Mimi ni mkatoliki ila hili tukio la bikira maria kuwatokea watoto wa fatima kule ureno linafikirisha sana.
Kwanza mkuu wa kanisa katoliki yani papa ni Rais wa Vatican pia kama nchi kamili yenye kiti UN. Sasa tukio la kule ureno mwaka 1919 la bikira maria kuwatokea Lucia, Francis na Yasinta sio tukio la mchongo? Kwa maslahi mapana ya kanisa katoliki duniani?
Natambua tukio hili lilitokea Portugal na sio Vatican. Pia natambua mkataba wa Mussolini kuitambua Vatican kama nchi pale Roma Italy. Ila pia tutambue serikali zote duniani zina haya matukio ya kupangwa (staged). La fatima nahisi lilipangwa!
Hili tukio limetokea kwenye community kubwa, lilianza kuwa maarufu mitaani na serikali ya huko ilikuwa haitaki Ukristo kuenea. Serikali ilitumia njia zote kuzuia hizi taarifa na kumuonya paroko wa eneo hilo kulifatilia. Paroko alipowaita watoto kuwahoji aliwaomba wasiendelee kulieneza ili Kanisa lisifungiwe na serikali!
Wakati Paroko na wale watoto wakiendelea na mahojiano wakavamiwa na serikali wote wakakamatwa na Kanisa likafungwa kwa amri ya serikali. Wale watoto wakapelekwa gerezani kuwa interogated na kutishwa kuuawa ila waseme walizusha kutokewa na Bikira Maria!
Moja ya kutaniko la Bikira Maria na wale watoto walimuomba afanye muujiza ili watu waamini. Bikira Maria akawahaidi siku na muda wa kukutana ili afanye huo muujiza. Baada ya shinikizo la wananchi wale watoto wakaachiwa na ikafika hiyo siku!
Siku ya tukio walikusanyika watu zaidi ya 70 elfu kushuhudia vikiwemo vyombo vya habari maarufu huko, viongozi wa serikali ambao walienda ili muujiza usipotokea kama walivyotarajia waongee na wananchi kuacha imani potofu.
Ghafla eneo hilo ilinyesha mvua kubwa, muda ukawa unaenda, watu wakaanza kubeza na wengine kuanza kuamini wale watoto wazushi! Ghafla mvua ikakata na jua kuwaka! , Eneo zima likakauka na watu wote walionyeshewa kukauka kama mvua haikunyesha!
Hapo kidogo watu wakashtuka kinachotokea. Wale watoto pekee wakamuona Bikira Maria na kuanza kuongea nae huku wengine hawaoni wala kuelewa. Baada ya mazungumzo wale watoto waliomba tena muujiza ili waaminike. Ndipo wakaona Bikira Maria akinyoosha mkono kuelekea kwenye jua na ghafla jua huku likizunguka likaanza kushuka kwa kasi duniani!
Kile kitendo kilishuhudiwa na maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa serikali! Watu wote wakaanza kukimbia wengine wakipiga magoti wakifikiri ni mwisho wa dunia. Then lile jua likaanza kurudi mahala pake huku Bikira Maria akitoweka pia. Ndipo tukio hili " Sun miracle" , "Sun dance" likawa kubwa dunia nzima na kuripotiwa na vyombo vya habari ( Picha chache zilizopigwa eneo la tukio zipo google).
Prophecy zote alizosema Bikira Maria kwa wale watoto zilitokea, ikiwemo vita ya dunia kufikia ukomo, Papa kupigwa risasi, lakini pia Papa na maaskofu kutakiwa kufanya ibada maalum kwaajili ya Urusi otherwise huko mbele yatatokea machafuko makubwa ( Hili hakuna Papa aliyetimiza). Yapo mengine yaliyosemwa ila inasemekana Kanisa limegoma kutangazwa ikiwemo kutokea Papa atayekuwa mpinga Kristo.
Hili tukio lilitokea mwaka 1917 lakini Kanisa lilikuja ku approve ni muujiza mwaka 1930.