Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Wewe umeamua kuwa mjinga na sio kuwa watu nafsi zinawasuta

Kwako serikali iliyopita ni JPM!!! sio watendaji sasa hapa usaidiwe nini?

Na hao unaosema wala rushwa si ndio hawa hawa walikuwa madarakani na bado wapo??😜

Shida yako ni uwazi? upi?

umeulizwa hivyo vitu vinajengeka? vipo? vinaonekana? sasa kama mtendaji aliamua kuwa apige kazi na siasa zako weka pembeni...that is a true definition ya mwanaume

Labda na wewe unaungana na wale wajinga wanaodhania JPM alikuwa mpigaji? kwa nguo zile na maisha yale kwake nyumbani mpaka hana paved blocks?

JPM angekuwa mroho wa hela angekuwa tajiri kuliko mengi, bakhresa na manji...kakaa wizara ya ujenzi miaka mingapi?...

sasa huwa tunapenda muwaze pande hizo kuwa HE IS MOTIVE was pure, genuine and good...

ila ukiwasikiliza watanzania kama wewe nchi haiendi mahali hii....he decided is own way.....alifaulu JPM...wala report ya CAG isikupe faraja yoyote
Wote wezi tu msituchanganye buaaaaana
Serikali Awamu ya Pili mpaka Awamu hii sijui ya Tano au ya Sita Watawala wote ni dugu moja hakuna aliye msafi
Jiwe aliwachukulia poa kwa kutumia maneno ya wanyonge maskini etc
 
Miliozoe kupika data

Mfano wakati wa meko tuliambiwa ndege zinaleta faida lakini kumbe limekuwa likitengeneza hasara kwa miaka mitano
 
Why? kwasababu haikuridhishi kama ulivyotaka?

Au haijaenda kama ambavyo marehemu alikuaminisha kua hakuna hasara?
Hakuna, mtanzania anayekubaliana na hizo report. Kama huamini nenda huko Facebook kajioneee, comments zote zinakataaa
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ufisadi uliofanyika wakati wa miaka mitano ya Rais Magufuli tunaambiwa ni mkubwa sana. Kwamba, mabilioni ya fedha yameliwa na wajanja na kuwa fedha hizi zimeliwa na watu walioteuliwa na kusimamiwa na Rais Magufuli.

Kwa haraka haraka - kama kawaida naona siku hizi - wakosoaji wa Rais Magufuli (na hapa nawazungumzia wale wa kisiasa) wameruka ruka kwa shangwe wakisema "si tuliwaambia!". Na kinachosikitisha kidogo ni kuwa hata baadhi ya watu ambao wamejitambulisha kuwa ni wapinzani nao wamerukia kwa furaha tu na hata hawajui ni kitu gani wanaandaliwa. Sijui ni nani anayewalengesha hawa lakini kilichofanyika na kinachoandaliwa labda ni cha kutisha zaidi kuliko kilichotokea.

Kuna mtu aliuliza (jamaa yangu Philemon Michael) wakati msiba ulipotangazwa maswali ambayo sidhani kama kuna mtu atakuja kuyauliza hadharani au kutaka kuyajibu yaeleweke. Na kuna mtu aliuliza tena wakati CAG amewasilisha Bungeni ripoti yake kwamba je hii ndio ile ile ripoti ambayo kama JPM angekuwa hai angekabidhiwa? Sijui jibu lake... Kama ni ile ile inawezekana hakukuwa na jinsi ripoti hii ingekutana na JPM meza moja... Kama ni nyingine... Magufuli alikuwa sahihi mara ya 1.

Hii miaka mitano tumeshuhudia miradi mikubwa ya kila namna na hata tukajisikia kuwa kuna kifu kinafanyika... lakini leo tunaambiwa lote ni changa la macho. Hizo hospitali hakuna zilizojengwa, hakuna masoko, hakuna vituo vya mabasi, hakuna shule zilizofanyiwa matengenezo makubwa, hakuna hiki wala kile na hata ndege tulizoambiwa zilinunuliwa kwa fedha taslimu kumbe hazikununuliwa... yaani, hata hii SGR na Bwawa la Umeme la Nyerere yote ni geresha tu! Kwamba kote huku watu walikuwa wanakula tu na tunachokiona hakipo na kama hili ni kweli basi Magufuli alikuwa sahihi mara 2.

