Kama mipakani COVID19 iko hivi, Tanzania yenyewe hali iko vipi?

Kama mipakani COVID19 iko hivi, Tanzania yenyewe hali iko vipi?

Chifyono

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2017
Posts
921
Reaction score
1,659
Habari Wakuu,

Hali ya maambukizi ya corona hapa nchini kwa sasa haifahamiki zaidi ya sintofahamu tu huku watu wakiendelea kufanya shughuli zao kama kawaida

Watanzania tuko njia panda sasa tusielewe hali ya nchi hii kwa vita ya covid19 mpaka kujiuliza maswali kama hali ya mipaka ya nchi iko hivi, Tanzania yenyewe hali hali ikoje? I mean huko Dar es salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha na kwingineko kwingi maambukizi yakoje

Kwa sasa tunashuhudia mipaka ikifungwa na nchi zote jirani kututenga Rwanda, Uganda, Kenya, Zambia zote zimetutenga kwa sababu watanzania tunasambaza corona katika nchi hizo

Tuendelee kujiuliza yaani dereva wa lori ambaye anafika bandari tu kupakia mzigo huku akiwa ajajichanganya sana huko mitaani anapata corona je wale kutwa wanapambana na usafiri wa daladala, mishe za kariakoo, dereva bodaboda watakuwa na hali gani?

Tanzania tuna hali gani ikiwa wasafiri wa malori tu wasio na mizunguko na mchanganyiko mkubwa wa watu wanaathirika vibaya dhidi ya corona?
 
Uwezekano ni kwamba walokwishaambukizwa ni wengi sana ila lwakuwa kinga zao za mwili zinafanya kazi ndipo idadi ya wanaougua haiwi kubwa, kama hao madereva wangekuwa wanaugua hakika wasingeshika usukani kuendesha gari tena umbali mrefu.

Kumbuka hali ya upimaji nchini haiko kwa kasi. Watu wa afya wanapaswa kufanya uchunguzi mpya dhidi ya huu ugonjwa kwani visa vya wabaosemekana kufa nao ni vya ghafla sana.

Jihadhari ugonjwa upo
 
Kwani wewe hujaugua, tathimini anza kuchukua kwako mwenyewe, je unaumwa, familia yako wapo wangapi wagonjwa ndo utajua hali ilivyo mtaani.
 
Idadi ya mazishi kwenye makaburi imeongezeka maradufu haswa jijini Dar

Maeneo ya kuchomea wahindi yako bize sana hapo Dar

Kama huamini nenda kisutu na makabiri mengine kaulize
 
Embu sikilizeni hawa wakenya
Jana nilisikiliza vzr Sana taarifa kilichofanyika hapo 9 Kenyan Drivers were positive while 5 Tanzanian drivers were also positive cha ajabu sasa Wakenya waliruhusiwa kuendelea na Safari lkn Wapendwa Wetu Waliwekwa karatini/Sero nawaasa ndg zangu Charity begins at Dwell.
 
Mkuu mtaani maisha ni Yale yale mtaani kwangu sijashudia mgonjwa wa corona

Ila nikiingia Twitter na jamii forum Ndio Chadema wanaeneza sana uwongo kuhusu corona
Siku baba yako au mama yako akifa ndio utajua kuna corona na hapo ndipo utaacha huu ujinga. Unajua kuna watu kama wewe wataamini kauli zako za kijinga na waje kufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom