zipompa
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 11,432
- 24,596
mfano haufananiIpo hivi nitasimulia kwa ufupi sana atakaenielewa anielewe.
Mnaweza mkaishi Baba, Mama na Watoto mkaongeza na mfanyakazi wa ndani, mkaishi kwa furaha tele bila mikwaruzo ya hapa na pale ingawa changamoto za kutokuelewana zikawa hazikwepeki, hapa na pale mkashauriwa aongezeke mtu mwingine wa nne kuja kuweka mambo yenu sawa ili kuwapatanisha akaongezeka mtu wa nne kweli baada ya kipindi kifupi familia ikachangamka furaha ndani ya nyumba neema km zote, kipindi kifupi kikapita akaongezeka mtu mwingine wa tano, sasa unataka kujua Shetani anaonekanaje?
Huyu mtu wa tano yeye kazi yake iliyomleta ndani ya nyumba ni kuvuruga kila alichokikuta mwanzo hatotaka yoyote awepo aliemkuta awe na furaha km aliyomkuta nayo, mfitinishaji, msengenyaji, msema uongo, mkorofishaji, mchonganishi, nk ataanza na ngazi ya chini kwanza ataanza na binti kisha atahamia kwa mpatanishi, ataanza kusema huyu binti hafanyi kazi inavyotakiwa ukiangalia binti mmekaa nae zaidi ya mwaka ila yeye kafika hana hata wiki moja anasema binti huyu mrudiasheni kwao hafai kukaa hapa. Yule mpatanishi aliemkuta anasema nae hafai kukaa hapa bila kujua aliemkuta ndio mpatanishi wa familia. Anaanza kusema huyu mpatanishi aondoke hapa hatakiwi kua hapa si ameshawapatanisha sasa anasubiria nini hapa, bila kujua kwamba mpatanishi yupo kwenye hatua za mwisho za upatanishi kisha aende zake.
Sasa nini kitatokea mpatanishi ataondoka, binti ataondoka familia itabakia haina mshikamano km ilivyokua hapo mwanzo kipindi binti yupo na mpatanishi yupo sababu huyu mtu wa tano hatokaa muda mrefu na yeye mvurugaji ataondoka, unagundua kwamba huyu mtu wa tano ndio maana halisi ya Shetani maana amefika sehemu watu wanaishi vizuri kwa furaha akaamua kuiondoa ile furaha iliyokuwepo hapo awali na kuleta machafuko ya amani na furaha.
Shetani ni mtu yeyote anaeisambaratisha furaha ya watu wengine aidha kwa kujikomba kwa watu wengine ila mwisho wake ni kuiondoa furaha waliyonayo watu wengine au kwa kujipendekeza kwa watu wengine lengo likiwa ni kuiondoa amani na furaha waliyonayo watu wengine, Shetani ni mtu yeyote anaefanya kitu/jambo kwa ajili tu ya kuwaudhi au kuwakwaza watu wengine, huyo ni Shetani, Shetani ni mtu yeyote anaemshawishi mtu mwingine afanye jambo lisilo zuri kwa mtu mwingine ili wakosane na wakishakosana yeye anajitenga mbali km vile sio yeye aliesababisha yote. Shetani anaweza akawa mtu yeyote Babu, Bibi, Mjomba, Shangazi, Kaka, Dada, Binamu, Rafiki, nk.
Wazazi kuweni makini na wageni mnaowakaribisha majumbani mwenu na kuishi nao, wengine mnaowakaribisha na kuishi nao ni mashetani na mnaishi nao bila kujua kua mnaishi na mashetani kwenye nyumba zenu.
Niishie hapa.
Hii ikae hapa sifuti, hutaki utaisoma unataka utaisoma.
kumbuka wakati unamleta mtu wa 5 ulikuwa unafahamu tabia zake na unafahamu yatakayo tokea
kwa nini umlete nyumbani