Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Hawatakuelewa, watu wako bize kummezea mate mlegeza macho kwa udini. Wanapiga nae pambio mnafiki namba moja wa taifa, limbukeni wa madaraka mkojoa kwa kukaa yule. Bullshit.
Mkojoa kwa kukaa Yule [emoji850]SAWA
 
Msome vizuri CAG bila hasira. Hajasema hakuna kilichofanyika, wala hajasema kuna uchafu pote. Tena kasema zaidi ya 80% ya taasisi zina hati safi! Lakini zilizobaki ndizo chafu au zenue mashaka. Bahati mbaya ni kuwa hata miradi yetu kipenzi mingine ina kasoro, ikiwemo shirika la ndege. Sisi wengine tulijua toka mwanzo kuwa ndege hazitatengeneza faida. Ni mashirika machache sana ya ndege yanayotengeneza faida. Kwetu ndiyo kabisa, maana wasafiri na viwanja vyetu vya ndani havitoshi kwa ndege zile, Nje si rahisi kwenda au kushindana, na lilipoongezeka zuio la usafiri kutokana na korona tukaisha kabisa! Ilitakiwa tuambiwe ukweli tu, tungeshazoea. Tulizoea kusifu pasipo sifa, tukiambiwa ukweli huo sasa tunakaidi tu kuupokea.
 
Tunasafari ndefu sana tena sana
 
Na hii ndio shida yenu mnaona waTZ wajinga sana..... Eti kikundi kimelipwa? Kwamba hakuna mtu mwenye uwezo wa kukosoa au kufikiri mpaka alipwe? Hvi CCM mnajiona mnamiliki mawazo yetu kisa propaganda zenu.

1. JPM 2019 alidai ATCL imeingiza mabillion hadi ikatoa gawio sasa leo watu wakiona hasara miaka 5 yote wasicharuke

2. SGR haikukaguliwa sasa leo imegundulika ndani ya 35% za pesa iliyolipwa ilitumia infkated exchange rate na haikua ya siku ya malipo wala ya BOT. Rate ya benki za kibiashara. Sasa hya tungejua bila CAG?

3. Tunaambiwa SGR wafanyakazi wa kigeni hawakuwa na vibali hivyo kukosesha nchi mabillion ya fedha. Furthermore interest rate ilikua inakua kubwa kutokana na fedha kucheleweshwa makusudi.

4. Nyerere Dam ilitumia feasibility/EIA ya mwaka 70 na 80 ila haikufanyila harmonisation kwa standards na sheria za Tanzania za sasa ikiwemo sustainability ya flow ya maji kwa miaka tajwa. Haya yangejulikana lini kama sio CAG kutufungu macho?

5. TGFA iliwahi kukaguliwa? Imegundulika na wao ni liability na hakuna mwenye utaalam na uzoefu kwenye aviation industry. Hya tungeyajua bila CAG?

Kilicho pelekea haya yote ni TRANSPARENCY kutoweka. Kama mambo yangekuwa wazi unadhani kuna mtu angeshtuka? so sad Mzee Mwanakijiji nao wanageuka conspiracy theorists wkt facts zipo mezani
 
uwizi upi? makusanyo Tandahimba stand ambayo hayakupelekwa bank inakuwaje kosa la JPM!!!

haya JPM kaondoka, kaacha serikali yake sio? aliyemtua CAG si ni huyo huyo JPM!!

aisee
Ile trillion 1.5 iliyoliwa na Magufuli na CAG Prof Assad aliiandika kwenye ripot iko wapi
 
KAZI IENDELEE-NENO HILI UKILITAZAMA KWA JICHO LA 3 NI NENO PANA SANA
 
Jf ni great thinkers kweli au baadhi wanaendeshwa na midundo ya ngoma?
Mtu anauliza angewepo Magu report hii angekabidhiwa?
Ishu hapa siyo kukabidhiwa au la bali je report ya CAG ni sahihi na kama ya kupika hizo ofisi zijitokeze kujitetea.
Ifike wakati tukubali kuwa kuna watu walishindwa kuzungumza kwa kuwa:-

1.Hofu ya kupoteza kazi zao.

2.Kuawa au kuwekwa vilema vya maisha.

3.Kupoteza urafiki au undugu na

4.Kupigwa nyundo za uhujumu uchumi,kufungiwa biashara zao au kupotezewa uraia.

