala hili limekuwa na migongano mikubwa kutokana na historia ya uhamiaji, ukoloni, na madai ya pande zote mbili juu ya ardhi hiyo. Waisrael wa kisasa na Wapalestina wote wanadai haki ya kuishi kwenye ardhi hiyo, jambo ambalo limesababisha mzozo unaoendelea hadi leo.

Hitimisho​

Kwa kifupi, Wayahudi walikuwa wanaishi kwenye ardhi ya Kanaani (eneo la Israeli ya sasa na Palestina) katika zama za kihistoria. Hata hivyo, mzozo wa kisasa juu ya ardhi hiyo umeleta mgongano wa madai kutoka pande zote mbili. Wayahudi wa Biblia na Quran wanatajwa kupewa ardhi hiyo, lakini migongano ya kisiasa na historia imesababisha hali ngumu ya kiutata kuhusu nani hasa anastahili kumiliki na kuishi huko.
Mkuu ni kama historia umeianzia kati kati kuisimulia.

Wayahudi kuongozwa na Mussa kutoka utumwani kurudi Kanani, siyo kwamba walikuwa wanaenda nchi ya ahadi ambayo ni ngeni kwao, hapana.

Kabla ya kwenda Misri ambako mzee Yakobo alihamishia makazi yake kumfuata mwanaye Yusufu aliyeuzwa utumwani na ndugu zake huko ,kisha akawa boss kwa cheo mwenye mamlaka ya mema ya nchi.

Baadaye kwa chuki walifanywa watumwa na baadaye Mussa akaoteshwa ndoto za kuwarejesha kwenye nchi yao ya zamani.

Ukitaka kuunga historia sawa sawa kuwasimulia Wayahudi, lazima uanze na Abrahamu na mkewe Sara, wapi walitokea na walifikaje hapo.
 
Zipi hizo? Maana humu kumeandikwa mengi!
Kitabu kizima ni Fasihi andishi, Work of fiction.
Screenshot_20241227-164517.png
 
Kwa ivo ni Biblia tu ndiyo fasihi Andishi?

Dini nyingine vitabu vyake navyo vikoje? Pia ni fasihi Andishi?
Kila dini mkuu ni kazi za ubuni.

Ni watu tu walikua wakirekodi matukio ya watu maarufu na kuongezea chumvi.

Kama hadithi za alfu lela ulela.

Ungekua mfatiliaji wa falsafa tofauti na dini ungegundua binadamu anauwezo wa kufikiri vitu vyenye hekima sana.

Hebu pitia falsafa tofauti tofauti, baadhi zina mafundisho bora kuliko dini na ni matokeo ya akili za watu tu, dini je?
 
Kila dini mkuu ni kazi za ubuni.

Ni watu tu walikua wakirekodi matukio ya watu maarufu na kuongezea chumvi.

Kama hadithi za alfu lela ulela.

Ungekua mfatiliaji wa falsafa tofauti na dini ungegundua binadamu anauwezo wa kufikiri vitu vyenye hekima sana.

Hebu pitia falsafa tofauti tofauti, baadhi zina mafundisho bora kuliko dini na ni matokeo ya akili za watu tu, dini je?
Napenda fasihi.

Kwa ivo kulikuwa na matukio halisi halafu yakatiwa chumvi🙄

Kwa muktadha wa hoja hii kipi kilichotiwa chumvi. Waisraeli kuwa na asili ya Mashariki ya kati au nini?
 
Napenda fasihi.

Kwa ivo kulikuwa na matukio halisi halafu yakatiwa chumvi🙄

Kwa muktadha wa hoja hii kipi kilichotuwa chumvi. Waisraeli kuwa na asili ya Mashariki ya kati au nini?
Yaah mkuu!

Mfano boti ya nuhu inasemekana ni kubwa haijawahi tokea na haiji tokea ila kiuhalisia ni Chai "Uongo" sababu ziko meli kubwa duniani kuizidi safina ya Nuhu na bado haziwezi kuchukua kila sampuli ya kiumbe kimoja duniani.

Screenshot_20241228-125139~2.png

Pia kuchukua viumbe vyote sio jambo la kufikuri juu juu, ilitakiwa kila kiumbe Nuhu akitengenezee mazingira ya kusurvive;
Screenshot_20241228-125423~2.png

Unaona hii mkuu, ni logic sio BLAH! BLAH! 👇
Screenshot_20241228-125347~2.png

Huo ni mfano mdogo ku proove kwamba hizo ni fictious, Kwanza safina Ya nuhu ilikua ndogo kuliko hii Sea giant ya sasa ila iliweza kuchukua viumbe vyote, kama sio chumvi ni nini?

Huu ni mfano mmoja wa mia kuprove kwamba hizo ni kazi za Fasihi andishi tu.
 
Yaah mkuu!
Huu ni mfano mmoja wa mia kuprove kwamba hizo ni kazi za Fasihi andishi.
Nakubaliana na hoja yako. Lakini ni kwa nini watu wengi wakitaka kusema vitabu vya dini vina hadithi za kutungwa, mfano hutolewa kwa Biblia?

Ni Kwa nini Biblia ndiyo inayoongoza kwa kufanyiwa rejea ya hoja hii ya vitabu vya dini vya uongo?
 
Nakubaliana na hoja yako. Lakini ni kwa nini watu wengi wakitaka kusema vitabu vya dini vina hadithi za kutungwa, mfano hutolewa kwa Biblia.

Ni Kwa nini Biblia ndiyo inayoongoza kwa kufanyiwa rejea ya hoja hii ya vitabu vya dini vya uongo?
Kwasababu Christian ndiyo dini maarufu, Hata hivyo hukuniambia nitumie reference ipi, Hivyo nakua huru kutumia mifano ninayoitaka.
 
Kwasababu Christian ndiyo dini maarufu, Hata hivyo hukuniambia nitumie reference ipi, Hivyo nakua huru kutumia mifano ninayoitaka.
Yes.

Kimantiki kinachochaguliwa kwanza ndicho kinachofaa kuliko vingine vilivyopo.

Ukristo ni maarufu kuliko ubudha na Uislamu? Maana sioni watu wakinukuu Sana maandiko ya waislamu na kusema kuwa Quran ni hadithi za kutungwa.
 
Yes.

Kimantiki kinachochaguliwa kwanza ndicho kinachofaa kuliko vingine vilivyopo.

Ukristo ni maarufu kuliko ubudha na Uislamu? Maana sioni watu wakinukuu Sana maandiko ya waislamu na kusema kuwa Quran ni hadithi za kutungwa.
Yaah!

Na Kuchaguliwa hakumaanishi ubora, kwani wakati mwingine kinachochaguliwa kinaweza kuwa dhaifu zaidi kuliko vyote vilivyopo.
 
Yaah!

Na Kuchaguliwa hakumaanishi ubora, kwani wakati mwingine kinachochaguliwa kinaweza kuwa dhaifu zaidi kuliko vyote vilivyopo.
Nimesema kimantiki Kwa muktadha wa hoja yako. Kama umesema ukristo ndiyo dini maarufu duniani. Bila shaka kitabu chake hunukuliwa zaidi kutokana na ubora na udhaifu wake.

Ndiyo maana nauliza vitabu vingine kama Quran siyo hadithi za kutungwa?
 
Back
Top Bottom