Kama JWTZ halitowaomba Radhi Raia wasio na Hatia WALIOTESWA KINYAMA na MP wa Lugalo Juzi, nawashauri walishtaki Jeshi

Kama JWTZ halitowaomba Radhi Raia wasio na Hatia WALIOTESWA KINYAMA na MP wa Lugalo Juzi, nawashauri walishtaki Jeshi

Unaweza kunitajia kifungu Cha kwenye Code of Service Discipline,na kwenye The National defense Act, kinachosema askari anaruhusiwa kupiga raia/Kuvamia mitaani na kupiga watu?
Kama kipo kiweke hapa tukijadili.
Swali Hilo hapo limekushinda,
 
GENTAMYCINE sijapendezwa na Kitendo cha Raia Kato kujichukulia Sheria mkononi na Kumchoma Kisu Afande Lt. Col. Muna na ninalikemea sana.

Ila GENTAMYCINE sijapendezwa na Foolish Approach ya Wanajeshi ( hasa MP wa Lugalo ) ya kuamua Kuvamia hovyo Nyumba za Watu, Kuvunja Milango yao, Kupiga hovyo Watu na hasa hasa Kuwajeruhi vibaya sana Wamama ( tena Watu wazima ) ambao wengi Wao hadi Usiku huu GENTAMYCINE naandika huu Uzi Wanauguza Majeraha yao huku Mmoja wapo alikamatwa na MP hao akiwa Dukani Kwake na kuamrishwa Kuingia Garini huku akiliacha Duka likiwa wazi ambapo Wahuni waliingia na Kuiba Pesa zote za Hesabu na Simu zilizokuweko ndani.

Nijuavyo GENTAMYCINE ni kwamba JWTZ wana Kitengo chao cha Mawasiliano, Mahusiano na Elimu kwa Umma ( Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ) hivyo Kiungwana tu wangejitokeza na Kukiri Mateso haya kufanyika kwa Raia wasio na Hatia na kuomba Radhi ila wamechagua Kunyamaza na pengine hata Kufurahia kilichofanyika

Kuna Taarifa ambazo si nzuri nimezipata Jioni hii ( japo naendelea Kuzithibitisha ) kuwa kuna Wanawake Wawili waliokamatwa Baa ya Igole au ya Bombardier nao Kujumuishwa katika Kundi la Watu 74 Waliokamatwa na kupelekwa Kambini Mwenge kupewa Adhabu Kali za Kijeshi zilizojumuisha Kuchapwa na Virungu na Fimbo Ngumu Migongoni, wakirukishwa Vichurachura, wakibebeshwa Mawe na Kubiringitwa Udongoni Wamekufa ( Wamefariki ) leo.

Na kwa leo Mchana, Alasiri na hata Jioni hii GENTAMYCINE nimeshuhudia Raia kadhaa ( tena Wababa na Wamama ) Watu wazima bila kuwasahau Mabinti wakiwa Wamevimba Miguu, Macho, Ugoko na Pua zao na Wakilalamika sana na Kuhoji Kosa lao hasa hadi Kuteswa na Kupigwa kote kule Juzi Usiku kulikuwa ni nini?

GENTAMYCINE niliamua kwenda mbali zaidi kufanya Mahojiano na baadhi ya Wanasheria ( Mawakili ) juu ya Kilichofanyika na kudai kuwa kilikuwa ni Kinyume na Utaratibu wa Sheria za nchi na kwamba Wahusika wakiungana na kwenda Kushtaki hali itakuwa mbaya Kwao ( JWTZ ) hata kama wale MP wa Lugalo WALIOWATESA KINYAMA RAIA kwa kujua kuwa walichokuwa wanakifanya kilikuwa ni kibaya walivalia Kininja ili kuficha Nyuso zao Wasijulikane.

JWTZ nawapenda ila hapa mmebugi.
Mada chonganishi na huenda unatumiwa au bila kujijua
 
Kama hili swala halitazungumziwa Bungeni ili kutafuta suluhu ya kudumu huko mbele itakuwa ni hatari zaidi kwa raia!
Kwa mfano swala kama hili nadhani jeshi lingefanya upepelezi kwanza bila kutumia nguvu ili kuwabaini watu hao, then ndiyo liendeshe operation ya kuwakamata! Lakini siyo kuvamia makazi ya watu na then kupiga raia hovyo hovyo bila kujali waliomo na wasiokuwemo! Kwa kweli linaogopesha raia.
 
