Naona Kenya imejigeuza jukwaa la kutukania viongozi wa nchi hapo juu, hakuna namna tutashughulika na tabia hiyo?
Kidiplomasia ni kawaida kabisa.
Museveni alifanya harakati Toka Tz, Mandela wa ANC dhidi ya makaburu aliitumia Tz,John Garang alitumia Tz .
Kubwa Kuliko MMIAKA YA 2000'S AGATHON RWASA kiongozi WA Chama Cha upinzani kilichokuwa kinaonekana Cha waasi wa serikali ya Burundi ,maarufu kama F.N.L Paripehutu alikuwa anaishi Tanzania.
Tena alikuwa anaishi kilometa chache Toka Magogoni, Mtaa wa Ohio street, currently Barak Obama Road.
Aliishi Tanzania, kwa uwazi na kufanya harakati ndani ya ardhi ya Tz dhidi ya serikali ya chama tawala wakati huo.
Wewe unawashangaa wakenya??
Unawaonea wivu???
Inawezekana hata sasa Tz kuna wanaharakati wa Rwanda wanaompinga Kagame, au wa nchi nyingine ,wapo kwa siri, wanaweza pewa hata travel documents za Tz kificha utambulisho wao.
Kwenye uwanja wa diplomasia hayo ni mambo ya kawaida sana!!