Mimi nami niongezee hapo kwenye hayo maswali, japo najua kabisa hakuna mwenye majibu zaidi ya talalila;
Kama kweli Mungu anatupenda kama tunavyoaminishwa, kwanini baada ya shetani kuasi akaamua tena kumtupa DUNIANI ambako alijua kabisa kuna viumbe vyake pendwa (sisi) na alijua kabisa huyu jamaa atakuja kutusumbua na kutupotosha? Kwanini hakumtupa hata PLUTO huko au VENUS, JUPITER nk ambako hakuna kiumbe kinachoishi? Yaani ni sawa na wewe upambane na nyoka huko nje, ushindwe kumuua halafu umtupie chumbani kwa watoto! Inaingia akilini?
Halafu huyo nyoka akiwauma watoto, unaanza kuwalaumu tena wale watoto. Kwamba kwanini wamekubali kuumwa na nyoka, unawalaani wao na vizazi vyao vyote, unawaambia waombe msamaha kwako kwa kuumwa na nyoka uliewatupia wewe, la sivyo wakifa utawachoma moto MILELE!!!
Hapa kuna mawili tu;
AMA hizi hadithi za kwenye biblia ni za UONGO kama alfu lela ulela, AU huyo Mungu muweza yote alietuumba na anaetupenda SIO HUYO wa kwenye maandiko!
Usikute hata haya maandiko ni mpango wa shetani kututenganisha na Mungu wa kweli? 🤔 Eeh manake shetani tunaambiwa ana akili sana na yeye ndio mfalme wa dunia so anaweza kufanya chochote.
Nimependa jinsi ulivyoweka mfano wako huu, naomba twende taratibu ndugu najua tutaelewana na kueleweshana wote.
Tukianza na mfano wako wa nyoka, kumbuka wakati baba(Mungu) anapigana na nyoka(shetani) alafu akamtupia kwenye chumba (duniani) kama ulivyosema wewe tambua hakukuwepo watoto( binadamu) wakati ule wakati ugomvi unatokea, watoto walikuja baadae sana baada ya huo ugomvi.
Pili wakati baba(Mungu) alivyo waleta watoto(binadamu) aliwaweka chumba safi sana ambacho huyo nyoka hayupo ila anaweza kufika na asiwafanye chochote hao walioko humo ndani.
Tatu, wakati watoto anawaweka humo ndani aliwaambia kabisa kila kitu ni chema na naomba mtumie kila kilichomo humo ndani ya hicho chumba ila msilale kwenye hilo godoro laleni kwenye ngozi na akawaambia kabisa siku mkilala kwenye hilo godoro mtapata ukurutu.
Nne, wakati watoto wako ndani ya chumba akaja huyo nyoka ambaye ni mgeni machoni pao akawaambia laleni kwenye hilo godoro hamtapata ukurutu na watoto wakatii huyo mgeni licha ya kutokumuona hapo kabla (hapa mgeni hakuwalazimisha hao watoto au kuwashinikiza kulala au kuwalaza kwenye godoro bila wao kujua ila tu ni kwa utashi wao wale watoto walilala wenyewe).
Tano, baada ya yote hayo baba akaamua kuwapa dawa hao watoto kila wakati wajipake ili akija huyo nyoka asiwasogelee wala kuwashambulia
Wale watoto wengine wanajipaka wengine wanaona shida kujipaka ile dawa nyoka akija anawashambulia.
mfano( umepata ajira kanda ya ziwa ambako kitakwimu ni ukanda wa malaria, sasa nikakupa hiyo taarifa na kukupatia dawa ya kutumia ili ukifika ujikinge na mbu wasikuletee malaria ila wewe ukawa unaona usumbufu kutumia ile dawa licha ya kua unayo, baada ya mda ukaugua malaria, je hapo utamlaumu nani? Aliyekupa ajira kanda ya ziwa au wewe uliyeshindwa kutumia dawa ya mbu?)
Naomba tutafakari hili pia
Wewe ni mfinyanzi, ukaamua utengeneze chungu kwa jinsi unavyoona wewe na kwa umbo linalo kuvutia wewe, baada ya kufinyanga na kumaliza ukaamua uweke chungu chako kwenye jua kali, au uoteshee maua au ukitumie kwa jinsi unavyotaka wewe au ukivunje vunje na kukiharibu je chungu kinaweza kukuuliza kwa nini umenifanyia hivi na siyo vile? Jibu ni haiwezekani kwa sababu hakina mamlaka wala hakichagui jinsi ya kutumika.
Kwa maelezo hayo hapo juu ni kwamba sisi wanadamu ( watoto) hatuja chagua sehemu ya kuwekwa hilo litambue ni kwa sababu sisi ni vyungu kwa hiyo hatumpangii yule aliyetuweka huku kwa nini hajatupeleka kwingine ( kitengenezwa hakichagui na akina mamlaka yyt wala nguvu ya kuchagua pa kuwekwa au matumizi) kwa hiyo matumizi yote ya kile chungu inabaki kwa yule aliye kitengeneza
Sasa mpaka leo anayejua kwa nini tuliumbwa na kwa nini tuliletwa huku ambako tunapaona ni sehemu ngumu na yenye vitisho vingi ni yule aliye tufinyanga na ndiye anajua kwa nn ametuweka huku licha ya kuwa kuna vitisho vya yule mwalibifu (nyoka) LAKINI kumbuka ametupa ile dawa ya kutufanya yule nyoka asitusogele, je unaitumia ile dawa au unalaumu baada ya kutokutumia dawa ukang'atwa na yule nyoka?