Kama kweli ni chaguo la Mungu, tusisingizie vita/ tabia nchi

Kama kweli ni chaguo la Mungu, tusisingizie vita/ tabia nchi

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kama title inavyojieleza, hivyo ndivyo ilivyo.

Kama kiongozi wa nchi ni chaguo la Mungu, nchi hiyo itabarikiwa na itastawi. Hakuna sababu ya kusingizia mabadiliko ya tabia nchi, vita nk!

Binafsi kwa kipindi kifupi cha uongozi wake, nimeona mabadiliko makubwa ya tabia nchi tofauti na kipindi cha mtangulizi wake.

Wakati wa utawala wa mtangulizi wake nchi ilistawisha mazao, hapakuwa na ukame wa kutisha kama ilivyo sasa. Huenda ni kwasababu aliwasihi sana wananchi wamtangulize Mungu kwenye kila jambo. Tofauti na sasa inaonesha tunategemea zaidi watu wa kutusaidia kutoka mataifa tajiri!

Nchi haistawi. Malalamiko kila mahali. Hakuna mvua, Mfumuko wa bei, Magonjwa, Mgao wa umeme, maji nk.
Je, ni kweli ni mabadiliko ya tabia nchi au kuna mahali tumemkosea muumba, na hivyo tunapaswa kumrudia ili atuhurumie?

Ukweli ni kwamba, maeneo mengi hali ni mbaya. Mazao yanakauka. Hakujawa na mvua ya kutosha kwa misimu kadhaa! Mito, visima vinakauka!

Je, nini kifanyike? Kama tumeweza kufungua nchi, kwanini tusimuombe muumba wetu atusaidie kufungua anga ilete mvua yenye neema?
 
Mungu hajawahi kupiga kura wala hana Kitambulisho cha Mpiga kura
Huyu ni kiongozi wetu tumemchagua
Itoshe kusema hivyo
 
Samia amekua rais kutokana na Katiba yetu iliyotungwa na wanadamu sio Mungu
Mungu hahusiki, Rais, haya maneno ya kitapeli yalikuwa yanatumika na yule gaidi muuaji tuliyemzika Chato kuhalalisha ugaidi wake
 
Maombi hufanyika baada ya TOBA.

Je wametubu???

Wenye HAKI wakiwa na AMRI watu hufurahi Bali MWOVU atalapo, watu HUUGUA. Mithali 29:2.

Ameeeen.
 
Back
Top Bottom