Kama Magufuli alikuwa kichaa kama watu wanavyodai, kwanini Kikwete na Mkapa walimteua kama Waziri?

Kuwa Bora kazini hakuondoi dhana ya mtu kuwa na Afya ya Akili mkuu!Waulize wataalamu wa magonjwa ya Akili watakufafanulia vizuri tuu!
Namjua vizuri Dr Kweka na Muhumbili na nishakutana nae mara mbili kwenye semina zake,ndio maana nikasena hizi chai wakaziuze kwenye vijiwe vya kahawa na hivyo vitini vyao wanavyo viita vitabu.

Au na ww unaamini hizi porojo za kipuuzi?Maana kama undiminished basi na ww unaakili za kushikiwa.
 
Bongo kila kitu kinawezekana.

Hata Kingwendu akijipanga vizuri, kesho anaweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu na mpaka astaafu, atakuwa na PhD za heshima za kutosha kabisa kutoka vyuo vya jalalani, n.k.

Sisi tu ndio tunalialia.
Tunaishi kwenye jamii ya kanyaga twende yaani jamii ya Bora liende ambayo haiwezi kuchakata fikra chanya na hasi pia unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe

Hivi neno: 'Unworking government machinery' hutumika wakati gani
 
Ingekuwa kila issue lazima kuwepo ndiyo tusikie basi hii ingekuwa dunia ya hovyo. Shirikisha ubongo wako, kichwa siyo chungu cha kutunzia mifupa
So kwa hiyo ww unakubali zamani ulikuwa Sokwe? Maana tumeisoma kwenye vitabu au ww unaikubali kama ilivyo.......?

Si shirikishi ubongo wangu kwenye story za kwenye vijiwe vya kahawa kwani upuuzi mtupu.Si wengine hatuna akili za kushikiwa kama nyie ambao mnapelekwa pelekwa kama maboya.
 

Diallo alishathibitisha hilo.
 
Kwa nini Mkapa na Kikwete walimteua kwenye mabaraza yao ya mawaziri?
Hayo wanajua wao wenyewe. Nadhani ungejitafutia wasaa uwaulize wangekupa majibu kwa sababu humu hawapo Ili waweze kutoa majibu ya kwamba kwanini walimteua licha ya kuwa ni kichaa!
Kwakua yeye Mwenyewe alikiri hadharani mbele ya Wananchi kuwa ni kichaa, je Kuna Mtanzania anaweza kumsaidia kukanusha kwamba yeye sio kichaa.?

Hata Job Ndugai ambaye alikua mbunge na Spika wa Bunge alikiri mbele ya Wabunge ambao ni wawakilishi wa Wananchi kuwa yeye ni kichaa na ana faili mirembe. Matendo yake pia yaliweka bayana ukichaa wake mpaka ninyi ndani ya ya chama mkamshinikiza ajiuzulu nafasi ya uspika. Ni aibu kusema aliwahi kufika Galilaya na akakutana na Mkewe Yesu! Au kumfukuza mtu ubunge wakati yupo kwenye matibabu na kusema kabisa hajui alipo na hana taarifa nae.

Unaweza kuona vichaa wawili walipshikilia muhimili ya serikali ya nchi! Hali ilikua mbaya! Kwahiyo tuseme ndani ya chama Kuna vichaa wanaoshika madaraka, na Ndio mana wanafanya mambo ambayo ni ya ajabu Kwa jamii iliyostaarabika kama kuuwa watu na kusema kifo ni kifo.

Ni chama chenye vichaa na wanaweza kushika madaraka, kama mtu anasimama kwenye mimbari na kusema Rais yupo na anachapa kazi vizuri kumbe Rais tayari alishaaga Dunia, hapo utasemaje? Ni vichaa tu hao sio watu wenye akili timamu kama titafsiri ukichaa Kwa muktadha huo! Muone Chalamila kama ni mtu mwenye akili timamu? Mwenyekiti wa Chama alimoiga chini baada ya kuwaambia Wananchi wabebe mabango yenye matusi kumtusi kiongozi, huo ni ukichaa, na baada ya muda akamrudisha kwenye kifo kile kile huku akimsihi ",nadhani sasa umetulia ukafanye kazi"

Kwa hiyo mkuu huko chamani vichaa ni wengi na wanaoshika madaraka ya nchi ni hao hao! Magufuli tu ni miongoni mwao ambaye alishika madaraka makubwa ya nchi. Mama Abdul aliwahi kuwaita Mawazir Stupid, ni kichaa tu anaweza kutukana hadharani na Bado watu hao hao akaendelea kufanya nao kazi, wakati wa dp weld Tulia alizunguka Mbeya akiwatukana wakosoaji wa lile.dubwahsa ambalo wao wenyewe walikiri Lina matatizo kuwaita wapumbavu na kuamrisha vijana wale kuuwa watu watakaokuwa wanakosoa "piteni nao" hii ni kauli ya vichaa tu Wala sio kauli ya mtu alitestaarabika na mwenye akili timamu!

