Kama mbinguni Kuna utakatifu na hakuna dhambi Ibilisi(Shetani) alidanganywa na nani Hadi akaasi?

[7] I form the light, and create darkness: I make peace, and create evil: I the LORD do all these things. [8] Drop down, ye heavens, from above, and let the skies pour down righteousness: let the earth open, and let them bring forth salvation, and let righteousness spring up together; I the LORD have created it.

ISAIAH 45;7
 
Mkuu najua msimamo wako. Sisi tunao amini mungu yupo tunahitaji kujifunza
Mungu unayemwamini yupo ana
a lot of logical Contradictions, logical fallacies and confusion.

Ndio maana unapata ugumu wa kumwelewa na kujifunza. Kwa sababu Mungu huyo ni wa kubuniwa na watu tu ambaye ana mkanganyiko mkubwa sana wa kiimani.

Kiuhalisia Hakuna Mungu.
 
Akili ya Mungu haina kikomo, na akili ya binadamu inakikomo kuelewa mambo yanayomhusu Mungu, inahitaji kumwendea Mungu mwenyewe...kwa unyenyekevu na kicho kuelewa mambo ya kibinadamu mwenye kikomo inahitaji kumwendea binadamu,,,,,,,kamwe usichanganye file kaka.... Mambo ya Mungu usiende kutafuta majibu kwa binadamu hutapata! Swali lako linajibika vzr sana hata sio gumu
 
1. Moja Mungu alijua kuwa shetani ataleta madhara duniani ndo maana akamwambia adam awe makini kuna adui atakuja,,,,,
2. Pili Mungu alijua adam na hawa wataasi ndo maana akaandaa mpango wa ukombozi kabla ya kuumba dunia....


3. Baada ya dhambi kuingia Mungu alikuwa ana dili na njia ya kuondoa dhambi,,,,ili iwe faida kwa mwanadamu....binadamu angekomaa kumua shetani wakati already mwanadamu kaathirika, then anarudi kuua mwanadamu pia....hapa ingekuwa none sense!

4. Yesu alijua kuwa shetani atakuja kumjaribu ndo maana akaenda jangwani,
Umeanza kuona baado kuna safari kumwelewa MUNGU,,,,



kama unataka twende kwa Bible sasa,,, nicheki WhatsApp no 0752377430...Kama unataka kujua...neno la Mungu!!
Bwana hata kuacha, maana anatamani umwelewe!

Naitwa ANCENTY STANSLAUSE, niko DSM
I'm a SEVENTY DAY ADVENTIST.
 
Sasa huo moyo wa dhambi ulitokana na nini ili hali huko binguni wanaishi watakatifu yaani ni mwiko kuwaza maovu. Inamaana Mungu hakujua kuwa atakuja kuasi ili amdhibiti?
Mungu akumnyima mtu uhuru wa kuchagua mema au mabaya akushurutishi au kukulazimisha ummche anasema mbele Yako nimeweka uzima na mauti chagua angekulazimisha angeonekana dikteta kwaiyo amekuacha uchague mwenyewe
 
Nadhani jibu unalo
 
Ume
Umesema jambo zito sana
 
Mungu akumnyima mtu uhuru wa kuchagua mema au mabaya akushurutishi au kukulazimisha ummche anasema mbele Yako nimeweka uzima na mauti chagua angekulazimisha angeonekana dikteta kwaiyo amekuacha uchague mwenyewe
Hujajibu swali langu.

Ikiwa Mungu ni mjuzi wa mema na mabaya kwanini hakujua wala kutambua kuwa huyu kiumbe wake atakuja kuasi nakutaka kumpindua?
 
Karibu utujibu mkuu
 
Yohana 6:70 Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?
 
Unaambiwa ukimchunguza sana kuku hutomla. Mambo ya Mungu hayachunguziki, usiwe na masikio ya utafiti. We amini tu hivyo hivyo kwamba shetani/lusifa aliasi huko mbinguni na akatupwa duniani.
 
Nakupa simple answer ni kuwa Ibilisi alikuwa na KIBURI .Baba yetu Nabii Adam Allah alimuumba akamfanya kama doli au fremu tu kwanza wakati huo ibilisi anliona lile doli na kulichezea na kushangaa hiki kitu gani .Baada ya masiku kupita Allah akalitia ROHO na kuwa binadamu ndio hapo Allah akawapa Amri Malaika wote wamsujudie Nabii Adam Malaika wote wakasujudu ila Ibilisi tu na kiburi chake ndio hapo ugomvi ukaanza baina yetu na Ibilisi.
 