Tunamajeshi ya hovyo sana kwenye hii nchi yani nchi zilizoendelea wanatushangaa sana sasa unaenda kupiga wazee majumbani kisa mwenzao kauwawa hao wazee kosa lao ni nini, istoshe huyo mjeda mwenyewe aliechomwa visu hakua amevaa sare kato alijua nikibaka tu unaendaje kupiga mtu makofi hovyo hata kama ni mm lazima nijihami bora alivyokufa tu iwe fundisho wasipende kujichukulia sheria mkononi.
 
K

Kwa hiyo wapige raia halafu lisijirudie? Kwa I marehemu angeelewana tu na jamaa yangetokea haya? Ujeshi wenu huko huko kambini mkija uraiani nyie ni raia lazima mfuate sheria,taratibu na kanuni za mahala husika.
Ukiwaona huko mtaani JWTZ wakumbushe tu ubabe wenu hukohuko sio hapa mtaani kwetu, watakushukuru sana kwa kuwakumbusha.
 
Kibano kitaendelea hadi jasho liwatoke hakuna atakayewatetea awe wa ndani au nje ili siku nyingine mjifunze.Hata watoto au familia zao hamuwezi kuwafanya lolote.Jifunzeni kuheshimu majeshi yetu, mnanyonyana korodani sababu ya wao kujitoa mhanga usiku na mchana laiti mngejua mazingira wanayofanyia kazi na hawana pahala pa kulalamikia.Next time mjifunze na kuwa na adabu, hiyo ni trailer msiombe picha ianze
Kwa mujibu wa Aristotle jeshi inabidi iwe kazi ya watu wenye akili ndogo na utashi mkubwa. Wewe ni dhihirisho la hiyo theory.
 
Jwtz mnatesa wana Kawe kwa mateso ya Kinyama huku mkijisahau kwamba mmepanga mitaani kwao..ngoja muwekewe sumu kwenye chips na supu za utumbo mnazokunywa mitaani nyie si mnalewa na sisi
 
Kibano kitaendelea hadi jasho liwatoke hakuna atakayewatetea awe wa ndani au nje ili siku nyingine mjifunze.Hata watoto au familia zao hamuwezi kuwafanya lolote.Jifunzeni kuheshimu majeshi yetu, mnanyonyana korodani sababu ya wao kujitoa mhanga usiku na mchana laiti mngejua mazingira wanayofanyia kazi na hawana pahala pa kulalamikia.Next time mjifunze na kuwa na adabu, hiyo ni trailer msiombe picha ianze
mnapiga raia wasio na mafunzo yoyote ndio ndio maana mkikutana na M23 kule DRC mnakula kichapo hadi mnavua gwanda na kukimbia uchi wa mnyama
 
GENTAMYCINE sijapendezwa na Kitendo cha Raia Kato kujichukulia Sheria mkononi na Kumchoma Kisu Afande Lt. Col. Muna na ninalikemea sana.

Ila GENTAMYCINE sijapendezwa na Foolish Approach ya Wanajeshi ( hasa MP wa Lugalo ) ya kuamua Kuvamia hovyo Nyumba za Watu, Kuvunja Milango yao, Kupiga hovyo Watu na hasa hasa Kuwajeruhi vibaya sana Wamama ( tena Watu wazima ) ambao wengi Wao hadi Usiku huu GENTAMYCINE naandika huu Uzi Wanauguza Majeraha yao huku Mmoja wapo alikamatwa na MP hao akiwa Dukani Kwake na kuamrishwa Kuingia Garini huku akiliacha Duka likiwa wazi ambapo Wahuni waliingia na Kuiba Pesa zote za Hesabu na Simu zilizokuweko ndani.

Nijuavyo GENTAMYCINE ni kwamba JWTZ wana Kitengo chao cha Mawasiliano, Mahusiano na Elimu kwa Umma ( Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ) hivyo Kiungwana tu wangejitokeza na Kukiri Mateso haya kufanyika kwa Raia wasio na Hatia na kuomba Radhi ila wamechagua Kunyamaza na pengine hata Kufurahia kilichofanyika

Kuna Taarifa ambazo si nzuri nimezipata Jioni hii ( japo naendelea Kuzithibitisha ) kuwa kuna Wanawake Wawili waliokamatwa Baa ya Igole au ya Bombardier nao Kujumuishwa katika Kundi la Watu 74 Waliokamatwa na kupelekwa Kambini Mwenge kupewa Adhabu Kali za Kijeshi zilizojumuisha Kuchapwa na Virungu na Fimbo Ngumu Migongoni, wakirukishwa Vichurachura, wakibebeshwa Mawe na Kubiringitwa Udongoni Wamekufa ( Wamefariki ) leo.

