Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Mwanakijiji,
Zamani kuna watu walikuwa wanaitwa Nyumbu, mie nilikuwa sijui, sasa ndiyo nimeamini humu Nyumbu ni hawa wafuasi wa wapinzani, sometimes na wapinzani wenyewe. Kwanza wana attack individual, wanasahau kuwa system ndiyo mbovu. Angalia wamesahau kabisa kuwa Kikwete ndiyo alikuwa mtesaji wao kile kipindi cha awamu ya nne, sasa kawa JPM. Hawajui hao wote ni system ambayo ipo na CCM, na itakuwepo wakati wote.

Pili baada ya kifo cha JPM wanaongea mengi sana, ok I am independent, sikupenda JPM his part of human rights, lakini kwa kazi zake ni nani kama yeye? Sasa angalia Nyumbu wamebadirishiwa "narrative" na hiyo hiyo system kuwa JPM alikuwa fisadi sasa wanaamini na kushangilia ati mnaona? Ukweli upo pale pale CCM na system iliyopo ndivyo ilivyo. Angalia huyu mama Samia, mimi naona ni mama wa Mipasho tu, alikuwa na magufuli pamoja yeye ni VP atajitengaje na yale aliyoyafanya magufuli?? Or let say, JPM was sleeping with the Devil? Unam-support mtu kwa maneno kumbe moyoni sivyo? What I am seeing ni kuwa huyu Mama wa Mipasho na JK were very patient, the Vultures, are Patient Birds. Na kweli sasa wanabadirisha "Narrative" sasa Nyumbu wanashangilia. Hawajui kuwa muda si mrefu watalia.

Halafu kuna Group la tatu, hawa watendaji waliokuwa na JPM, wachumia tumbo. Hawa lazima waonyeshe mwelekeo wao maana lazima wajue watakula wapi. Kama tunavyoona Ngugai, kabadirika ghafla, CAG kabadirika ghafla, HK kabadirika ghafla, Nape katoa makucha, they must show where they are.

"The way the coockie crumbles" JPM itakuwa ndvyo alifikiria alipoona kifo kinakuja, we only live once!!
Umeandika kitu hapa, ninavyofahamu madudu ya ofisi za huko serikalini huwa yapo kila awamu, japo sasa tunaaminishwa yamezidi kwa awamu iliyopita, ningedhani pia kwa uelewa wangu wapinzani sasa waje na solution nini cha kufanya ili kuepuka hiyo situation mbele ya safari, badala yake naona wapinzani wameungana na lile kundi jingine la CCM kumshambulia mwendazake, hapa mwenye akili timamu lazima ujiulize, hawa wapinzani wa sampuli hii lengo lao ni nini hasa?

Wamejisahau wanamshangilia huyu mama tokea aingie ikulu, hata madudu yake yaliyotokea hivi karibuni bado hawajayaona, wao ni kushangilia tu kwa hali hii kwanini tusiendelee kutawaliwa na CCM miaka yote? hii ni kwasababu watu wameacha kufuata akili zao wanafuata za viongozi wao wa mitandaoni ndio maana.

