Hapa JF kuna watu 'wanajua' mambo mengi sana ya nyuma ya pazia,ila watu 'wasiojua' huingiza ubishi mwingi sana wanapoelezwa kuhusu mambo.(Mfano:kuna watu wakiambiwa kwamba uchawi upo kwenye maisha ya kawaida na kwenye soka,utashangaa mpuuzi mmoja anajitokeza na kusema "hayo mambo hayapo!na yangekuwepo basi sisi Tanzania tungelibeba Kombe la Dunia zamani sana", sasa mjinga kama huyu anayejitia ujuaji unabaki unamchora,ila baadae anakuja kuona matokeo yake).
Nikuulize swali Mkuu:ulishawahi kufatilia nyuzi nyingi za huyu mtoa post hasa kwenye soka letu?
Mimi nilishamwelewa zamani mno,Kuanzia ile mechi ya Simba vs Nkana na kuendelea hadi leo,threads zake huwa zinaleta matokeo aliyotabiri.Labda ya juzi ya Simba vs Al Ahly aliyosema itaisha kwa droo ndo alibugi kidogo.