Kama ilishindwa EU ndiyo BRICS itaweza kupambana na Marekani?

Kama ilishindwa EU ndiyo BRICS itaweza kupambana na Marekani?

Mkuu kwa hiyo wewe unadhani USA atakuwa kiranja wa Dunia miaka yote,au husomi historia kulikuwa na dola zenye nguvu huko nyuma nazo zilianguka.
Yes,BRICS wataweza sababu kuu ni Moja Nchi za BRICS zinaongoza kwa Rasilimali na soko kubwa LA bidhaa na huduma tofauti na EU ambayo haina rasilimali.

Moja ya malengo makubwa ya BRICS ni kuondoa mfumo kandamizi wa kiuchumi na unyonyaji wa hiyo USA,na moja kati wa washirika wa BRICS-Russia amefanikisha katika uondoaji wa matumizi ya USD katika mfumo wake wa kiuchumi.

Hali iliyopelekea Nchi nyingi kuiga kufanya trade katika currency zao.Najua unafahamu matokeo yake matumizi ya USD duniani yamepungua zaidi ya 10% kuliko hapo awali.
Bado hizo embargo zimepelekea Chumi za USA na Nchi za Ulaya kuyumba mara dufu.

Kama uliuliza kwa lengo LA kujifunza utakuwa umepata hints,kama ulikuwa ni ushabiki njoo na hoja.
Hizi data mnatoa wapi mbona matumizi ya Dollar yako palepale, 88% ya miamala yote ya kibiashara duniani imefanyika Kwa Dola. Mwenzetu data za kupungua kwa 10% umezitoa wapi?!!!!

Sent from my Mi 9T using JamiiForums mobile app
 
Mfano huu hausadifu tunachokiongelea.

Hebu nigeuze swali. BRICS ilikuwaje ikaanzishwa na ni kwa nini Marekani haimo kwenye BRICS??
Kwani si ushajibiwa BRICS Ni mbadala wa G7 au unajibu lako moyoni unalazimisha ujibiwe unavyotaka wewe?. BRICS ni opposite ya G7 sio EU ila tofauti kidogo BRICS mtaji wao mkubwa rasilimali watu ili baadaye watakapokuja kufanya biashara ndani ya soko la BRICS tu kuna watu wakutosha wakuwauzia bidhaa ila G7wao wamejichagua mabwenyenye tu wenye pesa ila hawana rasilimali watu wa kutosha wanategemea kuzalisha kuwauzia hao waliowatenga wanaowaona masikini na wanawategea mpaka kwa malighafi ya hivyo viwanda vyao.NB G7 ni nchi zinazoongoza kwa viwanda duniani ikiwemo na Marekani ipo kwenye G7 halafu unataka tena Marekani iwepo kwenye BRICS hivi unaanzaga kufikiri kabla ya kuandika kweli au ndio kati ya wale wasomi wetu wa degree moja ya kukariri history?
 
Kuna watu ni waja kwenye medani hii ya kimataifa, ngoja tuwakumbushe kidogo.

Nchi za ulaya ziliungana ziwe na mfumo mmoja wa kiuchumi Ili kushindana na Marekani.

Leo BRICS wanaungana Kwa lengo hilo hilo. Swali ni je fupa lililowashinda wajuvi wa Ulaya wasauzi wataliweza?
Wanajichekesha
Ni njozi za mchana
US $ itabakia mtawala
 
Hapa Brics sio suala la kupambana wala ugomvi bali ni kuwekeza pamoja na kupandisha uchumi wao
Kwa mfano Brazil akija kuwekeza kwenye kilimo kwenye nchi kadhaa Africa ni vizuri na hakuna madhara wala kushindana na 🇺🇸 hayo ni mawazo tu EU pia wana NATO pamoja na huyo huyo
Sisi waafrika huwezi kuona mtanzania anaenda nchi kama Nigeria au Egypt kutafuta bidhaa zao na kuleta hata nguo ila ataenda China na Dubai why?

Hatusaidiani kabisa waafrika acha tuone hao waliokubaliwa kujiunga
 
The United States is the most popular country for immigration, with over 50 million immigrants in 2020.

The United Nations ranked the United States as the top destination for immigrants, followed by Germany and Saudi Arabia.
Umechelewa sana hivi sasa kila mmarekani lengo lake ni kufika Dubai
 
Kuna watu ni waja kwenye medani hii ya kimataifa, ngoja tuwakumbushe kidogo.

Nchi za ulaya ziliungana ziwe na mfumo mmoja wa kiuchumi Ili kushindana na Marekani.

Leo BRICS wanaungana Kwa lengo hilo hilo. Swali ni je fupa lililowashinda wajuvi wa Ulaya wasauzi wataliweza?
Kitendo chs kutotumia Dollar huo ni ushindi tosha. Na biashara tayari zinaendelea bila Dollar. Wewe unataka tuendelee na mfumo wa Dunia nzima kununua kwa Dollar.
Wakina Biden wakiamka asubuhi wanazuia wenzao wasitumie Dollar , wasitumie Banks na mifumo yao, kupora pesa za watu kisa hawakubaliani.
Rejea Zimbabwe alichofanywa na mifumo ya west kisa kuwafukuza makabaila.
Kiufupi hata AFRICA tubuni mfumo wetu wa fedha .
Bidhaa zetu yuwauzie wazungu kwa fedha zao ila wao watuuzie kwa Dolla. Huu ujinga mpaka lini?
BIDEN anaweweseka chumbani kwake, huenda katafuta na bwana wa kumkuna kuna makalio.
TABIA ZA KITUMWA BADO ZIPO VICHWANI MWETU SISI WAAFRICA.
 