CCM ni wale wale, kulindana kuko pale pale lakini watu wanashangilia tu kwa ufupi wa kumbukumbu zao, baada ya siku kadhaa akili zitawarudia waanze kulia tena, just a matter of time.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ufisadi uliofanyika wakati wa miaka mitano ya Rais Magufuli tunaambiwa ni mkubwa sana. Kwamba, mabilioni ya fedha yameliwa na wajanja na kuwa fedha hizi zimeliwa na watu walioteuliwa na kusimamiwa na Rais Magufuli. Kwa haraka haraka - kama kawaida naona siku hizi - wakosoaji wa Rais Magufuli (na hapa nawazungumzia wale wa kisiasa) wameruka ruka kwa shangwe wakisema "si tuliwaambia!". Na kinachosikitisha kidogo ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wamejitambulisha kuwa ni wapinzani nao wamerukia kwa furaha tu na hata hawajui ni kitu gani wanaandaliwa. Sijui ni nani anayewalengesha hawa lakini kilichofanyika na kinachoandaliwa labda ni cha kutisha zaidi kuliko kilichotokea. Kuna mtu aliuliza (jamaa yangu Philemon Michael) wakati msiba ulipotangazwa maswali ambayo sidhani kama kuna mtu atakuja kuyauliza hadharani au kutaka kuyajibu yaeleweke. Na kuna mtu aliuliza tena wakati CAG amewasilisha Bungeni ripoti yake kwamba je hii ndio ile ile ripoti ambayo kama JPM angekuwa hai angekabidhiwa? Sijui jibu lake... Kama ni ile ile inawezekana hakukuwa na jinsi ripoti hii ingekutana na JPM meza moja... Kama ni nyingine... Magufuli alikuwa sahihi mara ya 1.

Hii miaka mitano tumeshuhudia miradi mikubwa ya kila namna na hata tukajisikia kuwa kuna kifu kinafanyika... lakini leo tunaambiwa lote ni changa la macho. Hizo hospitali hakuna zilizojengwa, hakuna masoko, hakuna vituo vya mabasi, hakuna shule zilizofanyiwa matengenezo makubwa, hakuna hiki wala kile na hata ndege tulizoambiwa zilinunuliwa kwa fedha taslimu kumbe hazikununuliwa... yaani, hata hii SGR na Bwawa la Umeme la Nyerere yote ni geresha tu! Kwamba kote huku watu walikuwa wanakula tu na tunachokiona hakipo na kama hili ni kweli basi Magufuli alikuwa sahihi mara 2.

Lakini kingine ni kuwa baadhi ya watu ambao waliteuliwa na Magufuli, walifanya naye kazi, na waliimba "maendeleo" "maendeleo" na hata kusifia kuwa tumeachiwa "urithi" kumbe si kweli; tumeachiwa madeni na ufisadi. Na kwa vile hakuna anayejitokeza kuwa na ujasiri wa kutetea walichokifanya kwa sababu kuna mtu anaitwa "Mwendazake" ameende na utetezi wake kumbe watu wamelia bure. Leo wengine (kina Ndugai) wanageuka wazi wazi; kumbe walikuwa wanaunga mkono uongo; walikuwa wanashangilia ulaghai, na walikuwa wanaficha ufidadi.. hapa watanyoshewa kidole wote kuanzia aliyekuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri wote (na wengi wamerudi au kuhamishwa) na kwa kweli inawezekana wabunge wote walioweza kuingia wakisimama nyuma ya Magufuli. Kama hili ni kweli kwamba ufisadi umetokea wakati watu wale wale ambao leo wanatufunulia ufisadi huo walikuwepo basi Magufuli alikuwa sahihi mara ya 3.

Swali kubwa ni usahihi gani ambao ninauzungumzia? Mwenye kusoma na aelewe. Kama kinachodaiwa na kushangiliwa leo ni kweli basi nchi haina kitu kingine cha kufanya bali kurudi kwenye uchaguzi mkuu mapema zaidi (labda Oktoba mwaka huu) kusafisha uchafu huu; ili wananchi wasisubiri kupigwa tena miaka mitano ijayo... Kama kina Majaliwa na wenzake wote hawakubaliani na assessment hii ya kuwa wamekuwa ni serikali ya kifisadi basi Waziri Mkuu aongoze kujiuzulu mara moja ili kumpa Rais nafasi kweli ya kuunda serikali anayoitaka ambamo ndani yake asirudi HATA MMOJA ALIYEKUWA NDANI YA SERIKALI YA MAGUFULI. Ndio maana ya KUWAJIBIKA KWA PAMOJA.

