Kama mipakani COVID19 iko hivi, Tanzania yenyewe hali iko vipi?

Kama mipakani COVID19 iko hivi, Tanzania yenyewe hali iko vipi?

Habari wakuu
Hali ya maambukizi ya corona hapa nchini kwa sasa haifahamiki zaidi ya sintofahamu tu huku watu wakiendelea kufanya shughuli zao kama kawaida

Watanzania tuko njia panda sasa tusielewe hali ya nchi hii kwa vita ya covid19 mpaka kujiuliza maswali kama hali ya mipaka ya nchi iko hivi, Tanzania yenyewe hali hali ikoje? I mean huko Dar es salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha na kwingineko kwingi maambukizi yakoje

Kwa sasa tunashuhudia mipaka ikifungwa na nchi zote jirani kututenga Rwanda, Uganda, Kenya, Zambia zote zimetutenga kwa sababu watanzania tunasambaza corona katika nchi hizo

Tuendelee kujiuliza yaani dereva wa lori ambaye anafika bandari tu kupakia mzigo huku akiwa ajajichanganya sana huko mitaani anapata corona je wale kutwa wanapambana na usafiri wa daladala, mishe za kariakoo, dereva bodaboda watakuwa na hali gani?

Tanzania tuna hali gani ikiwa wasafiri wa malori tu wasio na mizunguko na mchanganyiko mkubwa wa watu wanaathirika vibaya dhidi ya corona?

MKuu tuongeze dua tu.
 
Juzi siuliona Huwan, Denmark, France shule zinafunguliwa, Italy jana watu wapo nje wameanza kutoka bila vibali league ndio kama hivyo zitaanza kuchezwa Epl, Laliga na Bundesliga.

Trump mwenye analalama tu wako ndani lakini bado wanakufa tu muda sio mrefu atawaachi watu uraiani tutaendelea kuna mikono na kuvaa groves huku tukifanya shughuli zetu tena ndio mm nachokiona maana chanjo hapa mpaka miaka iende ndio tupate.

ndugu wacheni ujinga,
Hizo nchi zote zisha kontrol huu ugonjwa, na wanajua wapi upo na wapi hakuna, nani anao na nani hana, kwasasa maambukizi ni machache na ndio maana wanafikira kufungua badhi ya sehemu.

huku kwetu hakuna takwimu na hakuna anayejua status ya maambukizi ikoje kama inashuka au inapanda.

kifupi tumekwisha.
 
Habari wakuu
Hali ya maambukizi ya corona hapa nchini kwa sasa haifahamiki zaidi ya sintofahamu tu huku watu wakiendelea kufanya shughuli zao kama kawaida

Watanzania tuko njia panda sasa tusielewe hali ya nchi hii kwa vita ya covid19 mpaka kujiuliza maswali kama hali ya mipaka ya nchi iko hivi, Tanzania yenyewe hali hali ikoje? I mean huko Dar es salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha na kwingineko kwingi maambukizi yakoje

Kwa sasa tunashuhudia mipaka ikifungwa na nchi zote jirani kututenga Rwanda, Uganda, Kenya, Zambia zote zimetutenga kwa sababu watanzania tunasambaza corona katika nchi hizo

Tuendelee kujiuliza yaani dereva wa lori ambaye anafika bandari tu kupakia mzigo huku akiwa ajajichanganya sana huko mitaani anapata corona je wale kutwa wanapambana na usafiri wa daladala, mishe za kariakoo, dereva bodaboda watakuwa na hali gani?

Tanzania tuna hali gani ikiwa wasafiri wa malori tu wasio na mizunguko na mchanganyiko mkubwa wa watu wanaathirika vibaya dhidi ya corona?
Hali ni mbaya - majaliwa
DAR watu wanapukutika - Makonda
 
kaka kukaa ndani kazi jamani

kumbuka TZ 80% YA RAIA wanaishi kwa kutegemea kipato cha siku

serikali ina waajiriwa kama laki saba tu, private sector ajira rasmi imeajiri watu milion tatu tu, population yetu ni 56m, ukitoa hawa waajiriwa rasmi wa serikali na private unabaki na watu kama 50m, nusu ya hawa ni wazee na watoto

una watu watu karibu 20m hawana ajira za kueleweka..na wahawa wabeba karibu wategemezi 15m ya wazee na watoto

DSM kwa mfano ina wasiojariwa na sekta sio rasmi kama 2.5 !!!