Lakini kingine ni kuwa baadhi ya watu ambao waliteuliwa na Magufuli, walifanya naye kazi, na waliimba "maendeleo" "maendeleo" na hata kusifia kuwa tumeachiwa "urithi" kumbe si kweli; tumeachiwa madeni na ufisadi. Na kwa vile hakuna anayejitokeza kuwa na ujasiri wa kutetea walichokifanya kwa sababu kuna mtu anaitwa "Mwendazake" ameende na utetezi wake kumbe watu wamelia bure. Leo wengine (kina Ndugai) wanageuka wazi wazi; kumbe walikuwa wanaunga mkono uongo; walikuwa wanashangilia ulaghai, na walikuwa wanaficha ufisadi.. hapa watanyoshewa kidole wote kuanzia aliyekuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri wote (na wengi wamerudi au kuhamishwa) na kwa kweli inawezekana wabunge wote walioweza kuingia wakisimama nyuma ya Magufuli. Kama hili ni kweli kwamba ufisadi umetokea wakati watu wale wale ambao leo wanatufunulia ufisadi huo walikuwepo basi Magufuli alikuwa sahihi mara ya 3.

Swali kubwa ni usahihi gani ambao ninauzungumzia? Mwenye kusoma na aelewe. Kama kinachodaiwa na kushangiliwa leo ni kweli basi nchi haina kitu kingine cha kufanya bali kurudi kwenye uchaguzi mkuu mapema zaidi (labda Oktoba mwaka huu) kusafisha uchafu huu; ili wananchi wasisubiri kupigwa tena miaka mitano ijayo... Kama kina Majaliwa na wenzake wote hawakubaliani na assessment hii ya kuwa wamekuwa ni serikali ya kifisadi basi Waziri Mkuu aongoze kujiuzulu mara moja ili kumpa Rais nafasi kweli ya kuunda serikali anayoitaka ambamo ndani yake asirudi HATA MMOJA ALIYEKUWA NDANI YA SERIKALI YA MAGUFULI. Ndio maana ya KUWAJIBIKA KWA PAMOJA.

Wakitaka kuendelea bila kuwajibika ni lazima kuna kitu kingine kinaandaliwa. Ajenda ya Magufuli haijafa, haitakufa na kwa hakina haitoachwa ife. Maana, kama ufisadi huu umefanyika kwa kiasi hiki basi inawezekana Magufuli alikuwa ni genius aliyepindukia. Yaani, kama ufisadi kama huu ungefanyika wakati wa Mkapa au JK hii nchi ingekuwa mbali sana!
Mzee umewaka hasira sana. Pole
 
Wewe umeamua kuwa mjinga na sio kuwa watu nafsi zinawasuta

Kwako serikali iliyopita ni JPM!!! sio watendaji sasa hapa usaidiwe nini?

Na hao unaosema wala rushwa si ndio hawa hawa walikuwa madarakani na bado wapo??[emoji12]

Shida yako ni uwazi? upi?

umeulizwa hivyo vitu vinajengeka? vipo? vinaonekana? sasa kama mtendaji aliamua kuwa apige kazi na siasa zako weka pembeni...that is a true definition ya mwanaume

Labda na wewe unaungana na wale wajinga wanaodhania JPM alikuwa mpigaji? kwa nguo zile na maisha yale kwake nyumbani mpaka hana paved blocks?

JPM angekuwa mroho wa hela angekuwa tajiri kuliko mengi, bakhresa na manji...kakaa wizara ya ujenzi miaka mingapi?...

sasa huwa tunapenda muwaze pande hizo kuwa HE IS MOTIVE was pure, genuine and good...

ila ukiwasikiliza watanzania kama wewe nchi haiendi mahali hii....he decided is own way.....alifaulu JPM...wala report ya CAG isikupe faraja yoyote
Kwa watu wenye akili finyu kama wewe ndiyo maana mwendazake hakuwa na kazi ngumu ya kuwadanganya na kuwatumia kama ngao ni mtetezi wa nyonge.

Kwani wewe unajua mali zake zote zilipo au wewe ulikuwa ndiyo mtunza siri zake.

kuna aina mbili za mataga
Ya kwanza ni wale ambao wanatetea matumbo yao, wanafiki, Mfano HK, Ndugai
Ya pili ni wale ambao hawajielewi(wapumbavu) ndiyo kama wewe
 
Hakuna, mtanzania anayekubaliana na hizo report. Kama huamini nenda huko Facebook kajioneee, comments zote zinakataaa
Ukweli wa report hauangaliwi kwa namna idadi ya watu wengi walivyoipokea

Ukisema tutumie mitandao ya kijamii kama hakikisho la kujua reaction ya watu dhidi ya report ya CAG utafeli kwasababu Kuna mwenzako huko juu kapinga kukubaliana na misimamo ya kimitandao kwa ku refer watu wa twitter juu ya report hiyo
 
Ukisoma mitandao ya kijamii hasa twitter utafikiri kweli hii nchi imeibiwa kila kitu na hakuna kitu kimeachwa, kumbe sio kweli.

