Kama ilipo Israel siyo Israel, Wayahudi wanaotajwa kwenye Quran na Biblia walikuwa wanaishi wapi?

Kama ilipo Israel siyo Israel, Wayahudi wanaotajwa kwenye Quran na Biblia walikuwa wanaishi wapi?

Huo siyo muktadha wa hoja yako,hoja yako ni uspesho wa israel, hakuna hicho kitu,spesho wamewekwa utumwani miaka!!
Waliambiwa ukikosea kitakutokea hiki na hiki. Ni kama vile wewe ukiambiwa uache uzinz ila ukikaid kuna adhabu
 
Hao wanaotajwa hapo ni watu siyo nchi.

Kafanye homework yako.
Aisee, Yani hayo majina Israeli, Hebroni, Yerusalemu yote ni watu sio maeneo? Yani mtu ni mfalme; ana governing body, ana jeshi, ana watu anaowaongoza(makabila 12), kuna sheria, ana maeneo yote anayoongoza yana mipaka inayoeleweka halafu unasema sio nchi?

Na umetoa wapi maandiko yanayosema Daudi au Suleiman walitokea Misri au waliongoza Misri?
 
Hilo ni kweli kabisa, ilikuwa Tanganyika, na kabla ya Tanganyika ilikuwa ni Zanzibar.
Yaani Tanganyika ilikuwa sehemu ya Zanzibar Au unamaanisha Zanzibar ilihusisha baadhi ya maeneo ya Tanganyika mpaka Mombasa (himaya ya Sultan)?
 
Yaani Tanganyika ilikuwa sehemu ya Zanzibar Au unamaanisha Zanzibar ilihusisha baadhi ya maeneo ya Tanganyika mpaka Mombasa (himaya ya Sultan)?
Kabla ya kuwa Tanganyika ilikuwa ni Zanzibar. Mkutano wa Betrlin ndiyo ukaikatakata Afrika kama keki, wakagawana wazungu.

Ilikuwa mpaka Somalia na chini huko mpaka Maputo (Sofala).
 
Kuambiwa kuacha uzinzi siyo ahadi,elewa
Nimekutolea mfano kuwa waliambiwa ukifanya hiki utaadhibiwa usipofanya unabarikiwa. Ni kama vile vitabu vitakatifu vinasema ukitenda dhambi utaangamia ukiishi maisha ya utii kwa Mungu utabarikiwa. Mbona Rahisi kueleweka mzee
 
Ukiambiwa ukimbie kilomita saba kwenda na kurudi utapewa milioni,ukashindwa kukimbia ukaishia njiani,bado utadai milioni?
Mungu sio binadamu mzee na hizo ahad alitoa kwa babu na baba zao so kulikuwa na option kwenye biblia inasema huko walikofukuziwa wakitubu watasikilizwa na watarudishwa nyumban kwao. Na tena anasema japo watachukuliwa mateka atawaacha wachache japo wanyonge.
 
Wacha story nipe dalili wapi Israel ipo kwenye Bibilia kama ni Taifa, nipe reference usilete story za bar hapa.
2 SAMWELI 7:20 – 23

20
Na mimi, Daudi, nikuambie nini tena zaidi? Iwapo wewe umemjua mtumwa wako, Ee Bwana MUNGU.

21 Kwa ajili ya neno lako, na kwa moyo wako mwenyewe, umetenda makuu hayo yote, ili umjulishe mtumwa wako.

22 Kwa hiyo, wewe ndiwe mkuu, Ee Bwana Mungu, kwa maana hakuna kama wewe, wala hapana Mungu mwingine ila wewe, kwa kadiri tulivyosikia kwa masikio yetu.

23 Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako, kama Israeli, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa kwa ajili yake, wawe watu wake mwenyewe, akajifanyie jina, na kutenda mambo makuu kwa ajili yenu, na mambo ya kuogofya kwa ajili ya nchi yako, mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri wawe wako, kutoka katika mataifa na miungu yao.
 
Sasa kama wanajua kuongea kiebrania huoni kama huo ni uthibitisho kuwa ndio wayahudi halisi.Je kuna mpalestina yeyote anaweza kuongea kiingereza cha kuzaliwa,si mpaka akae darasani ajifunze.Ila kama wanaweza kuongea kiebrania kwa kuzaliwa hao ni wayahudi hata kama ni wazungu.Allah sio mjinga amuumbe mzungu halafu ampe Lugha ya kiebrania.
Wayahudi ni kabila miongoni mwa watu waliokuwa wanaishi palestina ila siyo hawa wazungu wazungu waliotoka ulaya kisa wanajua kuongea kiebrania.
 
