Mnafiki Wa Kujitegemea
JF-Expert Member
- Dec 30, 2022
- 3,751
- 6,337
Nashindwa kuacha kushangaa hata mimi mkuu.Cbg wanaweza kuwa waalimu,wanaweza soma a.griculure,food and bioprocess eng food science,kimsingi kufuta hizo kombi ni kukurupuka
Yaani mkuu ndio maana viongozi waropakaji na wakurupukaji km akina Chalamila wataonekana viongozi makini sana nchi hii kwani watoa maoni wengi hasa wanaotetea uamzi huo wanaonekana wamefungiwa ktk kisiwa flani cha mafichoni na wamenyimwa mawasiliano.Nimesoma maoni ya watu wengi humu, kuhusu combination ya cbg, nimegundua waTanzania wengi niwavivu wa kusoma na ufuatiliaji wa mambo wengi mnafikiria ndani ya kile mlichofundishwa tu , cbg inampa mwanafunzi uwanda mpana sana, kuanzia mambo ya aquatic science,environmental science, zoology, botanic science, microbiology, labaratory technology, biotechnology, agricultural science, agribusiness, chemistry, geology and so forth, food science, food processing engineering, kwa kifupi hii ni combination maarufu duniani kote na katika nchi nyingi zilizoendelea watu hawa pia kama wanaufaulu mzuri wa physics o level wanasoma medicine bila shida, tatizo wengi wenu humu mnaenda kama manyumbu, Elimu ina uwanda mpana sana nje ya combination, somo moja tu la natural science mfano biology, chemistry, physics likisimama lenyewe bado linampa mwanafunzi mwangaza mzuri kiutaalamu tofauti na hesabu, historia, so as long as CBG iko na two natural science subjects ni upuuzi wa hali ya juu kuifuta hii combination [emoji108]
Sijui wao wanadhani wale zoologist wamesoma masomo gani sasa wakati ndio wanaochukua mpunga wa kutosha huko TANAPA,maafisa mifugo,uvuvi na kilimo.
Wanaenda mbali zaidi wanasema wanaosoma CBG wanaenda kuwa walimu,sasa unajiuliza kwani kusomea ualimu ni dhambi au huwa wana walazimisha?