Usiifananishe EU na BRICS, EU ni kichaka cha Marekani. Unaweza nipa sababu zenye mashiko Kwann UK alijitoa???
UK ilijitoa sababu EU kuna free mouvement of people,sasa wapoland wengi walihamia UK. Uk haikutaka wahamiaji.
 
Kitu ambacho nimegundua ni kuwa hapa jamiiforums nje ya ushabiki watu wengi wana uelewa mdogo sana juu ya masuala ya siasa za kimataifa na uchumi wa Dunia.....wengi wanaochangia wanasukumwa na chuki na mihemko ya kishabiki juu ya masuala ya kimataifa.......

Kwa namna uchumi wa dunia ulivyo kwa sasa na nchi ya Marekani ni dhahiri kuwa mataifa au taifa lolote Duniani itawachukua miaka zaidi ya mia kuweza kuja kwenye ushindani na Marekani....au mataifa ya magharibi....

Kwa kifupi uchumi wa Marekani una ofa vitu vingi kwa Dunia kuliko nchi yoyote Ile Duniani..... Marekani Bado itakuwa economic hub ya dunia kwa zaidi ya miaka mingi mbele.......

Leo hii muwekezaji yeyote mwenye pesa akifika Marekani anakutana na wigo mpana wa kiuwekezaji na usalama wa fedha zake kuliko nchi zingine.........

Siasa za na system nzima ya maisha na uendeshaji wa kibiashara unawavutia wawekezaji na nguvukazi nyingi Duniani.....leo ni kila ndoto ya watu kutoka mataifa mbali mbali kuishi Marekani achilia mbali kuwa raia wa Marekani.......

Soko la hisa la Marekani Bado linashikilia mitaji ya makampuni makubwa Duniani na linazidi kukua.......

Uchumi wa Marekani umebuniwa au kutengenezwa kwa namna ambayo mataifa mengi huvutika kufanya biashara na Marekani.......

Inawezekana anguko la Marekani linakaribia Kwa kuwa hakuna Dola linalodumu milele lakini si kama inavyoainishwa na baadhi ya wadau hapa jamvini........
 
Twendeni polepole jamani hoja hazipigwi mkuki.
Screenshot_20230827_081753_X.jpg
 
Mkuu kwa hiyo wewe unadhani USA atakuwa kiranja wa Dunia miaka yote,au husomi historia kulikuwa na dola zenye nguvu huko nyuma nazo zilianguka.
Yes,BRICS wataweza sababu kuu ni Moja Nchi za BRICS zinaongoza kwa Rasilimali na soko kubwa LA bidhaa na huduma tofauti na EU ambayo haina rasilimali.

Moja ya malengo makubwa ya BRICS ni kuondoa mfumo kandamizi wa kiuchumi na unyonyaji wa hiyo USA,na moja kati wa washirika wa BRICS-Russia amefanikisha katika uondoaji wa matumizi ya USD katika mfumo wake wa kiuchumi.

Hali iliyopelekea Nchi nyingi kuiga kufanya trade katika currency zao.Najua unafahamu matokeo yake matumizi ya USD duniani yamepungua zaidi ya 10% kuliko hapo awali.
Bado hizo embargo zimepelekea Chumi za USA na Nchi za Ulaya kuyumba mara dufu.

Kama uliuliza kwa lengo LA kujifunza utakuwa umepata hints,kama ulikuwa ni ushabiki njoo na hoja.
Hiyo BRICKS Payment System inaanza lini? Ili tuanze kuona faida. Mtaalam kutoka South Africa aliulizwa swali hilo, akasema mfumo wa fedha uchukua miaka 20 hadi 30 kukaa sawa, maana yake Pesa ya Bricks itachukua muda huo. Ni vema wakaanza mapema, atujui dunia itakuaje 2040 au 2050.
 
Kinacho Fanya US kuwa na uchumi mkubwa ni global $ dominance. Sasa kitendo BRICS kuja na mkakati wa kutotumia $ kutaifanya dola ikose nguvu, linapokuja suala la global dominance reserve curence; jambo litakalopelekea influence ya marekani kupungua duniani kwani, uwezo wake wa kutumia economic power utakuwa umepungua.
Rudi shule ukasome tena
 
Watu wanakaa wanawaza namna ya kuwapambania watu wao kiuchumi..kupitia huo umoja..wewe unawaza kushindana na Marekani..
Waafrika akili zetu tunazijua wenyewe
Unadhani BRICS kuna mtu wanamtetea au wanatetea Uongozi wa milele kwenye nchi zao?

Asilimia 90 ya nchi za BRICS hazina uchaguzi huru
 
Back
Top Bottom