Kama mapenzi hayajawahi kukuumiza jua wewe bado hujakua

Kama mapenzi hayajawahi kukuumiza jua wewe bado hujakua

binafsi nilishawahi kuumizwa ila ni maumivu ya siku moja 2 ikienda sana wiki yameisha nasonga mbele sio yale ya kunifanya nikate tamaa na maisha kabisa nishindwe kula wala kulala.

hio ilikuja baada ya kuwasoma Wanawake akili zao zilivo maana Mwanamke yeye mwenyewe haelewi nini hua kinamfanya anazama kwa Mwanaume ndio maana Mwanamke unaweza ukamnunulia gari ila akampenda aliyemtumia elfu 30 ya kuweka mafuta na akakusaliti.

au ukamjengea nyumba ila akakusaliti na aliyemlipia bill ya maji ya mwezi mmoja.

kifupi Mwanamke ni kiumbe ambaye haeleweki.

Baada ya kusoma mchezo kwanza siwezi kuzama kwa manamke mmoja maana siku akinitema ndio chanzo cha kutaka kujidhuru ndio maana nikaacha kabisa ujinga wa kumuamini Mwanamke 100%.

hio inanifanya nikiwa na Mwanamke nampenda 40% na 60% najali maisha yangu binafsi hio inanifanya niwe mguu ndani mguu nje maswala ya kuzama kwenye mapenzi mzima mzima niliachaga baada ya kusoma mchezo wa mapenzi ulivo wa kifala.

asante kwa kunisikiliza …
 
Kuna tatizo kubwa nimekuwa naliona kwa watu wengi sana.


Jambo likitokea kwa watu wengi mara zote limekuwa likifanywa kuwa ndiyo General Rule over Every Person or Everything Anyhow. iko hivi wakuu, sio wanachopitia au walichopitia wengi basi iwe ni Ndiyo jibu pekee pasiwe na jibu tofauti na hilo la wengi. Haina tofauti na mtu aliyeishi maisha ya kimasikini katika makuzi yake basi akaona yeye pekee ndiye anaeyafahamu maisha vizuri. Umasikini sio sifa wala maumivu hayakufanyi uwe bingwa wa kuyapatia ufumbuzi mambo katika maisha
 
Ukiona nyani mzee jua kakwepa mishale mingi.

Kumcheka au kumdharau mtu aliyeumizwa na mapenzi ni dalili ya immaturity.

Kama hujawahi kuumizwa na mapenzi jua wewe bado hujakua na hata kama umekua hujapevuka yaani unakuwa mtu mkubwa na sio mtu mzima (tofautisha)
Kama hujaumizwa na mapenzi wewe bado unakua bikra moyoni mwako kabisa, ila mkuu hebu tuelezee kidogo kuna mtu yeyote kakucheka ndugu yangu?
 
Kama hujaumizwa na mapenzi wewe bado unakua bikra moyoni mwako kabisa, ila mkuu hebu tuelezee kidogo kuna mtu yeyote kakucheka ndugu yangu?
Kwa kuangalia threads za watu wanaohitaji msaada wa kimawazo baada ya kuumizwa vibaya mno, afu kuna watu wana comment "tafuta hela" au "unaumia kisa mapenzi" nk , hiyo ni sawa na kumcheka mtu
 
Raha ya mapenzi uwe ushapigwa nyundo kama mbili tatu hivi

Huko kunakobaki ni mwendo wa usain bolt tu

Hakueleweki unaingia mitini kabla spana haijahusika
 
Tena usiombe ukaachwa bila taarifa!. Unakomazwa ndani na nje!,halafu Kuna watu wanavipaji huyohuyo aliekuacha bila taarifa anakurudia ukikataa anakuroga!,akishaona limbwata limekolea vizuri ndo anakuacha Sasa na taarifa.. usiombe kuachwa huku limbwata bado linafanya kazi unaweza kuuma Pete ya uchumba ukaimeza mbaya zaidi ukute aliekuacha ni mchawi anajua namna ya ku update limbwata.. mengine mi nimewaachia walimwengu...🤣
Hahhh et ku update limbwata 😂
 
Back
Top Bottom