Kwahiyo nadhani umepata majibu kwamba humo chamani Kuna vichaa wengi na Ndio mana wanateuana kushika madaraka ya nchi!
 
So kwa hiyo ww unakubali zamani ulikuwa Sokwe? Maana tumeisoma kwenye vitabu au ww unaikubali kama ilivyo.......?
Unaeza kupiga picha sehemu ya hicho kitabu inayosema binadamu zamani alikua Sokwe? Kama huwezi utakua sehemu ya vichaa vile vile sababu ya kushindwa kufanya uwasilishaji wenye mantiki
 
Alikua mtendaji kinara na ndiye alibeba mawaziri mizigo
Kwamba alikua waziri Mkuu? Na kwamba licha kuwa na Wizara yake alifanya kazi kama kiraka kwenye Wizara nyingine zote? Au aliwahi kuwa waziri asiyekua na Wizara maalum? Ili Yote hayo yatumike kusema kwamba aliwabeba mawaziri mizigo? Afya ya akili Bado ni changamoto kubwa Kwa Taifa
 
Hilo la mtu mwenye faili milembe mbona dogo, tunaweza kusema hawalupitia mafaili yote yavmtu.

Kuna kipindi walisema wameteua Marehemu 😀

Kwa matukio kama haya, bado unashangaa kwann vichaa walipewa madarak 😀
Hahaha Hawa watu hawajikagui!
Kuna wakati watu waliteuliwa na kabla hawajaapa wakatenguliwa! Ni dhahiri kwamba hakuna veting!
 
Unaeza kupiga picha sehemu ya hicho kitabu inayosema binadamu zamani alikua Sokwe? Kama huwezi utakua sehemu ya vichaa vile vile sababu ya kushindwa kufanya uwasilishaji wenye mantiki
Huoni kama na wewe ni kichaa ,maana kwenye elimu ya shule ya msingi katika vitabu vya historia hii topic ipo hata secondary au uliiruka may be na wewe ni kichaa? Sema hatuna tabia ya kuweka vitabu vyetu online ningekuwekea.

Maana unataka kupaka rangi, huo uwasilishaji wenye mantiki upoje?
 
Inadaiwa Magufuli alikuwa na faili lake Mirembe!

Na lilikuwepo toka siku nyingi.

Mirembe ni taasisi ya serikali.

Serikali inaongozwa na CCM.

Walishindwa kuyaona hayo?
Uwezekano ni mkubwa Kwa sababu hawana mfumo imara wa vetting!
Na Hilo Lina ushahidi tu wanapoteua na kitengua Kwa muda mfupi ikiwemo kuteua marehemu!
Magufuli mwenyewe alikiri hadharani kuwa yeye ni kichaa wewe ni nani upinge kauli ya mtu
 
Kama ni kweli alionekana ana tatizo la akili na akapelekwa kutibiwa Ujerumani basi Dialo aliyedai kuwa jamaa ana faili Mirembe alikuwa sahihi. Yaani alitaja Mirembe (kwa sababu ndiyo hospitali maarufu kwa Tanzania kutibu vichaa) kumaanisha kuwa mhusika aliwahi kutibiwa hospitali yoyote inayotibu wagonjwa wenye matatizo ya akili.
 
Una akili gani sasa za kushikiwa?
 
Wakati huu mtu ni rahisi kuyazungumza yanayokuja kichwani mwake
Muhimu ni kuchuja mzungumzaji na anayeongelewa nani kichaa
 
Narudia tembele maktaba ya taaisi ya elimu Tanzania IPO na vitabu vyote hewani bila shida yoyote na u-extract text inayosema : binadamu alitokana na Sokwe. Ukifanya hivyo nitajitoa jamii forums leo. Tafuta maarifa na hapo utajikuta unajisifia umesoma sayansi na huwezi kueleza Darwin theory of emergence of species!
 
Kichaa alikuwa mtendaji kinara na kichaa huyo huyo ndiye aliyewabeba mawaziri mizigo wenye akili timamu?
Yeye mwenyewe ndio alietutangazia kuwa ni kichaa, kwahiyo ukifuatliia matendo yake ndo unaprove ni kweli, akisemacho MTU mwenyewe ndo uhalisia wake
 
Hapa anaongelewa Magu msihamishe mjadala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…