Na kwa leo Mchana, Alasiri na hata Jioni hii GENTAMYCINE nimeshuhudia Raia kadhaa ( tena Wababa na Wamama ) Watu wazima bila kuwasahau Mabinti wakiwa Wamevimba Miguu, Macho, Ugoko na Pua zao na Wakilalamika sana na Kuhoji Kosa lao hasa hadi Kuteswa na Kupigwa kote kule Juzi Usiku kulikuwa ni nini?

GENTAMYCINE niliamua kwenda mbali zaidi kufanya Mahojiano na baadhi ya Wanasheria ( Mawakili ) juu ya Kilichofanyika na kudai kuwa kilikuwa ni Kinyume na Utaratibu wa Sheria za nchi na kwamba Wahusika wakiungana na kwenda Kushtaki hali itakuwa mbaya Kwao ( JWTZ ) hata kama wale MP wa Lugalo WALIOWATESA KINYAMA RAIA kwa kujua kuwa walichokuwa wanakifanya kilikuwa ni kibaya walivalia Kininja ili kuficha Nyuso zao Wasijulikane.

JWTZ nawapenda ila hapa mmebugi.
Jeshi safiiiiiii sn hivi mnamua mtu nyinyi mnaona amchukui hatua. Jeshi msafishe wahuni wote wadakwe
 
Af nikishakukanda ukaite wenzako? Kwani wanaoanzishaga ugonvi si wanakuaga ivo ivo?

We mp mzima unampiga bibi et kutia adabu, we ni kenge tu, huwezi unesha ubabe kwa bibi au wadada bar wasio na hatia
Unafikiri yana akili ya kuja yenyewe kama yenyewe haya makima ?,utakuta limeandaa kambi nzima eti linaingia kitaa kupambana na raia mmoja
Ndina sana hawa wavaa batiki
 
Chief ebu nenda kawe kawatetee mbona ni jambo rahisi sana!
Pale ukwamani kuna kituo kikubwa cha polisi pia kuna ofisi ya mtendaji wote wapo kimya.
Usalama wamesha tuliza eneo lote la kawe hakuna ujinga wowote unaoendelea huko kila kitu kikoo fresh mishe kama kawa wakulungwa!!
 
Mtagongwa mchakae mbwa nyinyi jaribuni muone, fanyeni km mnajaribu kuvamia kambi na kuanzisha vuruga ndio mtawajua vizuri vamieni kambi kisha ueni wanajeshi hata wawili tu mtaeleza kilichomtoa kanga manyoya watahusishwa hata wasiohusika, mtalia hadi makamasi mtalia hadi mnye na mjinyee pimbi nyinyi, mnaleta dharau kwa majeshi yenu
Kuvamia kambi na mikono mitupu bro hilo haliwezekani,hakuna raia wajinga kama wwe!!
 
Picha unazoziona hapona bus kampuni ya HAPPY NATION (TAIFA LENYE FURAHA)
T 508 EBS
Kampuni hili ni waswahili na walaghai
Kwanini Mnamo tarehe 30.10.2023 nimekata tiketi ya kutoka MOROGORO kwenda MUSOMA na wakakiri ya kwamba ndio mwisho wa Bus lao cha Ajabu nafika MWANZA mjini wanapaki bus lao NATA na kunijibu ya kwamba hawaendi tena MUSOMA
UJUMBE wangu kwa wasafiri wenzangu
Usiwape pesa ya MUSOMA kampuni hili kwani hawa nao ni wezi kama wezi wengine tu tunaowajua
KONDAKTA amekana hata kunirudishia pesa yangu
Kwani nilimwambia nipe nauli yangu ili niendelee na safari
KANIJIBU KWA MAJIVUNO
sikupi chochote wewe potea hapa
Kwani ulilazimishwa kupanda bus hili

NINA mengi juu ya wizi wa kampuni hili juu ya kuwaharibia watu bajeti zao

SASA ni makampuni mawili wezi hasaaa
1.HAPPY NATION
2.SUPER NAJIMUNISA
ila Happy Nation ni mpaka na bus namba hiyo hapo .View attachment 2798432View attachment 2798433
PXL_20231030_191433522.MP.jpg
 
Back
Top Bottom