Lakini ungomvi ulianzia mbinguni kabla hajatupwa huku kwa adamu. Je aliwezaje kuasi huko mbinguni na hatimae kutupwa duniani?
 
Unaambiwa ukimchunguza sana kuku hutomla. Mambo ya Mungu hayachunguziki, usiwe na masikio ya utafiti. We amini tu hivyo hivyo kwamba shetani/lusifa aliasi huko mbinguni na akatupwa duniani.
Haya mkuu.lkn vipi tunapoulizwa maswali haya na watoto wetu?
 
Nimependa jinsi ulivyoweka mfano wako huu, naomba twende taratibu ndugu najua tutaelewana na kueleweshana wote.
Tukianza na mfano wako wa nyoka, kumbuka wakati baba(Mungu) anapigana na nyoka(shetani) alafu akamtupia kwenye chumba (duniani) kama ulivyosema wewe tambua hakukuwepo watoto( binadamu) wakati ule wakati ugomvi unatokea, watoto walikuja baadae sana baada ya huo ugomvi.
Pili wakati baba(Mungu) alivyo waleta watoto(binadamu) aliwaweka chumba safi sana ambacho huyo nyoka hayupo ila anaweza kufika na asiwafanye chochote hao walioko humo ndani.
Tatu, wakati watoto anawaweka humo ndani aliwaambia kabisa kila kitu ni chema na naomba mtumie kila kilichomo humo ndani ya hicho chumba ila msilale kwenye hilo godoro laleni kwenye ngozi na akawaambia kabisa siku mkilala kwenye hilo godoro mtapata ukurutu.
Nne, wakati watoto wako ndani ya chumba akaja huyo nyoka ambaye ni mgeni machoni pao akawaambia laleni kwenye hilo godoro hamtapata ukurutu na watoto wakatii huyo mgeni licha ya kutokumuona hapo kabla (hapa mgeni hakuwalazimisha hao watoto au kuwashinikiza kulala au kuwalaza kwenye godoro bila wao kujua ila tu ni kwa utashi wao wale watoto walilala wenyewe).
Tano, baada ya yote hayo baba akaamua kuwapa dawa hao watoto kila wakati wajipake ili akija huyo nyoka asiwasogelee wala kuwashambulia
Wale watoto wengine wanajipaka wengine wanaona shida kujipaka ile dawa nyoka akija anawashambulia.
mfano( umepata ajira kanda ya ziwa ambako kitakwimu ni ukanda wa malaria, sasa nikakupa hiyo taarifa na kukupatia dawa ya kutumia ili ukifika ujikinge na mbu wasikuletee malaria ila wewe ukawa unaona usumbufu kutumia ile dawa licha ya kua unayo, baada ya mda ukaugua malaria, je hapo utamlaumu nani? Aliyekupa ajira kanda ya ziwa au wewe uliyeshindwa kutumia dawa ya mbu?)

Naomba tutafakari hili pia
Wewe ni mfinyanzi, ukaamua utengeneze chungu kwa jinsi unavyoona wewe na kwa umbo linalo kuvutia wewe, baada ya kufinyanga na kumaliza ukaamua uweke chungu chako kwenye jua kali, au uoteshee maua au ukitumie kwa jinsi unavyotaka wewe au ukivunje vunje na kukiharibu je chungu kinaweza kukuuliza kwa nini umenifanyia hivi na siyo vile? Jibu ni haiwezekani kwa sababu hakina mamlaka wala hakichagui jinsi ya kutumika.

Kwa maelezo hayo hapo juu ni kwamba sisi wanadamu ( watoto) hatuja chagua sehemu ya kuwekwa hilo litambue ni kwa sababu sisi ni vyungu kwa hiyo hatumpangii yule aliyetuweka huku kwa nini hajatupeleka kwingine ( kitengenezwa hakichagui na akina mamlaka yyt wala nguvu ya kuchagua pa kuwekwa au matumizi) kwa hiyo matumizi yote ya kile chungu inabaki kwa yule aliye kitengeneza
Sasa mpaka leo anayejua kwa nini tuliumbwa na kwa nini tuliletwa huku ambako tunapaona ni sehemu ngumu na yenye vitisho vingi ni yule aliye tufinyanga na ndiye anajua kwa nn ametuweka huku licha ya kuwa kuna vitisho vya yule mwalibifu (nyoka) LAKINI kumbuka ametupa ile dawa ya kutufanya yule nyoka asitusogele, je unaitumia ile dawa au unalaumu baada ya kutokutumia dawa ukang'atwa na yule nyoka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…