Habari za muda huu wana JF.
Kumekuwa na mtizamo kuhusu Taifa la Israel watu wakisema ni Taifa la Mungu yaani limeshindikana ulianzishwa nao vita hautashinda sawa unashindana na Mungu ,baadhi ya hoja zinazotumika;
Amezungukwa na maadui pande zote lakini hawamuwezi kila mipango yao kuisambaratisha Israel inafeli vibaya
Mandeleo yao makubwa kisanyansi ,teknolojia na kushikiria sekta nyingi muhimu hapa duniani.
Kushinda vita vyao mara kea mara dhidi ya maadui zao mfano ile vita ya siku sita dhidi ya mataifa mengi ya kiarabu waliyoungana.
Nk
Tukija kihistoria;
Kutokana na mapitio yangu inaonyesha waisrael wanaweza kuwa ni watu waliodhalilishwa na kupitia mateso zaidi katika ulimwengu huu kutokana na matukio matukio mbalimbali yaliyowapitia mfano.
1.Utumwani nchini Misri kuteswa ,kunyanyaswa na kuuliwa watoto wao japo utawala wa Firauni walikuwa mbali zaidi na Mungu kuliko Wana Israeli lakini wao walikuwa watu wa chini
2.Kuna mwamba wa kuitwa Nebuchadnezzar aliwatesa sana ,alivunja mji ,nyumba za ibada ,kufanya mauaji na kuwapeleka utumwani yeye alikuwa hamjui Mungu kama mpagani tu lakini aliwatekeza watu ambao wamewahi kupita Manabii na Mitume wakubwa katika vizazi vyao na kipindi hiko walikuwa na Nabii kama sikosei.
3.Kuvamiwa na kuwa chini ya utawala wa Roman Empire
4.Manyanyaso waliyopitia sehemu walizohamia mfano Ulaya wamepitia udhalili mkubwa na mateso na huko uarabuni waliwahi kuwepo Madina wakafurumushwa .
5.Nk
Swali langu ?
Hawa jamaa na ujiniazi kama tunavyoaminishwa wameshindwa vipi kujiorganize na kuwa na mipango bora kuepukana na mateso yote hayo mpaka kudhalilishwa vibaya na maadui kuwatoa mpaka kwenye makazi yao na kutangatanga ?
Maoni yangu :
Kufanikiwa katika jambo fulani au kushinda sio ishara ya moja kwa moja kuwa wewe unapendwa na Mungu maana watu wanaweza hata kufanya biashara haramu na kuwa mkana Mungu ila akawa na mafanikio makubwa kuliko yule ambaye msafi anayejibidiisha kwa Mungu kwani wakati mwengine inaweza kuwa na mtihani .
#UziTayari
Waisrael kuwa watumwa katika mataifa mengine isichukuliwe kama ulikuwa unyonge wao, hapana. Wanaisrael kutumikishwa katika mataifa mengine ilikuwa kutimiza malipizi kwa Mungu ili waendelee kuwa na mahusiano mema.
Tunapaswa kutambua kuwa, binadamu (wote) hatuwezi kuwa karibu na Mungu ikiwa tunemkosea kwa kutenda dhambi. Tunapaswa kujisafisha kwanza ndipo tuwe na mahusiano mema na Muumba wetu.
Mungu alitumia kila njia ili kuwasafisha Wanaisrael pale walipomkosea ili kutudisha uhusiano baina yao uliodumu kwa muda mrefu. Hivyo, Wanaisrael kutangatanga kote huko (kama ulivyosema), huko walikuwa wanapelekwa na Mungu ili wakatumikie adhabu na kutubu makosa yao, ili wamrudie Mungu.
Mambo haya yanaweza kuonekana magumu kueleweka, lakini tukijua ukweli kuhusu Waisraeli, inaweza kuwa rahisi kuelewa.
Tukirudi nyuma kidogo kuwajua hawa Wanaisrael, tunaona kuwa, Wanaisrael wanatokana na neno Israel, na Israel ni Yakobo. Kwahivi, Wanaisrael ni kizazi cha Yakobo.
Sasa hebu tuangalie; Yakobo ni nani? Yakobo alikuwa ni mwana wa Isaka. Na Isaka ni nani? Isaka alikuwa ni mwana wa Abram (Abraham). Tukifikia hapa kwa Abraham, sasa tuangalie mahusiano yaliyokuwepo kati ya Mungu na Abraham.
Abraham aliishi maisha yenye kumpendeza sana Mungu. Alikuwa na imani kubwa sana kwa Mungu. Alitoa sadaka kwa ukamilifu kwa Mungu. Itakumbukwa hata alipoambiwa na Mungu amtoe sadaka mwanae wa pekee (Isaka), Abrahamu alitii, lakini baadae Mungu alimpa mwanakondoo, na Isaka kutokutolewa sadaka.
Sasa mambo haya ambayo Abraham aliyaonyesha kwa Mungu, Mungu alifurahishwa nayo na hivyo kumpenda Abraham. Ni katika misingi hii Mungu alimbariki Abraham. Mungu alimwambia Abrahamu; nitakubariki wewe na vizazi vyako.
Kwa hivyo, kama Mungu alimwambia Abrahamu, nitakubariki wewe na vizazi vyako, maana yake, hata hawa Waisrael wa leo, nao wameambulia baraka hizo. Hivyo haya wanayoyafanya leo, Mungu alikwishasema na Abrahamu.
Mungu sio binadamu, ahadi zake ni za kudumu. Mungu anawapigania Wanaisrael kudumisha agano lake kwa Abraham. Nadhani sasa tunaweza kuona mwanga ni kwa nini Waisrael wawe jinsi walivyo.