Mwisho tukubali kuwa Magufuli alifanya mazuri mengi tu lakini pia alikosea mengi pia ila vyombo vya habari vilimbeba.
 
Kwangu mimi ukimlinganisha mkapa , kikwete na Magufuli bado Magufuli ni best ever na amewaacha mbali hao Marais wengine, Rais anatoa dira na kuanzisha miradi yenye kuliletea faida taifa, katika miradi hiyo kuna chain ndefu ya usimamizi, Rais peke yake hawezi maliza tatizo za rushwa ni lazima team yote uhusike na I we na dira moja katika kupambana na rushwa, kwani Magufuli ni mara ngapi ana msema Jacob kuwa halimashauri bado kuna wizi? mara ngapi kaenda bandari kufufua madudu? ni Magufuli huyo huyo ndie alie zuia ndege isiende nje kupakwa rangi, shida iliyopo Tz ni watu tuna hulka ya wizi na kuoneana huruma, Rais akiwatumbua sisi wananchi tulalamika na kusema Rais anaonea ni mbaguzi, hivyo wezi kupata support na huruma ya wananchi, Magufuli kapigana sana na ufisadi a uwajibikaji kushinda awamu zote zilizopita, tulimuita majina yote mabaya akipigana na ufisadi roho mbaya, tengua tengua , ana pendelea, mkabila hii aina ya kulia lia watanzania we have stop kama tuko serious na nchi.

Na kipindi cha Magufuli tundio tumeona miradi ya maana na yenye pesa mingi , chukulia tu miradi ya kikwete terminal 3 na mwendo kasi phase 1 , udom, mloganzila hizo ni just one project of Magufuli ya upanuzi wa bandari ya Dar ambayo Imegharimu trillion 1.2, hapo hujagusa tril 1.2 miradi ya maji, Radar nne katika airports zetu , anga letu lilikuwa ni giza, sasa miradi kama ya maji kama wizara husika aifuatilii kwa karibu lazima ufisadi utakuwepo tu.
 
Yani we jamaa ni kama mchawi aliyekutwa na ungo uchi wa mnyama katikati ya uwanja wa shule za Kayumba.

Ndo hali yako sa hiz.
 

Mkuu labda kwa kukusaidia na kwa akili ya kawaida tu

Kama wengine wanavyoita ‘Mwendazake’ ( Nafikiri sio neno la kubeza) alijaribu sana kuonyesha mafanikio ya serikali yake (na ambacho sio kitu kibaya) na kuna muda mpaka aliponda tawala zilizopita kwamba zilikuwa wapi kuona mauchafu yote yale aliyoyaona yeye

Ubaya unakuja ni kudhibiti kabisa vyanzo vyovyote vya taarifa kuhusu mapungufu ya serikali yake ukiachia mbali mikutano yake akiwa na msafara kusimamisha watu ili awatatulie shida zao ( ni kujiimarisha kisiasa zaidi hapa) lkn hakukuwa na njia rasmi kama vyombo vya habari / bunge au hata ripoti ya uwazi kama hizi kutoka kwa CAG kuonyesha matatizo ya uongozi na uadilifu (Rushwa, wizi) kwenye ofisi za umma

Hakuna ripoti yoyote itakayo kuja kuwa safi sana ktk awamu hii na zilizopita na zitakazo kuja sema tofauti moja ya msingi kuna awamu wananchi/watu walikuwa wanajua wanapigwa ( hata kama hawana namna) maana taarifa zilikuwa zinatoka hata kabla ya ripoti maalumu ya CAG kutoka na vyanzo ni kuanzia bungeni, vyombo vya habari lkn kwa kama mnavyomwita Mwendazake hakukuwa na taarifa zozote zaidi ya anazotaka/zinazotakiwa kutoka na hapa ndo tofauti ipo kubwa na inafanya watu wawe na hamasa kutoa maoni yao hasi au chanya kwa ripoti hii ya CAG baada ya so called Mwendazake kwenda

Na hili ndo limefanya ripoti hii iwe na msisimko maana kuna dhana ilijengwa kwamba utawala ni msafi na msimamizi yupo makini lkn kwa ujumla sio issue ya mtu mmoja tu hii kubwa kama jamii tunatakiwa tuanze kuona kwamba wizi, rushwa ni tabia mbaya kutoka mioyoni kwetu sio kwa sababu mtu mmoja na kwa kipindi kifupi tu katuaminisha kwamba tabia zetu hizi mbaya kama jamii eti zimekwisha/ zilikwisha
 
Wapinzani wanahusika vp na ripot ya CAG? Mbona mnashindwa kuficha ujinga wenu?
 