Lockdown kwetu isingewezekana hata kama JPM angeamua iwepo RAIA wangeingia barabarani, POLISI wanaongeka!!! Kenya polisi wanapewa hela wanaachiwa watu kidogo na maisha yanaendelea

swali ni je mpaka lini watu watakaa ndani??
experts wamekisikia corona inaisha lini?? -Hamna majibu
Juzi usiku saa 6 naangalia news mpaka sasa USA watu wasio na ajila ni 15% kabla ya corona saiz ni 33% mambo yanazidi kuwa magumu tu sasa kama taifa kubwa tu USA wanateseka sisi ni nani tufunge mipaka au tuake ndani?

kuna watu wanaona kinachofanyika ni upumbavu lakini hawajui chochote kuhusu ugonjwa ambao dawa yake ni chanjo na ni muda gani chanjo huchukua kukamilika na kuanza kutumika huchukua nawaona tu wanabwabwaja tu ila saiz kila mtu ataelewa tu vizuri ukweli wa mambo.

maana hakuna chanjo ya mwaka mmoja hizi taarifa tunazopata niza matumaini tu lakini chanjo huchukua miaka 10 kukamilika huko lakini kama hii itakamilika ndani ya muda mfupi basi itakuwa ndio chanjo ya kwanza kukamilika kwa muda mfupi toka dunia ianze kuumbwa lakini pia kumbuka chanjo ya Indonesia ile ya muda mfupi ilivyo uwa watoto na ndio maana watu weupe hawataki vaccines.
 
Ubaya ni uhaba wa taarifa lakini ubaya zaidi ni dhana tunazozitengeza kutokana na taarifa haba.
 
Habari wakuu
Hali ya maambukizi ya corona hapa nchini kwa sasa haifahamiki zaidi ya sintofahamu tu huku watu wakiendelea kufanya shughuli zao kama kawaida

Watanzania tuko njia panda sasa tusielewe hali ya nchi hii kwa vita ya covid19 mpaka kujiuliza maswali kama hali ya mipaka ya nchi iko hivi, Tanzania yenyewe hali hali ikoje? I mean huko Dar es salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha na kwingineko kwingi maambukizi yakoje

Kwa sasa tunashuhudia mipaka ikifungwa na nchi zote jirani kututenga Rwanda, Uganda, Kenya, Zambia zote zimetutenga kwa sababu watanzania tunasambaza corona katika nchi hizo

Tuendelee kujiuliza yaani dereva wa lori ambaye anafika bandari tu kupakia mzigo huku akiwa ajajichanganya sana huko mitaani anapata corona je wale kutwa wanapambana na usafiri wa daladala, mishe za kariakoo, dereva bodaboda watakuwa na hali gani?

Tanzania tuna hali gani ikiwa wasafiri wa malori tu wasio na mizunguko na mchanganyiko mkubwa wa watu wanaathirika vibaya dhidi ya corona?
Kwa hiyo unataka tufanye Nini Ndugu??
 
Hivi chadema walishakulia nini? Kila anayetoa taarifa humu wewe unawaza chadema du! Na unawachukia kweli. Utakuwa unaumia sana juu ya chadema. Si uwe una nyamaza tu. Eti hali mitaani ni kawaida, ndiyo ni kawaida kwakuwa wakubwa wamezuiliwa kupima, lamini wakipima wagonjwa ni zaidi ya elfu 10
Mkuu mtaani maisha ni Yale yale mtaani kwangu sijashudia mgonjwa wa corona

Ila nikiingia Twitter na jamii forum Ndio Chadema wanaeneza sana uwongo kuhusu corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
naona umeambiwa ukweli ndio unakasirika sasa, unaoenda kusikia habari mbaya

kuna ajali, kisukari, ukimwi, covid, cancer n.k na hata wewe baba yako na mama yako watakufa kwa ugonjwa fulani au washakufa

Tanzania msimamoa wake kila mtu anajua kuna corona na tunavaa barakoa, kunawa, sanitizing our hand, social distancing n.k ndio measures ya dunia nzima, na hata uko duniani waliokufa ni so innocent, hawakupenda ila imetokea

umeulizwa swali specific wwe kwa mfano mtaani kwenu hali ikoje??? umeona, sikia au kuona maiti ziko barabarani kwa corona?? wingi wa vifo vya corona tunavipimaje?? maana rate ya kufa kwaida kila siku nchi hata bila corona wanakufa watu si chini ya 200, kila siku kwa sababu zote

posting ya vifo sasa imechagizwa na issues za corona, well

mtaani kwenu hali ikoje??? tupe maelezeo usitishe watu hapa na kutukana
Acha upumbavu. Mtaani kwangu wamekufa wawili na zaidi ya watu watano walikua wanaumwa wamepona. Na pia kuna rafiki yangu arusha amekufa kwa corona. Acheni uchawi wa kuwaambia watu hamna ugonjwa na upo. Semeni ukweli kwa kumuogopa Mungu hata kama unauma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndugu wacheni ujinga,
Hizo nchi zote zisha kontrol huu ugonjwa, na wanajua wapi upo na wapi hakuna, nani anao na nani hana, kwasasa maambukizi ni machache na ndio maana wanafikira kufungua badhi ya sehemu.

huku kwetu hakuna takwimu na hakuna anayejua status ya maambukizi ikoje kama inashuka au inapanda.

kifupi tumekwisha.
Wana control nini? Watu acheni masihara.... Labda ungeniambia wanajaribu.
 
Karibu mtaani halafu baadae uje kupost ulichokiona,huku maisha bado yanaendlea kama kawaida ingawa taarifa za maambukizi hatuzipati lakini maisha ya kawaida yanaendelea mjini kazi kama akawaida ingawa wale watu wa utalii imekula kwetu.
 
Back
Top Bottom