Sasa kama wanajua kuongea kiebrania huoni kama huo ni uthibitisho kuwa ndio wayahudi halisi.Je kuna mpalestina yeyote anaweza kuongea kiingereza cha kuzaliwa,si mpaka akae darasani ajifunze.Ila kama wanaweza kuongea kiebrania kwa kuzaliwa hao ni wayahudi hata kama sio wazungu.Allah sio mjinga amuumbe mzungu halafu ampe Lugha ya kiebrania.
Wayahudi ni kabila miongoni mwa watu waliokuwa wanaishi palestina ila siyo hawa wazungu wazungu waliotoka ulaya kisa wanajua kuongea kiebrania.
 
Sasa kama wanajua kuongea kiebrania huoni kama huo ni uthibitisho kuwa ndio wayahudi halisi.Je kuna mpalestina yeyote anaweza kuongea kiingereza cha kuzaliwa,si mpaka akae darasani ajifunze.Ila kama wanaweza kuongea kiebrania kwa kuzaliwa hao ni wayahudi hata kama ni wazungu.Allah sio mjinga amuumbe mzungu halafu ampe Lugha ya kiebrania.
Wapo wapalestina wanaoongea kiebrania kuzidi hao wazungu hapo Israel
 
Wayahudi walikuwepo hapo hapo mashariki ya kati ila Sasa je hao wayahudi wa kale walikuwa na asili ya Ulaya magharibi/ mashariki (wazungu) kama hawa wa sasa?

zitto junior
Wayahudi wamezungukwa pande zote na waarabu, wao wamekuwaje wazungu. Utapeli huu
 
Kuna hoja ipo kuwa pale ilipo Israel kwa Sasa si Ardhi ya waisrael bali wapalestina.

Binafsi nakubaliana na hoja hiyo. Lakini swali la kujiuliza ni kwamba, kama ilipo Israel kwa Sasa siyo nchi ya waisrael, jee pale Mashariki ya kati, waisrael wanastahili kuwepo kwenye nchi Gani?

Quran na Biblia zina hadithi kuhusu wayahudi. Hao wayahudi wanaotajwa kwenye Quran na Biblia, zama hizo walikuwa wanaishi kwenye nchi gani ambayo kwa sasa haipo?
Kwao ni maeneo yote wanayoishi sasa pamoja na maeneo ya Westbank, Gollan heights waliyoikalia kimabavu, maeneo ya kusini mwa Lebanon, Gaza na maeneo ya Sinai Misri ukigoogle utaona.

Kusema walipo si kwao ni maneno ya kisiasa tu.

Ukisoma 'the history of Israel' katika wikipedia ama google utaona mtawala wa mwisho katika ufalme wa Israel alikuwa ni nani na baadaye kufuatia tawala za mataifa mbalimbali yakiwemo Assirians, Romans, Shirazzi, Egypty hadi Ottoman empare nk nk.

Katika tawala zote hizo ziliwakandamiza sana, kuwahamisha kwa nguvu katika maeneo yao pamoja na kuchukuliwa mateka na wengine kutawanyika katika mataifa mbali mbali ya Ulaya, Marekani, Asia, Africa na kwingineko duniani.

Uyahudi ni kabila, dini na utamaduni vilivyofungamana, hivyo popote walipoenda walitambulika hivyo.
Kwa utambulisho huo, ndiyomaana walivyopata uhuru wengi wao waliamua kurudi kwao.

Historia ni ndefu kidogo ni vizuri ukatafuta vyanzo ukasoma mwenyewe utaelewa vizuri zaidi.
 
Mungu hakuwahi kuwapotezea wengine wote na kujali kundi fulani
Kama wewe ni Mkristo rudi kasome Bible upya.

Vitu kama Torati ilikuwa lwa ajili yao tu sio wote. Sadaka za dhambi, hekalu n.k vilikuwa kwa ajili yao tu wengine Hatukuhesabiwa ndio maana kulikuwa na "Taifa la Mungu" na "Watu wa Mataifa"
 
Back
Top Bottom