Wakitaka kuendelea bila kuwajibika ni lazima kuna kitu kingine kinaandaliwa. Ajenda ya Magufuli haijafa, haitakufa na kwa hakina haitoachwa ife. Maana, kama ufisadi huu umefanyika kwa kiasi hiki basi inawezekana Magufuli alikuwa ni genius aliyepindukia. Yaani, kama ufisadi kama huu ungefanyika wakati wa Mkapa au JK hii nchi ingekuwa mbali sana!
Karibu kufupisha umeandika kitabu
 
Mnajitahidi kupaka rangi kaburi lakini kilichomo ni uozo mtupu.

“Nilibaini kuwa wakala wa ndege za Serikali ililipa bilioni 3.92 Kama gharama za matengenezo makubwa ya ndege. Baada ya ziara nilibaini ndege ilikuwa haifanyi kazi toka 2015.” CAG.
Si alipewa mangi kupiga rangi ndege kwa 500000 vipi tena!
 
Binafsi huyu CAG simuamini kamwe...
Sura yake tu inaonesha hayupo sawa sawa. Hata Mhe. Rais Samia alimwambia aache kujigongagonga ulimi wakati kutoa taarifa, ingawaje yaweza kuwa ni gelesha tu kwani yaweza kuwa ilipangwa hivyo.
 
Wapigaji wamerudi kwa kasi ili mambo yao yaende kazi ni moja kuua legacy yote ya mwendazake alafu waanze kupiga kama ilivyoada
Hii Trailer imewekwa vizuri….behind closed doors. Ajabu usikute wanatucheka sisi….siasa ni Zaidi ya mchezo mchafu.
 
unamalizia certificate wapi?

Kuna kosa miradi kuwa ya JK ikatekelezwa na JPM?? kuwa mkweli hapa...hakuna kosa

Sasa usichokijua mpaka nadhania una risiti mtihani wa form four ni kuwa miradi yote ni dira ya taifa!! iko kwenye ilani ya CCM...hata JK aliikuta ya mkapa, mkapa ya mwisho na hii stigler ni wa Nyerere

kuhamia dodoma ni Nyerere sio?

ila mahospitali, bus stand, busis ni ya JPM

Kingine ambacho nimedhania unarudia mtihani wa form two...umesahau yooote unayosema ya JK ndio hiyo hiyo ya JPM akiwa waziri

Kaombe msamaha kwa mama yako, hakukuzaa mjinga hivi
Kwanza kuhamia dodoma ilikuwa kukurupuka kwa jpm. Ndo Mana hela zote zikaelekezw huko huku ajira zikitoweka maazima. Sema ni hivi jpm alikuwa mtu hatari Sana na alikuwa Yuko radhi watu wote wafe ila yeye apatr ujiko tu. Watu wanasuffer mtaani kwa kukosa ajira miaka yote sita. Hata madaktari ambao tulizoea kipindi Cha jk wanaajiliwa bila kubaki lakini nao wanaendesha bodaboda na anajisifu eti ni rais wa wawanyonge. Mungu asingemchukua au akina jk wasingefanya yao nchi nzima ingejaa wamachinga.
 