Watu wanajifanya kushangaa ATCL kupata hasara, hivi mtu mwenye akili timamu unaweza kushangaa atcl kupata hasara? By the way, ni shirika gani la serikali linalopata faida? Lipi? Mashirika yote ni hasara kila mwaka kuanzia Tanesco, TPDC, TTCL, ATCL, NHC na mengine yote, kwa nini shida iwe kwa ATCL?

Halafu watu wanataka kusema Magufuli ange eliminate rushwa ama wizi wa mali za umma 100%, hilo jambo halipo Duniani. Duniani kote, kuanzia China ambapo kosa la rushwa unaweza kuuwawa ama Marekani ambapo mifumo iko strong bado watu wanaiba na kula rushwa, tusimsingizie Magufuli kwa kila kitu.

Kuna kikundi ama kingenge cha wahuni sijui kinalipwa na nani kutaka kumchafua Magufuli na report ya cag
Tatizo kubwa lilianzia ple Magufuli alipominya uhuru wa mihimili ya serikali kama bunge nk. Pia alizima taasisi ka hizi za mkaguzi mkuu kuwa huru na vyombo vua habari.
 
Usimwamini NDUNGAI MNAFIKI na huyu Mama ambae hana anachojua zaidi ya mipasho na taarab
Mipasho gani mkuu? Au hii ya kutoa Uhuru kwa CAG kufanya kazi yake bila bugudha? Au wewe ulitaka mama aendelee kuficha maovu kana kwamba tupo katika zama za tawala za machifu. Mnaanza kumshambulia mama kwasabu amekuwa muwazi na kiasi fulani ni democratic kitu ambacho nyinyi ambao mmezoea kuishi kwa kunyonganyonga mtakuwa hamna kazi.
 
Mwanakijiji,
Zamani kuna watu walikuwa wanaitwa Nyumbu, mie nilikuwa sijui, sasa ndiyo nimeamini humu Nyumbu ni hawa wafuasi wa wapinzani, sometimes na wapinzani wenyewe. Kwanza wana attack individual, wanasahau kuwa system ndiyo mbovu. Angalia wamesahau kabisa kuwa Kikwete ndiyo alikuwa mtesaji wao kile kipindi cha awamu ya nne, sasa kawa JPM. Hawajui hao wote ni system ambayo ipo na CCM, na itakuwepo wakati wote.

Pili baada ya kifo cha JPM wanaongea mengi sana, ok I am independent, sikupenda JPM his part of human rights, lakini kwa kazi zake ni nani kama yeye? Sasa angalia Nyumbu wamebadirishiwa "narrative" na hiyo hiyo system kuwa JPM alikuwa fisadi sasa wanaamini na kushangilia ati mnaona? Ukweli upo pale pale CCM na system iliyopo ndivyo ilivyo. Angalia huyu mama Samia, mimi naona ni mama wa Mipasho tu, alikuwa na magufuli pamoja yeye ni VP atajitengaje na yale aliyoyafanya magufuli?? Or let say, JPM was sleeping with the Devil? Unam-support mtu kwa maneno kumbe moyoni sivyo? What I am seeing ni kuwa huyu Mama wa Mipasho na JK were very patient, the Vultures, are Patient Birds. Na kweli sasa wanabadirisha "Narrative" sasa Nyumbu wanashangilia. Hawajui kuwa muda si mrefu watalia.

Halafu kuna Group la tatu, hawa watendaji waliokuwa na JPM, wachumia tumbo. Hawa lazima waonyeshe mwelekeo wao maana lazima wajue watakula wapi. Kama tunavyoona Ngugai, kabadirika ghafla, CAG kabadirika ghafla, HK kabadirika ghafla, Nape katoa makucha, they must show where they are.

"The way the coockie crumbles" JPM itakuwa ndvyo alifikiria alipoona kifo kinakuja, we only live once!!
For sure...[emoji120][emoji120]
 
Report zimepikwa, magufuli aliyoyafanya yanaonekana. Wananchi tunayaona. Hivi hii miradi wanadhani imejitengeneza bila fedha?

Oh au ndo hivyo tena marehemu hana haki?
Kumponda mtu aliefanya vitu vinavyoonekana unakuwa unajisumbus bure.

Shame on them.
Rip jpm
 
Binafsi huyu CAG simuamini kamwe.

Mzee wa Hasara [emoji3][emoji3][emoji3]

88825387-64af-4074-b7d0-e3dfe29f30f5.jpg
 
Hata Mimi sijamuelewa kabisa. Kitu ambacho hakijui, unapoandika usiandike kama utakyesoma ni wewe tu, andika ikiwa unazingatia kuwa watasoma wengine.
Pumba mwanzo mwisho.

Wewe ndiyo wa kusemea wenzio kuwa ni Pumba? Ama kweli nyani haoni.......
 
Ni ngumu sana kutegemeaa mabadiliko kupitia ccm..basi tu watanzania hatuelewi
 
Back
Top Bottom