Nazungumzia mfumo Wetu wa uajiri na siasa zetu za vyama namna lilivyoathiri. Ukweli ni kwamba tumeendekeza siasa ambapo chama kilichoshinda Iwe Kwa haki au mizengwe ndio kinaunda serikali na Kuwa na ushawishi kwenye Ajira zote nyeti.
Hatimae kwa takriban miongo mitatu sasa athari iko wazi.
Watu wenye vipawa na uwezo ilimradi sio CCM walikosa kuajiriwa Kwa kigezo sio mwenzetu na hatimae maeneo nyeti yanayohitaji uwezo walipeyana wenyewe Kwa mnasaba Wa kujuana na kisiasa.
Kama taifa, tumepoteza vipawa na rasilimali zetu wenyewe.
Mfumo mzima Wa veting na usalama umeathiriwa na siasa. Siku hizi inatangulizwa siasa kisha kujuana na mwisho uwezo Wa kitaaluma na utendaji.
Walau muongo Wa kwanza Wa vyama vingi 1995 - 2005. Bado tulifaidi uchanga Wa siasa na uongozi Wa kitaifa. Vipawa vilipewa nafasi.
Kadiri siasa ilivyokuwa, ndivyo ufa Wa kupendeleana ulivyozidi na mfumo kuwatenga wengine.
Zanzibar ndio kuliathirika zaidi, na sasa bara nako kumefuata nyayo. Huwezi kuajiriwa sehemu nyeti Kama si mfuasi kindaki ndaki.
Maslahi ya taifa yanaharibiwa na siasa zetu.
Ni wakati sasa Wa kutazamwa hili na kuchukua hatua. Tanzania tutaachwa nyuma Kwa siasa mbaya.
Vijana wangapi Wa upinzani Kwa mfano wameachwa na hali wana uwezo Wa kulisaidia taifa?
Idara nyeti za mifumo ya nchi kumejazwa watu Wa itikadi za CCM na sio itikadi ya Utaifa.
Uajiri Wetu unahitaji mabadiliko. Hapo kuna ulazima Wa kubadilishwa Katiba yetu na mitaala yetu ya Elimu.
Tukubali itikadi ya Utaifa na Umoja Wa kitaifa Katika uonngozi Wa nchi ilk tuondoe ukada katika utendaji na kutumia vipawa vyetu Kwa maslahi ya Taifa.
Tusisubiri kujuta zaidi.
Mbinu za kuuwa upinzani au kushurutishwa kuunga mkono juhudi Ili kupata nafasi ya kutumia vipawa vyetu Ina gharama kubwa kuliko Kuwa na maridhiano ya kitaifa na kubadili Sera zetu.
Siasa sio uadui. Hatukujiandaa na vyama Vingi, Huo ni ukweli. Lakini tusiwe watumwa Wa siasa wakati tuna maelfu ya wasomi na wataalamu Wa kuondoa changamoto hii.
Miongo 3 ya kuendekeza chuki na ubinafsi inatosha.
Tanzania itajengwa na wote.
Kishada.