Upinzani uko kwenye damu yangu; ila sasa hivi naona kama umepotea maana sijui ni nani amebakia upinzani kweli. Labda tuunde upya kabisa... maana upinzani umekubali jukumu lisilo lao...
Huna upinzani wowote. Hakuna. Wewe opportunist kama hao wengine. Mpinzani hayumbi hivyo uyumbavyo. Consistency hukujaliwa. Flexibility hata kwa mpinzani ipo. Ndio inayoonekana leo na ukasema upinzani umepotea. Jema halipingwi. Kipingwacho ni njia ya kulipata. Kodi ni njema. Ya mabavu hapana. Wenzetu wana vijitabu vya kodi. Kitu, bidhaa na huduma ipi inalipiwa kodi. Formula ni wazi kwa kila kilipiwacho. Unatoka nyumbani na kiasi sahihi cha kulipa. Hakuna mizengwe. Compliance iko juu sana. CAG naye anatufahamisha kodi yetu ilivyotumika kwa usahihi. Sio hayo mambo yako ya kishamba ya kutia shaka ripoti ya CAG.
CAG anakagua na kudhibiti tu mapato na na matumizi ya serkali. Kuna mwenye serkali. CAG sio mhimili. Hata baada ya mwaka mmoja waweza tumbuliwa. Maneno ya busara na hekima yaliyomkaribisha CAG. Mtangulizi wake hakutakiwa na serkali hata na spika aliyemtuma kukagua. Trln 1.5 zikazaa jambo!
 
Hawatakuelewa, watu wako bize kummezea mate mlegeza macho kwa udini. Wanapiga nae pambio mnafiki namba moja wa taifa, limbukeni wa madaraka mkojoa kwa kukaa yule. Bullshit.
kwani wewe mama yako mzazi huwa anasimamaga wakt wakukojoa?

huyo ambaye siyo mnafik na mzalendo, CAG anasemaje juu ya utawala wake?
 
Mkuu kama kujiuzuru si Majaliwa tu hata aliyekuwa makamu wa raisi,wote walikuwa ni timu moja huwezi ukasema sili nyama bali nakunywa mchuzi wa nyama na kwa mpango hata wa kule Zanzibar nae ajiuzuru si ndio wote walikuwa wakisema HAPA KAZI TU hadi akina Ndugai nao waondoke. Hakika nimejifunza kwamba Watanzania si watu wa kuwaamini,kama viongozi wanakuwa vigeugeu namna hii sijui mwananchi wa kawaida hali ikoje kwa maana haelewi kama kweli awaamini viongozi waliopo madarakani au asiwaamini.
 
Ni note kitu kwamba ufisadi kama huu ungelikuwa unafanyika tokea kipindi cha Mkapa hadi JK basi Tanzania ingekuwa mbali sana.
 
Umezungumza jambo zuri sana. Changamoto ni hii, je mfumo huu wa kulindana unaweza kuacha nafasi ya Taifa kupata mtu mwenye sifa ulizoziainisha?
Kwa sasa sidhani kama kuna mfumo unaoweza kutusaidia kumpata kiongozi wa sifa nilizoziainisha. Sidhani kama inawezekana, hata kwa nchi zenye mifumo imara ya uchaguzi, kama Marekani, kumpata kiongozi mwenye haiba fulani consistently. Ndio maana hata wao wanaweza kumuibua Obama awamu fulani, na kumuibua Trump awamu nyingine. Kitu kinachowezekanika kabisa ni kuweka malengo ya nini tunataka kiongozi afanye katika awamu yake ya uongozi, na kufanikiwa au kufeli kwake tumpime kwa malengo hayo. Style yake ya kufikia hayo malengo kama nalo ni miongoni mwa malengo tuliyoyaweka, basi tumwambie in advance. Kama kumbukumbu zangu zipo sawa hivyo ndivyo namna tulivyofanikiwa kumpata JPM. Wananchi tulichoka na ufisadi na uzembe uliokithiri hadi sauti zikasikika, hadi kutoka upinzani, za tunamtaka rais dikteta asiyetizama sura ya mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…