Kama mafanikio ya Taifa la Israel kwa sasa kunasababishwa na utukufu wao, Je kipindi walichokuwa wanafeli tuhesabu vipi?

Mafunzo yetu ya Kiiisilamu yanasema Banu Israiil walineemeshwa na Allah.

Which meanz aliwapenda Allah aliwapendelea kuliko jamii zingine za Mashariki ya Kati.
Yah ,wale wa wakati ule walineemeshwa kuliko watu wote wa kwa wakati wao kwani suala la kuletewa Mitume na Manabii miongoni mwao ni neema kubwa kama ilivyokuwa kwetu na ulimwengu kwa ujumla kupata neema ya kuletewa Mtume Muhammad (upon him be peace and blessing of Allah)
 
Waisrael kuwa watumwa katika mataifa mengine isichukuliwe kama ulikuwa unyonge wao, hapana. Wanaisrael kutumikishwa katika mataifa mengine ilikuwa kutimiza malipizi kwa Mungu ili waendelee kuwa na mahusiano mema.

Tunapaswa kutambua kuwa, binadamu (wote) hatuwezi kuwa karibu na Mungu ikiwa tunemkosea kwa kutenda dhambi. Tunapaswa kujisafisha kwanza ndipo tuwe na mahusiano mema na Muumba wetu.

Mungu alitumia kila njia ili kuwasafisha Wanaisrael pale walipomkosea ili kutudisha uhusiano baina yao uliodumu kwa muda mrefu. Hivyo, Wanaisrael kutangatanga kote huko (kama ulivyosema), huko walikuwa wanapelekwa na Mungu ili wakatumikie adhabu na kutubu makosa yao, ili wamrudie Mungu.

Mambo haya yanaweza kuonekana magumu kueleweka, lakini tukijua ukweli kuhusu Waisraeli, inaweza kuwa rahisi kuelewa.

Tukirudi nyuma kidogo kuwajua hawa Wanaisrael, tunaona kuwa, Wanaisrael wanatokana na neno Israel, na Israel ni Yakobo. Kwahivi, Wanaisrael ni kizazi cha Yakobo.

Sasa hebu tuangalie; Yakobo ni nani? Yakobo alikuwa ni mwana wa Isaka. Na Isaka ni nani? Isaka alikuwa ni mwana wa Abram (Abraham). Tukifikia hapa kwa Abraham, sasa tuangalie mahusiano yaliyokuwepo kati ya Mungu na Abraham.

Abraham aliishi maisha yenye kumpendeza sana Mungu. Alikuwa na imani kubwa sana kwa Mungu. Alitoa sadaka kwa ukamilifu kwa Mungu. Itakumbukwa hata alipoambiwa na Mungu amtoe sadaka mwanae wa pekee (Isaka), Abrahamu alitii, lakini baadae Mungu alimpa mwanakondoo, na Isaka kutokutolewa sadaka.

Sasa mambo haya ambayo Abraham aliyaonyesha kwa Mungu, Mungu alifurahishwa nayo na hivyo kumpenda Abraham. Ni katika misingi hii Mungu alimbariki Abraham. Mungu alimwambia Abrahamu; nitakubariki wewe na vizazi vyako.

Kwa hivyo, kama Mungu alimwambia Abrahamu, nitakubariki wewe na vizazi vyako, maana yake, hata hawa Waisrael wa leo, nao wameambulia baraka hizo. Hivyo haya wanayoyafanya leo, Mungu alikwishasema na Abrahamu.

Mungu sio binadamu, ahadi zake ni za kudumu. Mungu anawapigania Wanaisrael kudumisha agano lake kwa Abraham. Nadhani sasa tunaweza kuona mwanga ni kwa nini Waisrael wawe jinsi walivyo.
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] eti Netanyahu hana tofauti na Lewandosky[emoji23][emoji23]
 
Kwa miaka dahari kila mahali walipoka Mayahudi ama waliuwawa, kufukuzwa, au kulazimisha kuwa Wakristu (ref Spanish, Portuguese and Roman Inquisitions)
Baada ya kutua Palestine British Mandate (Israel ) baadaye waziri wake mkuu bi Golda Meir alifichua siri ya mafanikio yao na nchi Ni kwa sababu
"WE HAVE NOWHERE ELSE TO GO.
Wasipo kaza buti hapo wakitimuliwa unadhani wataenda wapi?
 
Mafunzo yetu ya Kiiisilamu yanasema Banu Israiil walineemeshwa na Allah.

Which meanz aliwapenda Allah aliwapendelea kuliko jamii zingine za Mashariki ya Kati.
Ndio ni kweli lakini ni Bani Israeli sio Mayahudi (Watu wanaoguta dini ya Uyahudi) kwa kuwaletea Mitume na Manabii wengi hiyo ni Neema kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…