Kama kuna mwanafunzi anasoma tahasusi CBG na HGE imekula kwake. NECTA yazifuta rasmi

Kama kuna mwanafunzi anasoma tahasusi CBG na HGE imekula kwake. NECTA yazifuta rasmi

CBG hapa wamepuyangaa, ila HGE hata mie nlikua nashangaa inakuajeee.
 
Mmhh mbona wapo wa CBG waliosoma veterinary, pharmacology, nutrition, nursing et al sasa wamefuta ili iweje, au wanataka hadi course kama nutrition na nursing nazo kila mtu ni lazima asome PCB tu basi
 
Nimesoma maoni ya watu wengi humu, kuhusu combination ya cbg, nimegundua waTanzania wengi niwavivu wa kusoma na ufuatiliaji wa mambo wengi mnafikiria ndani ya kile mlichofundishwa tu , cbg inampa mwanafunzi uwanda mpana sana, kuanzia mambo ya aquatic science,environmental science, zoology, botanic science, microbiology, labaratory technology, biotechnology, agricultural science, agribusiness, chemistry, geology and so forth, food science, food processing engineering, kwa kifupi hii ni combination maarufu duniani kote na katika nchi nyingi zilizoendelea watu hawa pia kama wanaufaulu mzuri wa physics o level wanasoma medicine bila shida, tatizo wengi wenu humu mnaenda kama manyumbu, Elimu ina uwanda mpana sana nje ya combination, somo moja tu la natural science mfano biology, chemistry, physics likisimama lenyewe bado linampa mwanafunzi mwangaza mzuri kiutaalamu tofauti na hesabu, historia, so as long as CBG iko na two natural science subjects ni upuuzi wa hali ya juu kuifuta hii combination [emoji108]
 
Back
Top Bottom