Kama ilivyoanzishwa kampeni ya kujenga Shule za kata sasa tuanzishe kampeni ya kupanga miji na maeneo yetu!

Kama ilivyoanzishwa kampeni ya kujenga Shule za kata sasa tuanzishe kampeni ya kupanga miji na maeneo yetu!

Kinachonisikitisha ni maeneo mapya ya ujenzi kuendelea kujengwa kihilela miaka hii. Tuanzie hapa tulipo kwa maeneo mapya yote yajengwe kisasa. Tukitaka kufanikiwa tuwe na mipango alafu wajinga wachache wasiojali ni kuvunja tu nyumba kadhaa kama JPM alivyofanya hapo kimara mbezi tuone kama watu hawatabadilika
 
Idadi ya hospitali, zahanati, vituo vta afya imeongezeka miaka y karibu. Hili ni jambo jema ama baya kwa wapanga na watunga sera?
 
1. Tanzania ya viwanda
2. Nchi kujitegemea
3. Miundombinu ya kuunganisha nchi
4. Umeme nafuu ila usaidie uzalishaji mpaka kwa mtanzania wa hali ya chini
5. Na mengine mengi
Viwanda vilianza kujengwa kipindi cha magufuli? Vingapi?

Nchi ilijitegemea kwenye nini?

Miundombinu gani alijenga kuzidi wenzake?

Umeme nafuu alianzisha yeye?
 
Kinachonisikitisha ni maeneo mapya ya ujenzi kuendelea kujengwa kihilela miaka hii. Tuanzie hapa tulipo kwa maeneo mapya yote yajengwe kisasa. Tukitaka kufanikiwa tuwe na mipango alafu wajinga wachache wasiojali ni kuvunja tu nyumba kadhaa kama JPM alivyofanya hapo kimara mbezi tuone kama watu hawatabadilika
Umesema Kweli kabisa
 
Veta KILA kata ndio mkombozi wa tatizo la ajira nchini
 
Sie tuliojenga Mbweni hili halituhusu. Pambaneni kivyenu.
 
Naungana na mtoa hoja. Hili Jambo nilikwisha liongelea siku moja humu jukwaani. Pitia hiyo link hapo juu.
 
Naungana na mtoa hoja. Hili Jambo nilikwisha liongelea siku moja humu jukwaani. Pitia hiyo link hapo juu.
Asante sana ndugu! Watu wengi sana tumeliongelea sana hili jambo humu! Ni wakati sasa kwa serikali kulifanyia kazi kwa kulipa kipaumbele maalum!
 
Nilichojifunza hapa Tanzania, ukidhamiria kufanya jambo fulani, ukalipa jitihada za kutosha na fedha , lazima jambo hilo lifanikiwe.

Kwenye moja ya sehemu ambayo kwa macho yangu nimeshuhudia hilo ni ujenzi wa madarasa zaidi ya 12,000 tena kwa viwango vizuri sana uliofanyika kipindi hiki cha Awamu ya Sita. Ndani ya miezi 3 tu, taifa limeshuhudia operesheni yenye mafanikio zaidi ya asilimia 95 ya ujenzi wa madaraka kwa ajiri ya watoto wetu kwenye viwango vya juu kabisa vya ubora!

Moja ya maeneo ambayo kwa Awamu zote 5 za nyuma Taifa hili tumekwama ni suala la kupima na kupanga miji na maeneo yetu

Jambo hili limekuwa likifanya Taifa letu kuonekana la hovyo kutokana na watu kujilimia na kujenga hovyo kila kukicha!

Leo hii ukitoka Manyara kwenda Arusha maeneo ya Tarangire unashuhudia ujenzi holela wa nyumba hadi kwenye eneo ambalo ndo yalikuwa mapito ya wanyama. Kilimo pia kinafanyika kwa kasi kwenye maeneo haya.

Leo hii ukienda Mwanza, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro, Songwe, Tanga, Dar es Salaam, Morogoro na mikoa mingi unaona Jinsi watu wanavyozidi kujenga kila siku bila mpangilio, Wengine wanajenga hadi maeneo ya hifadhi jambo litakaloleta hatari kubwa sana huko mbeleni maana kwa Jinsi watu wanavyozidi kuongezeka Tanzania, itafika wakati Taifa zima litakuwa squatters

Naomba serikali ya Awamu ya 6 ijiondoe kwenye dhambi hii! Watanzania wa sasa wana uwezo wa kujenga nyumba Nzuri tena sana na hili limeonekana hadi maeneo ya Dodoma yaliyopangwa na kupimwa vizuri. Kinachotakiwa kufanyika kuanzia sasa ni Serikali kuweka nguvu kubwa sana kwenye kupima na kuyapanga, maeneo yote na miji yote ya nchi hii na Kuhakikisha kila sehemu inaendelezwa na kulimwa kimpangilio.