Huo ndo mradi wa kishetani ambao hata bunge halijui ila jpm alikuwa anachota hela tu na zingine anaficha. Ana akaunti kibao south africa na ameumbuliwa na cag
Mbona hawakuhoji akiwa hai. Bunge si ni taasisi huru inayojitegemea kuisimamia serikali. Waache akili ya mbuni
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ufisadi uliofanyika wakati wa miaka mitano ya Rais Magufuli tunaambiwa ni mkubwa sana. Kwamba, mabilioni ya fedha yameliwa na wajanja na kuwa fedha hizi zimeliwa na watu walioteuliwa na kusimamiwa na Rais Magufuli. Kwa haraka haraka - kama kawaida naona siku hizi - wakosoaji wa Rais Magufuli (na hapa nawazungumzia wale wa kisiasa) wameruka ruka kwa shangwe wakisema "si tuliwaambia!". Na kinachosikitisha kidogo ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wamejitambulisha kuwa ni wapinzani nao wamerukia kwa furaha tu na hata hawajui ni kitu gani wanaandaliwa. Sijui ni nani anayewalengesha hawa lakini kilichofanyika na kinachoandaliwa labda ni cha kutisha zaidi kuliko kilichotokea. Kuna mtu aliuliza (jamaa yangu Philemon Michael) wakati msiba ulipotangazwa maswali ambayo sidhani kama kuna mtu atakuja kuyauliza hadharani au kutaka kuyajibu yaeleweke. Na kuna mtu aliuliza tena wakati CAG amewasilisha Bungeni ripoti yake kwamba je hii ndio ile ile ripoti ambayo kama JPM angekuwa hai angekabidhiwa? Sijui jibu lake... Kama ni ile ile inawezekana hakukuwa na jinsi ripoti hii ingekutana na JPM meza moja... Kama ni nyingine... Magufuli alikuwa sahihi mara ya 1.

Hii miaka mitano tumeshuhudia miradi mikubwa ya kila namna na hata tukajisikia kuwa kuna kifu kinafanyika... lakini leo tunaambiwa lote ni changa la macho. Hizo hospitali hakuna zilizojengwa, hakuna masoko, hakuna vituo vya mabasi, hakuna shule zilizofanyiwa matengenezo makubwa, hakuna hiki wala kile na hata ndege tulizoambiwa zilinunuliwa kwa fedha taslimu kumbe hazikununuliwa... yaani, hata hii SGR na Bwawa la Umeme la Nyerere yote ni geresha tu! Kwamba kote huku watu walikuwa wanakula tu na tunachokiona hakipo na kama hili ni kweli basi Magufuli alikuwa sahihi mara 2.

Lakini kingine ni kuwa baadhi ya watu ambao waliteuliwa na Magufuli, walifanya naye kazi, na waliimba "maendeleo" "maendeleo" na hata kusifia kuwa tumeachiwa "urithi" kumbe si kweli; tumeachiwa madeni na ufisadi. Na kwa vile hakuna anayejitokeza kuwa na ujasiri wa kutetea walichokifanya kwa sababu kuna mtu anaitwa "Mwendazake" ameende na utetezi wake kumbe watu wamelia bure. Leo wengine (kina Ndugai) wanageuka wazi wazi; kumbe walikuwa wanaunga mkono uongo; walikuwa wanashangilia ulaghai, na walikuwa wanaficha ufidadi.. hapa watanyoshewa kidole wote kuanzia aliyekuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri wote (na wengi wamerudi au kuhamishwa) na kwa kweli inawezekana wabunge wote walioweza kuingia wakisimama nyuma ya Magufuli. Kama hili ni kweli kwamba ufisadi umetokea wakati watu wale wale ambao leo wanatufunulia ufisadi huo walikuwepo basi Magufuli alikuwa sahihi mara ya 3.

Swali kubwa ni usahihi gani ambao ninauzungumzia? Mwenye kusoma na aelewe. Kama kinachodaiwa na kushangiliwa leo ni kweli basi nchi haina kitu kingine cha kufanya bali kurudi kwenye uchaguzi mkuu mapema zaidi (labda Oktoba mwaka huu) kusafisha uchafu huu; ili wananchi wasisubiri kupigwa tena miaka mitano ijayo... Kama kina Majaliwa na wenzake wote hawakubaliani na assessment hii ya kuwa wamekuwa ni serikali ya kifisadi basi Waziri Mkuu aongoze kujiuzulu mara moja ili kumpa Rais nafasi kweli ya kuunda serikali anayoitaka ambamo ndani yake asirudi HATA MMOJA ALIYEKUWA NDANI YA SERIKALI YA MAGUFULI. Ndio maana ya KUWAJIBIKA KWA PAMOJA.

