Kama Makamba atatenda anayoyazungumza kuhusu umeme ni jambo la muda, tutarajie umeme bora siku za mbeleni

Kama Makamba atatenda anayoyazungumza kuhusu umeme ni jambo la muda, tutarajie umeme bora siku za mbeleni

Nianze kwakusema mimi ni muhanga wa huu umeme wa Tanzania kwani nilishawahi kupata hasara ya mamilioni mara kwa mara kwasababu ya low voltage.

Mimi ni mjasiliamali mwenye kiwanda kidogo hivyo kutokana na umeme kuwa mdogo ilikua inalazimu kuwasha machine mojamoja kwani mbili kwa wakati mmoja ilikua haiwezekani lakini pia hata kwakuwasha moja bado mota zilikua zinaungua hovyo.

Kuna mzee mmoja mstaafu Tanesco,mzee huyu baada ya kuona kadhia hii akaona anisaidie,mimi nilifikiri kwamba tatizo transformer ni ndogo kumbe sivyo ,ndipo kupitia huyu mzee nilipojua kumbe niliteswa na size ya waya zilizotumika na Tanesco kusambazia kutoka kwenye Transformer kuja kiwandani.

Mzee huyu akaniambia umeme kutoka kwenye transformer kuja kwa mteja unatakiwa usizidi 1km yaani zisizidi nguzo ishirini.Size ya waya akaniambia isipungue 50mm,wakati tanesco walikua wametumia 25mm tena zile zilizopo uchi.Ukifuatilia hata sasa utagundua miradi mingi ya REA wanatumia zaidi 25mm kwenye usambazaji mtaani jambo ambalo ni kosa.

Nilipoenda Tanesco miaka hio nilikosa ushirikiano wakawa wanasumbua na smtz wanataka rushwa,baadae huyu mzee akaona anisaidie Akaenda mwenyewe lakini ilichukia miaka ndipo wakaja kubadilisha kwenye 2015 nakumbuka.

Walipo badili waya tu tatizo likawa historia.

Hapa unajifunza kwamba tunaweza kuwa na umeme mwingi tu kutoka bwawa la mwl Nyerere lakini kama tanesco wasipozingatia standard kwenye kuusambaza umeme bado tutaendela kuteseka.Binafsi naona kitu fulani kwa Makamba.

Jana nimemsikia makamba kipindi cha dk 45 ITV anasema walifanya tafiti kujua matatizo ya umeme nchini.Inawezekana walitumia pesa nyingi sana kufanya hizi tafiti zao.Huyu mzee anasema matatizo ya umeme nchi hii hayahitaji tafiti kwani standard zipo tatizo Tanesco hawazifuatilii.

Ni kweli kupitia huyu mstaafu anayoyasema makamba mimi niliyafahamu toka 2012.

Hata hivyo mh Makamba anatakiwa ajue bado Tanesco wanaendelea kutumia waya nyembamba kwenye usambazaji.Mimi nimeshuhudia line ya usambazaji iliokuja kwangu imejengwa 2021 na waya uliotumika ni 25mm.

Wandengereko wanasema 'zilongwa mbali zitendwa mbali'.Makamba asipokua mkali ataishia maneno mazuri wakati watendaji wake huku chini wanaendelea kuboronga.

Ningeomba tumpe muda makamba anaweza akapunguza matatizo yanayoikumba nchi yetu kwenye umeme.


Asanteni
Apewe muda kwenye hakuna?
 
Kama nilimsikia gharama halisi za kuunganishiwa umeme ni laki 8 (800,000/=) 🤷🏾‍♂️🤷🏾‍♂️🤷🏾‍♂️
 
Hivi ile mikataba aliyoingia hivi karibuni na makampuni ya uarabuni haina capacity charge?iwapo bwana la nyerere likiisha litazalisha umeme wa kutosha kwa nchi.hizo kampuni umeme wao wa gharama juu hawatauza wakati wamewekeza fedha zao zitarudi vipi? Kama sikupitia Capacity charge Kama Richmond,Aggreko nk?ambapo Taifa litapata hasara .
 
Back
Top Bottom