Hakuna gharama kwenye kupima na kupanga miji yetu na Tanzania nzuri Kama Dubai , Texas, New York inawezekana

Naomba kuwasilisha!
Nilishatoa wazu siku nyingi kwamba Serikali ianzishe wakala wa kujitegemea kwa ajili ya kuratibu matumizi ya ardhi na mipango miji na wawe na pesa zao ndio tutapata suluhisho.
 
Nilishatoa wazu siku nyingi kwamba Serikali ianzishe wakala wa kujitegemea kwa ajili ya kuratibu matumizi ya ardhi na mipango miji na wawe na pesa zao ndio tutapata suluhisho.
Kweli kabisa! Nimejaribu kufuatilia humu if watu wengi sana wameandika sana kuhusu serikali kujikita rasmi kwenye suala la mipango miji. Ni wakati sasa serikali kufanyia kazi Masuala haya

Kuna hii nyingine niliikuta!
 
Humu jukwaani hakuna viongozi wa serikali au?
 
Huu ni ujinga mwingine,kwamba kwa sasa mafundi ni wachache na wanatusua Sana sio?
Vijana ni masikini sababu hawana ujuzi,lengo la veta ni kuwapa ujuzi kupitia ujuzi wataziona fursa.Shida sio tatizo la ajira shida ni uelewa Mdogo kuhusu fursa zinazokuzunguka.Tafsiri ya neno
Umasikini ni ukosefu wa mbinu ya kuchukua pesa toka kwa watu. Watu wanazo pesa unazichukuaje sasa Ili zije kwako, hio ndio inaitwa skills, wape bidhaa, wape huduma, wape connection, nk wao watakupa pesa umasikini kwako utatoweka kupitia ujasiliamali.
Unakuwa masikini sababu umekosa mbinu za kuchukua pesa toka kwa watu,
 
Nipo hapa Arusha kwa kweli hali ya mpangilio wa mji ni ovyo sana, naomba swrikali itizame suala la mpangilio wa mji.
 
Vijana ni masikini sababu hawana ujuzi,lengo la veta ni kuwapa ujuzi kupitia ujuzi wataziona fursa.Shida sio tatizo la ajira shida ni uelewa Mdogo kuhusu fursa zinazokuzunguka.Tafsiri ya neno
Umasikini ni ukosefu wa mbinu ya kuchukua pesa toka kwa watu. Watu wanazo pesa unazichukuaje sasa Ili zije kwako, hio ndio inaitwa skills, wape bidhaa, wape huduma, wape connection, nk wao watakupa pesa umasikini kwako utatoweka kupitia ujasiliamali.
Unakuwa masikini sababu umekosa mbinu za kuchukua pesa toka kwa watu,
We bwana wee,soko la ajira ni kama tuu soko la bidhaa zingine,more supply less demand.

Saizi tuu huko mitaani hao hao vijana wachache waliopo wanafanya wanachofanya lakini demand ni ndogo.

Tukienda unavyosema itafika tuu mahali inakuwa kama sasa ambavyo degree ziko kibao Kazi hakuna.

Kila kitu kiwe regulated ndio kitaleta maana.
 
Ina maana watu awali,awanywi,wameacha kuvaa,awanunui sukari,chumvi, sabuni,mafuta, mboga,matofali,mkaa,mafuta ya kula,nk hizi zote ni fursa kwa vijana ndo maana ya VETA kutoa ujuzi wa uzalishaji.
Check gap la mafuta ya kula, vifaa vya ujenzi, nishati bei juu lakini kupitia vyuo vya maarifa watu wanaweza maliza tatizo la bidhaa hizo. Vitu bei juu tafsiri uzalishaji ni mdogo. Hakuna asiyetumia pesa kwa siku kununua bidhaa.
Sekta za madini na kilimo pekee zinafuta tatizo la ajira nchini zikitumika vyema.
 
Leo hii ukitoka Manyara kwenda Arusha maeneo ya Tarangire unashuhudia ujenzi holela wa nyumba hadi kwenye eneo ambalo ndo yalikuwa mapito ya wanyama. Kilimo pia kinafanyika kwa kasi kwenye maeneo haya.
Hawajali hili kwa Sasa, ila baadae zikianza lawama za wanyama kuvamia raia wa hapo ndio utasikia hao raia wamejenga kwenye mapito ya wanyama hivyo wavunjiwe.
 
Back
Top Bottom