Wakitaka kuendelea bila kuwajibika ni lazima kuna kitu kingine kinaandaliwa. Ajenda ya Magufuli haijafa, haitakufa na kwa hakina haitoachwa ife. Maana, kama ufisadi huu umefanyika kwa kiasi hiki basi inawezekana Magufuli alikuwa ni genius aliyepindukia. Yaani, kama ufisadi kama huu ungefanyika wakati wa Mkapa au JK hii nchi ingekuwa mbali sana!

Tuliambiwa kwamba magufuli alimaliza ufisadi.

Tuliambiwa kwamba tunajenga kwa fedha zetu wenyewe tutembee kifua mbere sisi ni matajri.

Tuliambiwa ATCL inapata faida sana mpaka wakaanza kugawa gawio serikalini.
 
Sura yake tu inaonesha hayupo sawa sawa. Hata Mhe. Rais Samia alimwambia aache kujigongagonga ulimi wakati kutoa taarifa, ingawaje yaweza kuwa ni gelesha tu kwani yaweza kuwa ilipangwa hivyo.
Body language yake tu leaves a lot to be desired....
 
Comment yako nitaisave kwa heshima, vita aliyokuwa anaiongelea Magufuli nimeielewa, kwamba maadaui wengine wapo ndani na huwaoni kutokana na pambio za sifa.

Mfano hai ni Ndugai ambaye jamaa alihakikisha anaheshima ya soko kubwa la kisasa Dodoma, leo atakuambia mzee wetu alishauriwa vibaya, ila fedha za ujenzi ule angepewa aweke kibindoni asilimia kadhaa asingeweza kwenda opposite na mwendazake.

Wanamipango yao ovu sana inakuja, Mungu atunusuru.
Acheni huu ujinga tatizo la jamaa yenu lilikuwa nikujiona Neno lake ni sheria uongozi wa namna hiyo lazima ukubaliane na lawama zote sema wafia Jiwe mnataka kuhamisha magoli tu ukweli nikwamba jamaa yenu Katia hasara Nchi

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ukiweza tuwekee mkataba wa bandari ya Bagamoyo (J.K), at least Magu alikuwa akitupatia hints za mikataba, ule wa madini nilishuhudia live wakiungolea, na mingine mingi.
Kwa heshima yako nitaitafuta nikuwekee hapa au pengine
 
Anachojaribu kusema ni hiki

Kama Magufuli alikuwa nduli, fashisti na fisadi basi alikuwa mzuri. Mtu Fisadi anakwapua pesa halafu anapeleka umeme kila kijiji na Elimu bure nchi nzima na zahanati nchi nzima na miradi ya barabara nk hadi vichochoroni. Mistendi kibao hadi mingine inaitwa stendi ya Ndugai hilo fisadi na fashisti na nduli wananchi tunalikubali sababu lilikuwa linakwapua na kuwapelekea wanyonge miradi kibao.

Lingebaki liendelee kufisadi na kupelekea wanyonge

Haya tunasubiri msio nduli na mafashisti na msio mafisadi tuone kama spidi ya maendeleo kwa wanyonge ya hilo nduli,fashisti na fisadi tuone kama spidi hiyo mtaiweza.Tuone nani zaidi kati ya nduli fashisti na Fisadi Papa Magufuli na ambao sio nani zaidi .Wanyonge ndio watakuwa mahakimu kwa hili
Tatizo mnataka kuongoza Nchi kama mnavyoongoza familia zenu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Subiri kidogo, miradi yote tunayoiona itasimama, ndipo utajua tofauti kati ukweli na uongo. Kati ya Rais na mwimba taarabu.

Awamu zote za marais waislam nchi hii huyumba sana. Subiri tu ujionee.
Tukiwaambia tubadili Katiba mnatoa povu miradi kusimama inawezekana issue ni vipaumbele tungekuwa na Katiba inayoeleweka wala msingejiliza namna hii unalaumu Tawala za Kiislam vipi za kikristo zinazounda vikundi vya wasiojulikana

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom