Kama Lissu anapinga serikali isiweke Kodi yoyote ile kwa wananchi, yeye atatoa hela mfukoni kuendesha nchi?

..hapa unapotosha.

..msimamo wa Lissu ni kwamba ukusanyaji kodi hautakiwi kufukarisha wananchi.

..naomba umsikilize Lissu ktk hotuba yake hapa chini.

..kuanzia dakika 5:15 Lissu anazungumzia masuala ya kodi.

Wewe chawa acha kupotosha lissu hajasema serekali isikusanye kodi bali kodi rafiki kwa wananchi sio zinazo wakomoa wananchi,,,kwani miaka yote tulikua tunaishi kwa kodi ya makato kwenye mitandao??
 
Kwa uelewa wangu, serikali inajiendesha kutokana na Kodi zinazolipwa na wananchi wake.

Katika hotuba ya Lissu, alipinga Kodi zote ambazo serikali inazikusanya na kuzitumia kulipa polisi waliokuwa wanalinda mikutano yake, kujenga uwanja wa ndege, kulipa mishahara, kujenga lami ambayo wafuasi wake Jana walifika mikutanoni bila kuwa na vumbi.

Je, anatuahidi kufuta Kodi zote, nchi ataiendeshaje? Au Ulaya alikokuwa ana wajomba zake ambao wamemuahidi kumpa trilioni mbili Kila mwezi?

Nani asiyejua msululu wa matozo na kodi za hovyo zisizokuwa na u lazima wa kuwepo?

Kwa nini walamba asali hawalipi kodi?

Vipi matumizi mabaya ya kodi zinazokusanywa?

Kulikoni raslimali zetu mapato kupotea?

Bandari, madini, maziwa, bahati, mbuga za wanyama, misitu, nk.

Haitoshi tu na tozo za Mwigulu juu?
 
Wewe chawa acha kupotosha lissu hajasema serekali isikusanye kodi bali kodi rafiki kwa wananchi sio zinazo wakomoa wananchi,,,kwani miaka yote tulikua tunaishi kwa kodi ya makato kwenye mitandao??
Tulia aseme clip hyo hapo juu ni dakika ya ngapi amekataa kodi
 
chiembe
Dingi mbona kimya. Umekimbia thread yako mwenyewe tena au unaandaa uzushi mwingine huko underground
 
Kwa uelewa wangu, serikali inajiendesha kutokana na Kodi zinazolipwa na wananchi wake.

Katika hotuba ya Lissu, alipinga Kodi zote ambazo serikali inazikusanya na kuzitumia kulipa polisi waliokuwa wanalinda mikutano yake, kujenga uwanja wa ndege, kulipa mishahara, kujenga lami ambayo wafuasi wake Jana walifika mikutanoni bila kuwa na vumbi.

Je, anatuahidi kufuta Kodi zote, nchi ataiendeshaje? Au Ulaya alikokuwa ana wajomba zake ambao wamemuahidi kumpa trilioni mbili Kila mwezi?
Haja kataa kodi. Amekataa tozo. Muwe mna tumia akili kwa kichwa na sio. Masaburi
 
Usitupangie jinsi ya kuelewa, kama vile sisi hatuwapangii kuelewa hotuba za CCM
 
Kwa uelewa wangu, serikali inajiendesha kutokana na Kodi zinazolipwa na wananchi wake.

Katika hotuba ya Lissu, alipinga Kodi zote ambazo serikali inazikusanya na kuzitumia kulipa polisi waliokuwa wanalinda mikutano yake, kujenga uwanja wa ndege, kulipa mishahara, kujenga lami ambayo wafuasi wake Jana walifika mikutanoni bila kuwa na vumbi.

Je, anatuahidi kufuta Kodi zote, nchi ataiendeshaje? Au Ulaya alikokuwa ana wajomba zake ambao wamemuahidi kumpa trilioni mbili Kila mwezi?
Kabla ya tozo kodi hazikuwepo? Anachohoji Lisu ni hizi tozo lukuki za Mwigulu
 
Bado maliasili zetu hazijatunufaisha kabisa.....
-Madini
-Mazao ya misitu
-Mazao ya Baharini,Maziwa na mito
-Virgin Land
-Wanyama Pori
-Rasilimali watu nk

Hivyo vyote vikitumika Kwa weledi,hatuna haja ya kukopa na kuomba omba kama Matonya
Umemaliza kazi
 
Usitake kutetea kisichokuwepo. Tozo zililalamikiwa Na watanzania kitambo sana.. Lisu ni mtu mmoja tuu Kati ya maelfu wanaolalamikia hizo tozo.
Hakuna Kodi iliyopokelewa kwa vigelegele, hata wakati mkapa anaweka VAT, sauti za vilio zilivuka mapaa ya mabati
 
Kwa uelewa wangu, serikali inajiendesha kutokana na Kodi zinazolipwa na wananchi wake.

Katika hotuba ya Lissu, alipinga Kodi zote ambazo serikali inazikusanya na kuzitumia kulipa polisi waliokuwa wanalinda mikutano yake, kujenga uwanja wa ndege, kulipa mishahara, kujenga lami ambayo wafuasi wake Jana walifika mikutanoni bila kuwa na vumbi.

Je, anatuahidi kufuta Kodi zote, nchi ataiendeshaje? Au Ulaya alikokuwa ana wajomba zake ambao wamemuahidi kumpa trilioni mbili Kila mwezi?
Nadhani umepotosha kusema kodi zote. Aliongelea tozo.

Lakini kiuhalisia kodi ndogo, huchochea uwekezaji na faida, faida huchochea ongezeko la mtaji, ongezeko la mtaji huchochea upanuzi wa uwekezaji, upanuzi wa uwekezaji, huongeza ajira na vyanzo vya kodi, kuongezeka kwa vyanzo vya kodi na idadi ya walipa kodi, huongeza mapato ya Serikali. Kuongezeka kwa mapato ya Serikali huboreshaji huduma za jamii na miundombinu ya uzalishaji na usafirishaji. Kuboreka kwa miundombinu ya usafirishaji na uzalishaji, hupunguza gharama za uzalishaji na gharama za kuyafikia masoko. Kupungua kwa gharama za uzalishaji na usafirishaji, hupunguza bei ya bidhaa na huleta unafuu kwa mlaji.

Ndiyo maana ukitaka tu kuongeza uwekezaji, cha kwanza kuangalia ni ukubwa na uwingi wa kodi.
 
Kwa uelewa wangu, serikali inajiendesha kutokana na Kodi zinazolipwa na wananchi wake.

Katika hotuba ya Lissu, alipinga Kodi zote ambazo serikali inazikusanya na kuzitumia kulipa polisi waliokuwa wanalinda mikutano yake, kujenga uwanja wa ndege, kulipa mishahara, kujenga lami ambayo wafuasi wake Jana walifika mikutanoni bila kuwa na vumbi.

Je, anatuahidi kufuta Kodi zote, nchi ataiendeshaje? Au Ulaya alikokuwa ana wajomba zake ambao wamemuahidi kumpa trilioni mbili Kila mwezi?
Na wajinga wanamuamini. Likipata hiyo nafasi nalo litajibu: hakuna serikali inayoendeshwa bila kodi. Watanzania hawajamjua Lissu bado. Hatumtakiiiii
 
Back
Top Bottom